Mazee ukishaamini tu kwamba mungu ndiye muumba wa kila kitu, basi mungu anakuwa responsible kwa dhambi zote zilizoko duniani, pamoja na vyote vilivyoumbwa.
Hata ukitaka kumpakazia shetani nitakuuliza huyo shetani kaumbwa na nani?
Huo uwezo wa dhambi kuwezekana umetoka wapi?
Halafu bora hata wangetuambia kwamba mungu hakuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu mzuri zaidi ya huu, ikambidi tu aumbe huu atupe maisha.
Lakini tunaambiwa mungu ana ulikuwa na uwezo wote na upendo wote!
Hogwash.
Huyo Heiyer haoni hii? Au kaenda kwa Baba sijui Mwana Askofu kutafuta majibu? Halafu usikute pamoja na ubishi wote alio nao, shuleni alikimbia mara tu baada ya kujua kusoma na kuandika, basi! Mtu kama huyu hata huyo mungu wake, kama ana akili timamu kabisa, lazima amshangae kabisa!