Mwacheni Mungu aitwe Mungu

Mwacheni Mungu aitwe Mungu

Siku utakayonipa ushahidi kwamba hakuna ukoo wa Wachagga wenye miguu mitatu wanaoishi juu ya mlima Kilimanjaro ndiyo siku nitakayokupa ushahidi kwamba mungu hayupo.

Nani alisema hakuna au wapo?
 
Siku utakayonipa ushahidi kwamba hakuna ukoo wa Wachagga wenye miguu mitatu wanaoishi juu ya mlima Kilimanjaro ndiyo siku nitakayokupa ushahidi kwamba mungu hayupo.

Why do you non-theists spend so much time worrying about "a" God you don't even believe exists?
 
Hapa ndipo pa kujiuliza maswali kuhusu hawa watu
Halafu ukiwataka wakupe ushahidi kuwa hakuna Mungu hawakupi wanasema eti wewe uliesema Mungu yupo ndio utoe ushahidi

Kitu ambacho hakipo kitakuwaje na ushahidi wa uwepo wake au kutokuwepo kwake? Sasa wewe unayesema kwamba kipo ndo una jukumu la kutoa huo ushahidi kwa wale ambao hawakioni hicho unachokiona wewe ili na wao waweze kuwa ukurasa mmoja na wewe.

Sasa unajiuliza huyu mtu amewezaje kukataa kuwa hakuna Mungu kama hata ushahidi hana?

Kitu ambacho hakipo ni hakipo tu. Na kwa muktadha wa uwepo wa mungu, mpaka sasa ushahidi wote ambao nimeshauona ni kwamba hauniridhishi wala kunishawishi hata chembe kwamba mungu yupo.

Sasa mimi kama agnostic sikatai kabisa uwepo wake kwani inawezekana kabisa yupo, ila, labda nyie mnaoamini (halafu unajua kwamba huwezi kuthibitisha imani?) hamna ushahidi wa uwepo wake na pengine huo ushahidi mnaodai unathibitisha uwepo wake ni wa uongo au ni finyu na kibaya zaidi labda hata hamlijui hilo.
 
kushangaa kwanini watu wanatumia nguvu nyingi kupinga mungu ambaye hayupo ni upungufu wa fikra.wapo watu wanapaza sauti kueleza kitu fulani kinachoitwa mungu, wanakisifia na kueleza sifa zilizotukuka kuhusu jambo hili.sasa wanatokea watu kuhoji kufananisha na kutafuta uhalisia.
mwisho wanajiridhisha haya yanayosemwa hayalingani na nguvu zinazotumika kulipaisha jambo hili.waaaminio wanawashangaa.ukiwauliza wanajtetea na vitabu na vitabu vyenyewe vipo complecated kinoma.wasioamini wanafanisha na kulinganisha na kuja na jibu hakuna kutu kama hicho.vipi waonekane mapunguani.
kinyume cha ipo ni haipo wanaomini yupo waamini yupo wasioamini vivyo hivyo.halafu mwishoni itafahamika tu.tutakutana huko kama kupo kulingana na mikwala tunayojazwa.
 
Kitu ambacho hakipo kitakuwaje na ushahidi wa uwepo wake? Sasa wewe unayesema kwamba kipo ndo una jukumu la kutoa huo ushahidi kwa wale ambao hawakioni hicho unachokiona wewe ili na wao waweze kuwa ukurasa mmoja na wewe.

Umejuaje kama hicho kitu hakipo bila ya kufanya utafiti? Tuletee utafiti ulio ufanya na kufikia jibu la kitu hicho hakipo. Ndio maana nilikwambia peleke cheap philosophies zako kwa wanao pigania kitu ambacho hakipo.

A thinker wasting her time talking about "kitu ambacho hakipo" Yaaack.
 
Hii umeitoa wapi?

Kwa kuamini kisicho uthibitisho.

Mtu anakwambia "Mimi ndiye taifa teule la mungu, shika kitabu hiki hapa kina instructions kutoka kwa mungu, nifuate mimi na hadithi za taifa langu, usiponifuata wewe ni mjinga, usipomkubali mungu wangu wewe ni mjinga".

Anajua binadamu anaogopa kuitwa mjinga. Kwa hiyo kuweka suala la ujinga ni mtego. Mjanja hataogopa kuitwa mjinga, atachunguza, mjinga wa kweli ataogopa kuitwa mjinga na kukubali bila kuchunguza, hence the insurance policy nature of the clause.

Rudia tena kusoma mfano wa bata huenda ukaelewa vyema!

Mfano wako nimeusoma, nimeuelewa ulivyotaka kuufanya ni jab against me, nikakupiga kile Wajapan wanachokiita Jiu-Jitsu.

Unapigwa kwa ngumi yako mwenyewe. Unafungwa kwa sheria yako mwenyewe.

Who told you so?

I declared, can't you read?

He!
Dakika moja iliyopita umesema wewe ni fool
Sasa unasema "i find a release in being fool"

Kwani hapo wewe umeelewa nini? Hii lugha hii!

Ni wakati gani ulikuwa fool?
Kabla hujaandika haya maelezo yako au baada?

Swali hili halieleweki wala kuwa na mantiki mpaka ujibu umeelewa nini kwa mimi kusema "I find a release in being a fool".

Niambie umeielewaje hiyo sehemu.

Inawezekana ni suala dogo la kuelewa kiingereza tu.
 
Umejuaje kama hicho kitu hakipo bila ya kufanya utafiti? Tuletee utafiti ulio ufanya na kufikia jibu la kitu hicho hakipo. Ndio maana nilikwambia peleke cheap philosophies zako kwa wanao pigania kitu ambacho hakipo.

Ni hivi, wewe unayedai kwamba kipo bado hujanishawishi vya kutosha na kuridhisha kuwa hicho unachoniambia kipo, kipo kweli. Kwa hiyo wala sihitaji kufanya utafiti kufikia jibu langu. Jukumu kubwa unalo wewe unayedai kuwa kipo kunishawishi mimi kwa kutumia ushahidi unaoyapa nguvu madai yako. Hivyo msingi wa mimi kukataa na kusema hakipo ni madai yako wewe pamoja na vizibiti ulivyonipa. Umeelewa?

A thinker wasting her time talking about "kitu ambacho hakipo" Yaaack.

Dhihaka kama hizi hazifanyi madai yako yawe na ushawishi. Usipoteze muda wako kudhihaki watu ambao wanakataa na kutilia shaka madai yako. Washinde na washawishi kwa hoja zenye nguvu na si viroja. Sawa Bw. Maxshimba?
 
Kitu ambacho hakipo kitakuwaje na ushahidi wa uwepo wake au kutokuwepo kwake?

Hakipo kwa mujibu wa nini/nani?
Sasa wewe unayesema kwamba kipo ndo una jukumu la kutoa huo ushahidi

Sasa wewe unabisha kwa sababu ipi?
Halafu hilo jukumu ni nani amenipa?
kwa wale ambao hawakioni hicho unachokiona wewe ili na wao waweze kuwa ukurasa mmoja na wewe.

Kisichoonekana hakipo?

Kitu ambacho hakipo ni hakipo tu.

Kwa ushahidi gani?
Na kwa muktadha wa uwepo wa mungu, mpaka sasa ushahidi wote ambao nimeshauona ni kwamba hauniridhishi wala kunishawishi hata chembe kwamba mungu yupo.

Ushahidi gani?
Wa Mungu gani?
Haukuridhishi au unadhani haukuridhishi?

Sasa mimi kama agnostic sikatai kabisa uwepo wake kwani inawezekana kabisa yupo,
ila, labda nyie mnaoamini (halafu unajua kwamba huwezi kuthibitisha imani?) hamna ushahidi wa uwepo wake
na pengine huo ushahidi mnaodai unathibitisha uwepo wake ni wa uongo au ni finyu na kibaya zaidi labda hata hamlijui hilo.
Kitu ambacho hakipo ni hakipo tu.
Kitu ambacho hakipo kitakuwaje na ushahidi wa uwepo wake au kutokuwepo kwake?

Hizi kauli sijui ni za viroba?
Hazieleweki kabisa
Mara Mungu hayupo
Mara inawezekana yupo
Mara haiwezekani kuthibitisha
Khaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!:heh::heh::heh::heh:
 
kushangaa kwanini watu wanatumia nguvu nyingi kupinga mungu ambaye hayupo ni upungufu wa fikra.wapo watu wanapaza sauti kueleza kitu fulani kinachoitwa mungu, wanakisifia na kueleza sifa zilizotukuka kuhusu jambo hili.sasa wanatokea watu kuhoji kufananisha na kutafuta uhalisia.
mwisho wanajiridhisha haya yanayosemwa hayalingani na nguvu zinazotumika kulipaisha jambo hili.waaaminio wanawashangaa.ukiwauliza wanajtetea na vitabu na vitabu vyenyewe vipo complecated kinoma.wasioamini wanafanisha na kulinganisha na kuja na jibu hakuna kutu kama hicho.vipi waonekane mapunguani.
kinyume cha ipo ni haipo wanaomini yupo waamini yupo wasioamini vivyo hivyo.halafu mwishoni itafahamika tu.tutakutana huko kama kupo kulingana na mikwala tunayojazwa.

Unajua hivyo wanavyoita "vitabu vitakatifu" ni wizi wa kazi za jamii za kale za Kimisri, kigiriki, kiasyria, etc. Na ndio maana hata Muhamad naye alichofanya ni kudesa tu toka Agano la Kale la Wayahudi akaja na madai kwamba kashushiwa aya! Swali rahisi nililowauliza waumini wa dini hizi, inakuwaje kwamba mie msukuma nilaaniwe na kuhukumiwa kwa dhambi ya asili aliyoitenda Adam na Eve? Babu yangu Masalakulangwa alikuwa na uhusiano gani na watu hao? Hakuna jibu la kueleweka.

Huko Ulaya watu wengi wamegundua kamba na utapeli mwingi katika hicho kitabu...ndio sababu hawashoboki tena na habari za masimulizi ya wayahudi...wamebaki watu wa Mashariki ya Kati waliodesa kutoka wa jirani zao wayahudi...kila siku wanauana kwa ajili ya Mungu...na cha ajabu inakuwaje Mungu wa waarabu atofautiane sana na Mungu wa wayahudi ilhali wote wanasema Mungu ni mmoja na Yesu/Isa ni mwana (Mungu Mtu)/mtume wake? Hapo utawaona jinsi watakavyobishana wao kwa wao na kuanza matusi ambayo hjawahi kuyasikia!
 
Dude ( Eiyer ) does not get the concept of "let a = b" while solving an equation.

Wala "for the sake of argument" katika ungwini.

Ukisema "let a = b" au "let's say god exists" ushamchanganyaaa!

Hivi simultaneous equation ulifanya wewe?
 
Hakipo kwa mujibu wa nini/nani?

Kwa mujibu wa vizibiti vyako na vya wenzako wenye imani moja na wewe.

Sasa wewe unabisha kwa sababu ipi?

Kwa sababu ya wanaoamini kushindwa kutoa ushahidi wa kutosha, kuridhisha, na kunishawishi.

Halafu hilo jukumu ni nani amenipa?

Umejipa mwenyewe kwa kudai kuwa mungu yupo.

Kisichoonekana hakipo?

Hapana, lakini kama binadamu tuna njia tano za utambuzi nazo ni; kuona, kunusa, kuonja, kugusa, na kusikia. Ushuzi hauonekani lakini mtu akiuachia penye watu, kama hao watu pua zao hazina mushkili, basi wataitambua harufu kwa kunusa kupitia pua zao.

Kwa ushahidi gani?

Kwa ushahidi wa njia tano za utambuzi.

Ushahidi gani?

Rejea hapo juu

Wa Mungu gani?

Yule muweza wa yote, mwingi wa rehma, huruma, baraka, na BS zingine kama hizo.

Haukuridhishi au unadhani haukuridhishi?

Hauniridhishi.

Hizi kauli sijui ni za viroba?
Hazieleweki kabisa
Mara Mungu hayupo
Mara inawezekana yupo
Mara haiwezekani kuthibitisha
Khaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!:heh::heh::heh::heh:

Kama huelewi jambo omba ueleweshwe maana yawezekana ni uwezo wako wa kuelewa ndiyo tatizo. Sawa?
 
Dude ( Eiyer ) does not get the concept of "let a = b" while solving an equation.

Wala "for the sake of argument" katika ungwini.

Ukisema "let a = b" au "let's say god exists" ushamchanganyaaa!

Hivi simultaneous equation ulifanya wewe?

Kiranga unaua muzee!! Ushindwe na ulegee!! Nimecheka sana mpaka wife anabaki kujiuliza kulikoni! The question is hilariously satirical and sarcastic! Sasa mtu haelewi basics za kujenga arguments lakini bado anahitaji kubishana kwa issues ambazo thinkers from time immemorial wamekuwa wakileta arguments and counter arguments...no wonder kina Sheikh Ponda na kina Lusekekelo wanazidi ku-flourish amid poverty and ignorance of believers!
 
Aiseeeeeeeeeee!. Ee Mungu naenda kulala, wewe tu ndiye unayejuwa kesho itakuwaje, basi nilinde usiku huu kama ulivyofanya kwa mchana wa leo. Amina.
 
Umenena vyema kabisa. Watu wanafuata dini kwa sababu ya fear of the unknown. Mtu anaona bora tu ajifiche nyuma ya Imani just in case...watu wengi hawawezi kabisa kuchambua na kufanya logical analysis ya kwa nini wanadamu tupo na tunakufa. Wanapokea tu mafundisho kutoka kwa wajanja wachache waliokariri stori za mababu wa kiyahudi na kiarabu na kulazimisha kuwa hiyo ndiyo proof ya uumbaji na destiny ya mwanadamu.

imekula kwako kwa uvivu wako wakutafakari ukiona akiliyako kilakitu inataka ihakikishiwe kwa macho ni kwamba akiliyako haina uwezo wakuchanganua mambo nawe ni mtu wa kuburuzwa tu.
 
Ndio ujuwe yupo anayeendesha maisha ya viumbe vyote,hakuna anayetaka kufa,hata mnyama pia hataki kufa,lakini Mungu,anaendesha maisha ya viumbe vyake,anafanya atakavyo.Hata wewe hutaki kufa ,lakini huna ujanja utakufa,kwa sababu yupo aliyekuumba,na anayeamua maisha yako.Mungu yup,hata www ukisema hayupo,ni sawa na kusema yule ana akli au yule hana akili,nani kaziona akili?Lakini twajuwa akili zipo,ila matendo ya mtu ndio yatakaotujulisha kama anazo akili au hana.Na hivyo hivyo,matendo ya Mungu tunayaona,ndio mana twasema Mungu yupo,miongoni mwa matendo hayo ni ni kifo cha kiumbe chochote,hakuna binadamu anayetaka kufa,na pia hajui atakufa vipi,tendo la kufa binadamu ndio ushahidi,miongoni mwa ushahidi kama Mungu yupo.Zuia asife yoyote ndani ya familia yako,ndio tutajuwa una uwezo.
hakuna aliyesena ana uwezo hapa.tunahoji vipi mungu mwema awaumbie wengine yasiyo mema, hiyo ndio pointi kufa kwaweza kuwa nature tu.mimi kukubali kufa hakunifanyi nikubali au nikatae uwepo wa mungu kwa kua sikuanzisha kufa.au sitakuwa wa kwanza kufa.
vipi mungu mwema mwenye nguvu mkarimu mweza wa yote aruhusu mateso kwa viumbe wake?.kwanini asitumie utukufu wake kutufanya tusikengeuke?.ni sawa na mzazi kuwazaa watoto halafu anatumia njia mbadala kuwafanya wamuheshimu.kwanini asingewajaza pumzi ya wema.
imani huja kwa kusikia na kwa kiasi kikubwa kabisa kwa kuona.tumesikia toka utotoni mafundisho ya mungu.na kwa kutumia akili na maarifa tuliyonayo tukichanganya na kuona ambao ndio msingi mkubwa kabisa wa kuamini,tunaona dunia inaangamia ingali tulisimuliwa kuna nguvu kubwa sana ya kupambana na shida za binaadamu.
 
imekula kwako kwa uvivu wako wakutafakari ukiona akiliyako kilakitu inataka ihakikishiwe kwa macho ni kwamba akiliyako haina uwezo wakuchanganua mambo nawe ni mtu wa kuburuzwa tu.
yeye anatumia akili yake kuhakiki alichosikia na kufananisha anachokiona.wewe umekipokea moja kwa moja na unakitumikia sasa hapo nani kilaza anayehoji au aliye kama dekio linazoa kila kitu ukiwamo uchafu.
 
Unajua hivyo wanavyoita "vitabu vitakatifu" ni wizi wa kazi za jamii za kale za Kimisri, kigiriki, kiasyria, etc. Na ndio maana hata Muhamad naye alichofanya ni kudesa tu toka Agano la Kale la Wayahudi akaja na madai kwamba kashushiwa aya! Swali rahisi nililowauliza waumini wa dini hizi, inakuwaje kwamba mie msukuma nilaaniwe na kuhukumiwa kwa dhambi ya asili aliyoitenda Adam na Eve? Babu yangu Masalakulangwa alikuwa na uhusiano gani na watu hao? Hakuna jibu la kueleweka.

Huko Ulaya watu wengi wamegundua kamba na utapeli mwingi katika hicho kitabu...ndio sababu hawashoboki tena na habari za masimulizi ya wayahudi...wamebaki watu wa Mashariki ya Kati waliodesa kutoka wa jirani zao wayahudi...kila siku wanauana kwa ajili ya Mungu...na cha ajabu inakuwaje Mungu wa waarabu atofautiane sana na Mungu wa wayahudi ilhali wote wanasema Mungu ni mmoja na Yesu/Isa ni mwana (Mungu Mtu)/mtume wake? Hapo utawaona jinsi watakavyobishana wao kwa wao na kuanza matusi ambayo hjawahi kuyasikia!
au kusema yesu alikuja kukomboa dhambi zetu.sasa kama dhambi zetu zishabebwa na mkombozi kwanini sisi tuhangaike kuomba na kutubu.hapa unagundua ni wanazi wanaotaka kulazimisha yesu awe mungu kwa kigezo cha mtoto wa nyoka ni nyoka.kwa kukazia na kitu kiitwacho fumbo la utatu mtakatifu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom