Mwacheni Mungu aitwe Mungu

Mwacheni Mungu aitwe Mungu

Wote wanaoamini hakuna Mungu,hawataki kufa,ikiwa hakuna Mungu mbona hamjiui,ili mkahakishe roho zenu zikitoka kama yupo au hayupo.Jiue ukahakishe kama yupo au hayupo,na kama hayupo fanya urudi uwajulishe watu kama hayuko.Wasema hakuna Mungu lakini kufa waogopa,wajuwa kama utakutana naye.

This is what I called "the collapse of structured thinking".

A potpourri of multiple non-sequiturs, contradictions, backassward assumptions, birdbrained "reasoning", criminally unethical encouragements, and just garden variety, run of the mill jellyfishlike invertebrate lack of spine.

Mimi siamini kama mungu yupo, sina mzigo wa proof. Wanaosema mungu yupo ndio wenye mzigo wa proof.

Kwa hiyo kama kuna mtu anatakiwa kujiua ili a prove kwamba mungu yupo, ni wewe unayesema kwamba yupo, si mimi ninayesema kwamba hakuna ushahidi kwamba yupo.

You got it backasswards!
 
Wote wanaoamini hakuna Mungu,hawataki kufa,ikiwa hakuna Mungu mbona hamjiui,ili mkahakishe roho zenu zikitoka kama yupo au hayupo.Jiue ukahakishe kama yupo au hayupo,na kama hayupo fanya urudi uwajulishe watu kama hayuko.Wasema hakuna Mungu lakini kufa waogopa,wajuwa kama utakutana naye.
Irrelevant!! Kwa nini sisi tunaoamini kuwa tutaenda mbinguni tusijiue?ilhali tunaamini mbinguni ndiyo sehemu bora kabisa ambayo sisi wapinzani wa kina Kiranga tutapumzishwa huko?kwa nini ajiue yule asiyeamini juu ya maisha baada ya kifo?mimi nakusanya ushahidi tu!! Siku nikiupata pasipo shaka kuwa nitaenda mbinguni nitajiua siku hiyo hiyo,sababu pia ninachoka na mateso ya dunia hii.
 
Last edited by a moderator:
Kama kuwako Mungu,ambaye ndiye aliyeumba viumbe vyote na kila kilichomo duniani, si za kweli basi pia kila kilichotengenezwa duniani,hakikutengenezwa,kimejitengeza mwenyewe.Nina uhakika ukisema Gari aina yoyote au Radio aina yoyote au Nyimba aoina yoyote hakuna aliyevitengeza hivyo utaonekana mjinga na Huna akili.Ni sawa na kuona unyao wa simba,halafu useme unyao huo umejitengeneza wenyewe,utaonekana huna akili au akili zako hazina akili.Kila unachokiona kwa macho yako kwa kuhisi ujue yupo aliyekifanya kiwepo.Na ndio huyo huyo aliweka production date na expire date.Ndio mwanadamu anazaliwa,ndio production date yake,na anakufa ndio expire date yake.Kwa hiyo huyo Mungu aliyemuumma mwanadamu ndio huyo amewka production date na expire date.Wewe unayo production date yako,sasa unasubiri expire date yako.Sasa kama hakuna Mungu,ondoa Expire date yako,usife,au ondoa expire date ya umpedaye yoyote,kama mkeo au mwanao au mzazi ,au mpenzi wako.Wasife,waishi milele,hapo ndio hoja zako zitaonekana zina akili.ukishimdwa hapo kuondoa expire date,ujuwe Mungu yupo.Ipo mifano mingi kwa mwemye akili kujuwa kuwa yupo muumbaji,ambaye ndiye Mungu.
Kikwajuni one,

Mwenyezi Mungu ni mwingi wa rehema ameumba binadamu na wanyama halafu wanyama hakwafanya mahayawani bindamu akatupa akili ndiyo hizo tunazozitumia sasa hivi kupingana na mwongozo ndani ya maumbile na kuona kama Mungu hayupo ni stori tu.

Wapo wapi kina firauni waliokuwa wanajifanya ndiyo Mungu.

Hivi mwili wa binadamu mfano kwenye tumbo, Ini, Figo, Bandama, Moyo, Mapafu, vimejitengeza venyewe, au vimezuka, lakini anakubali injini, computer, imetengenezwa na binadamu.

Tatizo binadamu wanataka kufikiri mpaka nje ya uwezo wao.
 
Last edited by a moderator:
Ndio lakini kwa tabu na mateso makali.

Theory ya uumbaji hai make sense. Mimi binadamu wa kawaida mwenye madhambi kibao namuonea huruma huyu mwenzangu, iweje Mungu ambae yeye tunaambiwa ni Mungu wa upendo Mungu wa huruma hana huruma? Hizi imani za Mungu uwepo wa mtu kwenye mawingu anaeumba vilema halafu anasifiwa ni total nonsense na binadamu anazikubali hook line and sinker. Duuuh....

mungu sio mtu afanani na chochote ukifikiriachi.u have a worse concept about God.do u think u and ur body mechanism came from no where.go on hell will be ur home
 
Genesis :31
ulichokiandika kina mantiki fulani ila mimi ninaweza kusema labda mungu anawaumba hawa vilema ili utukufu/matendo yake makuu yaweze kuonekana au unasemaje?

Ni mambo kama haya ndiyo yanayofanya watu tutambue uwepo wa mungu. Pasingekuwa na watu kama hawa kila kitu kingekuwa sawa hakuna mtu ambaye angemkumbuka mungu.

Cc; kiranga.
 
By Anheuser Hivi unaweza kutengeneza kitu kibovu ili kitu kizuri ulichotengeneza kiweze kuonekana? Toyota Motors watengeneza magari machache mabovu ili magari yao makali yapate utukufu! Si ndio wataharibu market ya magari mazuri? It does not make any sense whatsoever!

Okay, kwa hiyo tukiona vilema ndio tunamkumbuka Mungu, kwamba anatutisha kuwa atatugeuza vilema au ni vipi? Tukimwaga ugali atamwaga mboga, nothing short of laughable.

Na kama hivyo ndivyo, kwa nini amemtoa huyo jamaa kama mbuzi wa kafara ili sisi tupate fundisho, jamaa amekosa nini? Huyo Mungu anaetoa watu kafara mbona ana operate kama mchawi mchawi, kama wanaokamata innocent albino at random kuwatoa viungo ili kufikia malengo fulani. Hana huruma!

Na kama hivyo ndivyo, kamtoa jamaa kafara ili tumkumbuke Mungu, mbona the whole plan is not working? Nani anamkumbuka Mungu maisha haya kwa kuona vilema? Dunia imejaa madhambi na maasi, obviously his plan ain't working.

Halafu kwa nini huyu mungu anapenda kutukuzwa sana? Utafikiri Idi Amin Dada bwana!

Kupenda kutukuzwa ni sign of insecurity, huyu mungu mwenye uwezo wote kwa nini anahitaji sana approval na kutukuzwa na binadamu?

Wengine mpaka wamfanyie sala tano kwa siku, za nini zote?

Hata wanadamu hatulazimishani kuamkiana mara tano kwa siku.

Huyu mungu mwenye uwezo wote ana inferiority complex gani?
 
Halafu kwa nini huyu mungu anapenda kutukuzwa sana? Utafikiri Idi Amin Dada bwana!

Yeye anapenda kutukuzwa ama waumini ndo wanapenda kumtukuza?

Coz for all I know he, she, or it has never spoken publicly about kupenda kutukuzwa.
 
mungu sio mtu afanani na chochote ukifikiriachi.u have a worse concept about God.do u think u and ur body mechanism came from no where.go on hell will be ur home

Kama mungu hafanani na chochote anachofikiria Anheuser , wewe umewezaje kumfikiria? Umewezaje kujua hilo?

Wewe una sense ya tano inayopita the electromagnetic spectrum huko umeitumia kumuelewa mungu ambayo sisi wengine hatuna?

Kama huna, una senses tano kama zetu wengine, inawezekanaje useme mungu hafanani na chochote afikiriacho Anheuser wakati hata hujui Anheuser anafikiria nini?

Mungu kwa majibu yenu mpaka sasa anaonekana ni concept tu isiyo na ukweli wowote. Mnashindwa kuthibitisha, hususan kwa sababu hata kuthibitisha kwamba mungu yupo kutakuwa ni kuthibitisha kwamba mungu hayupo.

You cannot prove god (Judeo-Christian omnipotent, omniscient, omnipresent, omnibenevolent ) exists, the moment you think you have proved god exists, you have proved that that which you think is god is not god at all.

For whatever can be contained in a proof system cannot be god. God is not containable.

Unaona contradiction hapo?
 
You do not understand the truly universal set.

Ukishaanza kutoa exception kwamba mungu hayupo, huwezi kuwa absolutist kwamba vingine vyote lazima viumbwe.

Framework yako ishaanza na loophole ya exception.Universe yako imeanza na mbegu ya exception, huwezi kutegemea kwingine kusiwe na a similar exception.

Basically umekubali kwamba si lazima vyote viumbwe, kwa sababu umemtoa mungu katika kuumbwa.

Na ukishakubali kwamba si lazima kwamba vyote viumbwe, ushakubali kwamba si lazima hata mwanadamu na vingine vyote viumbwe pia.

God is an ugly conundrum, created by human minds. This explains why the god idea is so ugly, full of holes, inconsistent and fallacious.

Kiranga i salute you... siendelei kukusoma mwisho nami ntakuwa atheist. By the way umesoma nakupitia kwa umakini arguments za st thomas aquinas aliyekuwa askofu wa.Roma juu ya uwepo wa mungu. ??
 
Last edited by a moderator:
Yeye anapenda kutukuzwa ama waumini ndo wanapenda kumtukuza?

Coz for all I know he, she, or it has never spoken publicly about kupenda kutukuzwa.

Kasema anapenda sio tu utukufu, bali pia ana wivu kama jibaba lenye sura mbaya na mke kigoli.

Ukimsoma huyu mungu unabaki kucheka kwa nini watu wengi wanamuamini.
 
Kikwajuni one,

Mwenyezi Mungu ni mwingi wa rehema ameumba binadamu na wanyama halafu wanyama hakwafanya mahayawani bindamu akatupa akili ndiyo hizo tunazozitumia sasa hivi kupingana na mwongozo ndani ya maumbile na kuona kama Mungu hayupo ni stori tu.

Wapo wapi kina firauni waliokuwa wanajifanya ndiyo Mungu.

Hivi mwili wa binadamu mfano kwenye tumbo, Ini, Figo, Bandama, Moyo, Mapafu, vimejitengeza venyewe, au vimezuka, lakini anakubali injini, computer, imetengenezwa na binadamu.

Tatizo binadamu wanataka kufikiri mpaka nje ya uwezo wao.

huyu kiranga hata mimi kaniacha hoi.. lakini anazopoint za msingi.
 
Last edited by a moderator:
Kikwajuni one,

Mwenyezi Mungu ni mwingi wa rehema ameumba binadamu na wanyama halafu wanyama hakwafanya mahayawani bindamu akatupa akili ndiyo hizo tunazozitumia sasa hivi kupingana na mwongozo ndani ya maumbile na kuona kama Mungu hayupo ni stori tu.

Kabla ya kusema mwenyezi mungu kaumba binadamu na wanyama, kwanza prove kwamba yupo. Hujaprove kwamba yupo usharukia kwamba kaumba?

Wapo wapi kina firauni waliokuwa wanajifanya ndiyo Mungu.

Kina Firauni wamekongolewa na entropy per the second law of thermodynamics, kama ambavyo kila kitu kitakongoroka.

Sasa unataka kusema entropy na the second law of thermodynamics ndiyo mungu?

Hivi mwili wa binadamu mfano kwenye tumbo, Ini, Figo, Bandama, Moyo, Mapafu, vimejitengeza venyewe, au vimezuka,

Hata nikisema sijui jibu la swali hili, hilo halina maana jibu lake ni mungu.

Ukiniuliza square root ya mbili ni nini? Nikasema sijui, hilo halina maana jibu lake ni nane. Why should it be nane, show me how.

Kwa nini binadamu awe kaumbwa na mungu? Nioneshe.

Kama unasema complexity ni lazima iwe na muumba, ultimately kwa principle hiyo hiyo itabidi mungu naye awe na muumba, na muumba wake awe na muumba, ad infinitum.

lakini anakubali injini, computer, imetengenezwa na binadamu.

Cha kushangaza hapa ni wewe unayekubali kwamba complexity ndogo kama injini inatengenezwa na binadamu, lakini complexity kubwa kama mungu haitengenezwi.

Ni kama kukubali kwamba mkokoteni ni lazima utengenezwe na binadamu, hauwezi kutokea wenyewe, lakini Jumbo Jet linaweza kujitengeneza lenyewe tu.

Kama binadamu (low complexity) ni lazima awe ameumbwa na mungu, na complexity ni alama ya intelligent design, then mungu (high complexity) naye ni lazima awe ameumbwa, na muumba wake lazima awe ameumbwa.

This god falls on his face.

Tatizo binadamu wanataka kufikiri mpaka nje ya uwezo wao.

Wakiweza kufikiri maana yake hapo si nje ya uwezo wao, by definition binadamu hawezi kufikiri nje ya uwezo wake.

Usiogope kufikiri kwa kuogopa kufikiri nje ya uwezo wako.Utakuwa kama mtu anayeogopa kutembea kwa kuogopa kufika mwisho wa dunia na kudondoka.
 
Kiranga i salute you... siendelei kukusoma mwisho nami ntakuwa atheist. By the way umesoma nakupitia kwa umakini arguments za st thomas aquinas aliyekuwa askofu wa.Roma juu ya uwepo wa mungu. ??

Nimejitahidi kusoma anthologies zilizokusanya malumbano ya manguli hawa, nilianza na "Philosophy of Religion: An Anthology" kabla hata sijaenda high school, humo wameandika arguments kibao za kina Plato, Aristotle, Aquinas, Augustine, Anselm, Kant,Nietzsche,Berkeley,Russell tangu my coming of age, nika augment na kina Dawkins, Hitchens, Kung na wengine wengi mpaka outside of western thought kwa kina John Mbiti na kwenye ma Dhammapada, Tripitaka, Bhagavad Gita, Vedanta, Upanishads etc.

Nimeangalia mpaka the gnostic bible, nimesoma si Quran na biblia tu, bali mpaka vitabu vilivyokatwa vikatolewa nje ya biblia na Constantine hapo Nicea.

Kwa hiyo si kwamba nasema haya kwa ubishi tu bila kufanya the basic readings first.

Ndiyo maana mara nyingine nauliza maswali ambayo hayapati majibu, haya maswali ni kutoka kwenye classical arguments ambazo mpaka leo hazijapatiwa majibu.

Hata kama nakataa uwepo wa mungu, huwezi kusema nakataa kwa sababu sijamtafuta. Nimemtafuta mpaka kwenye quantum theory huko, hayupo.
 
Ndio lakini kwa tabu na mateso makali.

Theory ya uumbaji hai make sense. Mimi binadamu wa kawaida mwenye madhambi kibao namuonea huruma huyu mwenzangu, iweje Mungu ambae yeye tunaambiwa ni Mungu wa upendo Mungu wa huruma hana huruma? Hizi imani za Mungu uwepo wa mtu kwenye mawingu anaeumba vilema halafu anasifiwa ni total nonsense na binadamu anazikubali hook line and sinker. Duuuh....

Pole sana kwa mawazo mgando! Siku moja ukipatwa na majanga, jaribu ku-apply hizo theory zako!
 
Kama kipara (kukosa nywele) si rangi ya nywele wala nywele, basi pia kukosa imani si imani.

.
Kipara kutokuwa nywele haimaanishi kwamba nywele huota kutoka kipara. Hivyo basi nywele ikiwa ni nyeupe au nyeusi ni lazima zimetoka/ota katika kipara. Haiingii akilini mtu kudai kwamba nywele zimeota kutoka katika utupu(No where). Maana yake ni kwamba wanaosema hakuna Mungu ni imani walioipata kwa kusikia sawa na wale wanaosema kuna Mungu. 'imani' ndio bayana yao na sii vinginevyo au Karanga unaweza ku-pfoof bila shaka imani yako kwamba hakuna Mungu?
.
 
Nimejitahidi kusoma anthologies zilizokusanya malumbano ya manguli hawa, nilianza na "Philosophy of Religion: An Anthology" kabla hata sijaenda high school, humo wameandika arguments kibao za kina Plato, Aristotle, Aquinas, Augustine, Anselm, Kant,Nietzsche,Berkeley,Russell tangu my coming of age, nika augment na kina Dawkins, Hitchens, Kung na wengine wengi mpaka outside of western thought kwa kina John Mbiti na kwenye ma Dhammapada, Tripitaka, Bhagavad Gita, Vedanta, Upanishads etc.

Nimeangalia mpaka the gnostic bible, nimesoma si Quran na biblia tu, bali mpaka vitabu vilivyokatwa vikatolewa nje ya biblia na Constantine hapo Nicea.

Kwa hiyo si kwamba nasema haya kwa ubishi tu bila kufanya the basic readings first.

Ndiyo maana mara nyingine nauliza maswali ambayo hayapati majibu, haya maswali ni kutoka kwenye classical arguments ambazo mpaka leo hazijapatiwa majibu.

Hata kama nakataa uwepo wa mungu, huwezi kusema nakataa kwa sababu sijamtafuta. Nimemtafuta mpaka kwenye quantum theory huko, hayupo.

Sasa mbona mimi nikienda kanisani nakumuomba huyo mungu.. nafarijika sana na pia sometime huwa anajibu maombi kwA shida zangu kutatulika
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom