Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?

Junius,

Singapore???? Kwani sii Comoro au Madagaska??

LOL!
zanzibar ina almost every economic opportunities walizonazo wa-singapore tatizo kubwa fursa ya kuzitumia kwa mapana imewekewa "herizi" Dodoma, itawachukua kama miaka kumi kuwafikia wa - singapore,kama haya "mambo" ya kukwazana mnayoita muungano yatarekebishwa kwa maslahi.
 
Wanaowaza kuvunjwa kwa Muungano wana ubinafsi.Kuvunja Muungano si suluhisho au tiba ya matatizo aidha yaliyoko Zanzibar au Tanzania Bara.

Dawa na tiba kwangu ni kujadiliana kwa uwazi juu ya matatizo yaliyopo ya muungano na kuyarekebisha au kusahihisha.

Kumbukeni kabla ya wageni - wakoloni kugawa mataifa yetu hatukuwa na Tanganyika wala Zanziba.Wakoloni ndiyo waliotugawa kwa kuweka mipaka ili watutawale kwa urahisi.walichofanya wazee wetu - Mwl.J.K.nyerere na Karume ni kurejesha umoja na undugu wetu uliovunjwa kwa makusudi na Wakoloni.

Kama wanaotaka kuvunjwa kwa muungano wanaona hivyo, maana rahisi ya mawazo yao ni kwamba wanapuuza mawazo ya wazee wetu na kuthamini ya Wazungu! Jamani mambo haya ni ya aibu.

Msimamo wangu: Muungano uwepo, uendelee lakini tusahihishe makosa kama yapo.
 
huu si muungano wa Pinda na Shamsi, ni wananchi wapewe fursa ya kusema kinaga ubaga, wasituletee ule usanii wa tume aya jaji Kisanga "white paper" hapa direct kwenye hoja ie referendum, au njia yoyote bora itakayowakilisha mawazo ya wananchi kila upande kivyake
 
0000126865_0008.gif
0000126865_0009.gif
0000126865_0010.gif
0000126865_0011.gif
 
Junius,
Mkuu wangu huu ni mwaka wa 7 toka nimetoa suggestion ya referendum kwa viongozi wa CUF bara na visiwani..Nilimwandikia in personal, Sharrif Hamad (2003) kuhusiana na hili na hakunijibu pengine yawezekana hakupata ujumbe wangu..
Kwa nini viongozi wote wanacheza mchezo wa siasa mahala ambapo wazi waamuzi wa Muungano ni wananchi wenyewe?.. Kama kweli wananchi wa Zanzibar wanataka Muungano ufe, Referendum ndio mwamuzi na ikumbukwe tu kwamba Bara na Visiwani hapatakalika!..
Leo hii kuna Wapemba na Wakomoro kibao bara, Wabara wapo Visiwani wote wana enjoy uraia wao kwa sababu ya Muungano wa watu na sio nchi wala vyama..Muungano Ukivunjika tu kuweni tayari kwa yote yatokanayo na kuvunjika kwa Muungano huu, kwani Mapinduzi ya mwaka 1964 yalifanywa na wahuni wakuli wabeba mizigo bandarini walioweka rekord ya dunia ktk Mapinduzi ya haraka!.
 
Kuwepo kwa Wapemba na wacomoro hakutazuia walio wengi kudai ikiwa wanaona Muungano haupo katika njia sahihi ,ikiwa Muungano unawakilisha nchi moja na nchi nyingine haijulikani ilipo ,inaonekana mnababaisha au ni wagumu wa kufahamu au hamtaki kufahamu,WaZanzibari wanahoji ipo wapi Tanganyika ,hilo tu,na huko iliko ijitokeze ili kuijenga Tanzania sasa hapo pana ugumu gani ?
WE needs the lost Tanganyika and the existing Zanzibar to be on the same line on constructing Tanzania ,Zanzibar alone can do nothing at all to deal with Union matters ,let Tanganyika ijitokeze ili kupanga mikakati. Union set hatuikubali ,hivi kwanini Mawaziri wa Muungano hawaishughulikii Zanzibar na wanapoamua kuishughulikia inaonekana ni kuibana kiuchumi ?
 
JK yuko kwenye wakati mgumu kweli sasa hivi, mara mafisadi, mara ZNZ

hivi karume leo anajifanya hali ya hewa mbaya ....wakati marais wote wa zanzibar wamekuwa wakilala dar na kuenda zanzibar asubuhi...leo ameshindwa kuja au anaendeleza dharau kwa kikwete.....kikwete amejiweka katika hali ya kudharaulika kutokana na vitendo na maneno yake yasiyo na utekelezaji......sasa hapo karume kampiga kibao cha usoni bosi wake...waliokuwepo vipi....waziri kiongozi na shamuhuna[msema ovyo] walikuwapo??????
hii ni sababu nyingine ya kikwete kutoendelea ..ameonesha dalili ya kushindwa kuulinda muungano ..aliyoapa...utamfia mkononi huu!!
 
Junius,
Mkuu wangu huu ni mwaka wa 7 toka nimetoa suggestion ya referendum kwa viongozi wa CUF bara na visiwani..Nilimwandikia in personal, Sharrif Hamad (2003) kuhusiana na hili na hakunijibu pengine yawezekana hakupata ujumbe wangu..
Kwa nini viongozi wote wanacheza mchezo wa siasa mahala ambapo wazi waamuzi wa Muungano ni wananchi wenyewe?.. Kama kweli wananchi wa Zanzibar wanataka Muungano ufe, Referendum ndio mwamuzi na ikumbukwe tu kwamba Bara na Visiwani hapatakalika!..
Leo hii kuna Wapemba na Wakomoro kibao bara, Wabara wapo Visiwani wote wana enjoy uraia wao kwa sababu ya Muungano wa watu na sio nchi wala vyama..Muungano Ukivunjika tu kuweni tayari kwa yote yatokanayo na kuvunjika kwa Muungano huu, kwani Mapinduzi ya mwaka 1964 yalifanywa na wahuni wakuli wabeba mizigo bandarini walioweka rekord ya dunia ktk Mapinduzi ya haraka!.
kwanza tukubaliane si kweli kuwa wazanzibar wanataka muungano ufe, suala liliopo hapa ni muundo gani bora wa muungano,ambao utasimamia majukumu ya kila upande(yasiyokuwa ya muungano) kwa wazanzibar na hata watanganyika wanaona huu tulionao, si muundo bora wa muungano(serikali mbili)kwa kuwa hauweki wazi mambo hayo.Hivi kweli kama wananchi wataamua muundo wa muungano wanaoutaka wao ndo nchi hazitakalika? hata kama wataamua iwe basi mm si dhani hivyo, kwa kuwa huu utakuwa si muungano wa kwanza duniani kufa, Yugoslavia ipo vipande vipande sasa na kila nchi na lake, hakuna ugomvi, nimeskia hivi karibuni kuwa hata hiyo Montenegro iliyobaki imeshajitenga hakuna tatizo lolote. Hata muungano wa USSR ulikuwa na nchi nyingi na matatizo kama yetu hapa na walipoona kuwa hawawezani kila mmoja kenda na hamsini zake na hakuna ugomvi. Muungano wa Malay,walipelekana kama Tanganyika na zanzibar, kama hivi , walipoona hawawezani, kero hazishi kila mmoja akatafuta njia yake. Na nchi zote hizo watu walioana, wakazaana na kutengena kwao hakukuwasumbua kitu kila mtu akatafta lake linalo muhusu basi.
Hoja ya msingi katika Muungano wa Tanganyika na zanzibar ni kuwa kwa kuwa kiini cha matatizo ya muungano kina juulikana basi marekebisho yafanywe kwa nia njema tu, ili pande zote ziridhie namna bora ya muungano, kwa kuwashirikisha kikamilifu wananchi. Hila na vitisho havitasaidia kwani zama hizi si zama za kutishana, wananchi wanajua haki zao, wanajua wanachokitaka katika maisha yao, ni vigumu sasa kuwaimbisha nyimbo za "harusi" wakiwa katika "msiba" hawatakuelewa. Ni bora kwa namna yoyote ile hili suala waachiwe waamue wananchi ndo wenye nchi ati.
 
..haya ni mafuta tuu wanayoamini wanayo,waache waende wakajenge Islamic Republic yao!
 
Kuwepo kwa Wapemba na wacomoro hakutazuia walio wengi kudai ikiwa wanaona Muungano haupo katika njia sahihi ,ikiwa Muungano unawakilisha nchi moja na nchi nyingine haijulikani ilipo ,inaonekana mnababaisha au ni wagumu wa kufahamu au hamtaki kufahamu,WaZanzibari wanahoji ipo wapi Tanganyika ,hilo tu,na huko iliko ijitokeze ili kuijenga Tanzania sasa hapo pana ugumu gani ?
WE needs the lost Tanganyika and the existing Zanzibar to be on the same line on constructing Tanzania ,Zanzibar alone can do nothing at all to deal with Union matters ,let Tanganyika ijitokeze ili kupanga mikakati. Union set hatuikubali ,hivi kwanini Mawaziri wa Muungano hawaishughulikii Zanzibar na wanapoamua kuishughulikia inaonekana ni kuibana kiuchumi ?
hapa nikubaliane nawewe kuwa , pana kesi ya washirika wawili "partners" na tatizo limejitokeza. Ili tutatuwe tatizo lazima patners wote wawepo. "status quo"
kama walivyoyaanza wao wawili na wayamalize wakiwa wawili kama awali.
 
..haya ni mafuta tuu wanayoamini wanayo,waache waende wakajenge islamic republic yao!
huyooo tena, matatizo ya muungano yameanza tokea "day one" ya kuundwa kwa muungano wenyewe. Hili la mafuta limekuja kuengeza muwako wa kandili.mambo yaliharibika toke asubui bwana
 
Kuanzia Raisi hadi Mawaziri wa Muungano wanaifanya Zanzibar kama mwana wa kambu tena yule asiependwa maana kuna wengine huwapenda wanawao wa kambu.

Kelele za kudai Zanzibar kama Nchi zilimfanya Raisi Kikwete aende kwa vishindo Zanzibar na kutoa hotuba kali sana na kuwatisha na kuwadhalilisha WaZanzibari ,wakati kelele za kujitenga ziliwahi kusikika Kigoma na hatukumuona Kikwete kuelekea huko na kutoa vitisho

Halikadhalika Mawaziri wa Muungano wamesikika na wao wakiponda mambo ya Zanzibar tena kwa dharau ,hivyo utaiona picha ambayo inamueleza vitendo anavyofanyiwa mtoto kama wa kambu asiyependwa na hakuna ukali wowote ule kwa mtoto Tanganyika maana ni wao wenyewe wanamdekeza huku wanamnyoa :D Na mtoto Tanganyika anamkodolea macho Zanzibar
 
Mchukia Fisadi, Bubu Ataka Kusema, n.k.,

Mimi sioni ni vipi kiongozi wa Tanzania Bara, fisadi and such, anaweza kunufaika binafsi na Muungano. Kwa mfano kivipi, hebu nipeni nadharia moja. Nionavyo mimi, kama wewe ni kiongozi wa Tanzania bara, ungetaka huu muungano ufe, sababu moja ikiwa ni kwamba Wazanzibari wanamaliza Oxygen ya uongozi huku kwetu.

Wazanzibari tumewapa ki affirmative action fulani hivi, wanatengewa nafasi za uongozi lukuki wakati wanatoka kwenye kiwilaya kimoja tu, I mean, Unguja, Pemba zote (1660 sq. km) zinamezwa na Masasi (8,940 sq. km). zaidi ya mara tano. Lakini tunawapa V.P. wa muungano, mawaziri kibao, yani ni bwena, na wabunge lukuki wakati wanawakilisha watu kiduchu. Can't believe it, I mean, there are more Mtwarans than Zanzibaris. Sasa ni kwa nini waachwe wamalize Oxygen ya uongozi huku kwetu bara?

175px-Tanzania_Mtwara.png

Hebu tueleze unajadili kitu gani? Kama hujui maana ya Muungano si uzibe mdomo na ungojee utakaloweza kulifahamu? Unafikiri huo ukubwa wa Tanganyika una maana gani kiinchi, mbona kuna visiwa vidogo vidogo tu duniani vilivyo huru na kwa vile Zanzibar ni nchi sawa na Tanganyika Kistatus suala la ukubwa unabidi mlione nyie mnaowabana walio wadogo. Eti Masasi? Ina Status gani ulimwenguni?
 
Dawa mmetuandalia ili mtunyweshe sisi, lakini bahati mbaya mmeamua kuonja wenyewe kabla hamjatunywesha sasa mnapata maumivu ya bure. Tunywesheni basi hiyo ilobaki nasi tupate maumivu ili yatupe nguvu ya kudai Tanganyika.

Tunazungumza hili la kuingilia mambo yasiyowahusu. Kwani Mzee si tayari umefura Eti wanakuamulieni mambo yenu ? Naam na wao hawapendi nanyi muwaingilie mambo yao na wanaona uchungu kama unavyojisikia wewe kukufikiria kwamba kuna kitu unakihitajia. Kwa ufupi kama unahisi wao hawana haki ya kukufikirieni jambo basi nanyi hamna haki hivyohivyo. Naamini umefahamu na tutajadili jengine sio hili.
 
ukweli uliopo, jamaa wa CUF, wamewawin CCM kwa hili, lakini agenda ya CUF siku zote ni ubaguzi tu japokuwa wanauficha, lengo na madhumuni makubwa ya wana CUF ni kuchukua Pemba na kisha kujirudisha kwa sultan wao wa Oman, kwani sidhani kabisa kwamba hawa jamaa wanajiona ni waswahili, na ni ukweli usiofichika kama hawa jamaa wakijitenga hata mwaka haufiki Pemba na Unguja nazo zitajitenga

Naona umeishiwa Hoja kwani CUF pia walikwambieni mkatae SHIRIKISHO LA AFRIKA MASHARIKI? Kwani kwenu Muungano si sawa na Ibada kila ukiifanya sana ndio utapata pepo zaidi? Basi ipelekeni nchi shirikisho la Afrika Mashariki huko hilo Limuuungano litakuwa kubwa zaidi.
 
Mbona mnazungumzia kuunda serikali ya tanganyika kama suluhisho la muungano....kama tatizo kila upande uwe na serikali yake basi kwanini tusiondoe serikali zote ijulikane kuwa wote tumekosa na ibaki hii ya Jamhuri ya Muungano maana naona tu wazanzibar wanatuamulia mambo yetu kama vile sie hatuna hisa kama hii UNION....nilichangia kwenye thread zilizopita na naendelea na msimamo wangu kuwa wanazenji acheni kutumika kisiasa kwani hakuna mantiki ya hoja mnazozitoa.

Kama ni usawa basi uanze kwa kuvunja serikali yenu afu ndo tuanze kuongelea haja ya serikali mbili. Mambo ya kumangamanga kisiasa hayatasaidia.

Kwa kipindi cha miaka 45 hiyo serikali ya Muungano imekuwa ikijishughulisha na mambo ya Tanganyika TU na tayari mmeshajijenga kuwa ni yenu. Wazanzibari wanataka muwe na Serikali yenu au kwa maana nyengine Serikali ya Muungano iache kushughulikia Tanganyika ijiondowe huko na mjifunze kuendesha Serikali sio kubebwa na Serikali ya wote.

Amma kuhusu hoja nadhani hujawahi kuwa na hoja iwapo hoja ni upande mmoja uuamulie mwengine hiyo si desturi ya ubia ulio sawa.
 
Dilunga anashindwa kufahamu kuwa hawa mafisadi wakuu ni mawaziri kuanzia Lowasa na wenziwe mpaka Mkapa nafasi walizonazo ndio zimewafanya wavuruge na kukwiba kama kungekuwa na serikali tatu basi leo hii wangekuwepo gerezani ,sidhani kama kungekuwa na serikali ingeweza kuwalinda watu hawa au mafisadi hawa ,sasa tuambie nguvu za hao watu wengi wa Mtwara wamewafanya nini akina Mkapa na kundi lake ?Mbali ya wale wahindi saba ambao wanawaendesha puta ? Hii Serikali ya Muungano kusema kweli haijulikani inamuwakilisha nani maana WaZanzibari wanaiona serikali hii ni jinamizi linalokula na kunywa damu zao kushinda County Draculla na watanganyika nao wanashindwa kuielewa kwa jinsi inavyosuasua katika kuwachukulia hatua wezi hawa.
Ndio tukasema kupambana na wizi huu mkubwa wa hazina ya Nchi hii Tanganyika fahamu kuwa mali zinazoibiwa ni za Tanganyika na hazimo katika Muungano hivyo kuna ulazima wa kuirudisha Tanganyika ili kupambana na wezi hawa ,wezi wamo ndani ya Serikali ya Muungano wanaiibia Tanganyika ,Zanzibar hana uwezo na kinachoibiwa sio chake hakimuhusu nde wala sikio ,pale panapo mhusu tutafikishana mbali ,kuna asilimia fulani tunaifuatilia,kuna hisa tunazifuatilia,kila pale ambapo tunahusika tukiona mafisadi wanapakaribia basi tutawashika ukosi na tumeona wanayanyemelea mafuta ndugu tumewazuia kwa sababu hapa kuna Zanzibar hivyo ni haki yetu kuigombania ,hatuwezi kuhoji mambo ya madini au misitu huko hayo si yetu ,mbona mnashindwa kufahamu ?

Wandugu wezi hawa tumewashika pabaya tena pabaya sana ,hatupendi ushindani wa jazba kwa kuona WaZanzibar wachoyo hawataki na kitu chao ,huo sio ukweli ni upotoshaji tu ,maana mafisadi wanajua fika kurudi kwa Tanganyika itakuwa mwiba kwao,waTanganyika hawatokubali kufanyiwa upumbavu huu wa watu kujichotea hazina ya Taifa na kufanya Ikulu sehemu ya kuombea vibali na kufanyia biashara.

Kuna serikali ya Muungano,kuna serikali ya Zanzibar halafu kuna serikali ya Tanzania ,mwizi huyo atapitia wapi na kuvuka na vipolo vya nyara za Taifa ? Tanganyika ni lazima irudi au mna hoja ya msingi ? na haina haja ya kuirudisha !
 
Back
Top Bottom