Muungano Hatuutaki!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungano Hatuutaki!!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by GHIBUU, May 27, 2011.

 1. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Assalaam Alaaykum, Waungwana
  Kwanza ninashirikiana na ndugu zetu katika kuombea duwa nafsi zetu na ndugu zetu waliomo kwenye mitihani ya siha, Sheikh Ali Baucha, Bi Salma, japo naye kwa sasa Alhamdulillah. Mwenyezi Mungu Mtukufu atujaalie sisi, wao na jamii ya Waumini siha na furaha na uwezo wa kutenda mema na kuepuka maovu, Aamyn. Jana tulijaaliwa kwenda kumzuri Sheikh Ali, Alhamdulillah anaendelea vyema; salamu zake ni kwa ndugu zetu wote katika ukumbi wetu huu. Tuzidi dua.
  Pili, napenda nilete machache kukhusu yale niliojaaliwa kuyaona na kuyasikia katika vikao vya Mhishimiwa Samuel Sita, mjumbe wa Mhishimiwa Rais wa JMT kwa Wazanzibari.
  Ujumbe wa Wazanzibari kwa Rais Jakaya Kikwete
  “Muungano Hatuukati! Muungano Hatuutaki!! Muungano Hatuutaki!!!” Ni ujumbe aliopewa Mhishimiwa Sameul Sita kuufikisha kwa Mhishimiwa Rais wa JMT kutoka kwa Wazanzibari.
  Ni Imani ya Wazanzibari juu ya Mhishimiwa Sita
  Mhishimiwa Samuel Sita, alifika Zanzibar akiwa ni mgeni rasmi na wa hishima kwa Wazanzibari na kwa Zanzibar. Mhishimiwa Sita na tume yake walifika Zanzibar kumuwakilisha Rais Kikwete katika kutafuta maoni ya Wazanzibari kukhusu pendekezo la uwendeshaji mpango wa urekibishaji katiba ya Tanzania. Mhishimiwa Sita alifanya vikao viwili, Bwawani na Haleisalasi. Wazanzibari wengi, wa vyama vya siasa, jumuia za dini, Waislamu na hata Wakiristo walihudhuria vikao hivi muhimu na kutoa maoni yao kwa uwazi na uhuru kaamili. Humalizi kuwataja wahishimiwa waliohudhuria vikao hivi na kutoa maoni yao. Maoni yote kwa jumla yalikuwa na ujumbe mmoja kwa Rais Kikwete, “Wazanzibari muungano (huu) hatuutaki”. Tukitaja wachache waliohudhuria na kutoa maoni yao haya ni, mzee wetu Mhishimiwa Hassan Nassor Moyo, Profesa Abdulshariff, Mhishimiwa Hamza, Mhishimiwa Salim Bimani, Mhishimiwa Jamila Abeid, Mhishimiwa Edy Riami, Mhishimiwa Farid, na wengi wengineo. Kwa jumla wote hawa na waliohudhuria walidhihirisha kutoridhia kwao kwa huu muungano, hivyo wakamuomba Mhishimiwa Sita afikishe ujumbe huu kwa Mhishimiwa Rais wa JMT. Mhishimiwa Sita aliahidi mbele ya umma uliohudhuria, kwamba ataufikisha ujumbe huu wa Wazanzibar kama anavyo upokea, bila ya kupunguza wala kuzidisha. Ni imani yetu kubwa juu ya uwaminifu wa ndugu yetu, Mhishimiwa Sita kwamba ameufikisha ujumbe kama alivyo ahidi.
  Kura ya Maoni Juu ya Muungano
  Wazanzibari tangu sikumosi ya mavamizi na kumezwa nchi yao, Zanzibar; wamo katika kuwania kurejea Dola yao kama ilivyokuwa pale ilipopata uhuru wake na kujiunga na Umoja wa Mataifa, Disemba 10, 1963. Wazanzibari muda wote huu wakiwa katika juhudi hizi za ukombozi wa Dola yao, Zanzibar; kwa sauti kuu wakikanya, na wanakanya; mpango wowote ule wa “kura ya maoni”. Kama walivyo bainisha ndugu zetu, Virus 99 na Alkindy, kwamba kura ya maoni ndio turufu kuu na ya mwisho wanayoitayarisha watawala Tanganyika kwa kuhalalisha haya mavamizi yao ya 1964 na umezwaji wa Dola ya Zanzibar waliofanya April, 1964. Hadhari wanayoitoa ndugu zetu kuepuka “kura ya maoni” ni muhimu sana. Wajibu wetu Wazanzibari tusimame qauli moja – na hata kwa vitendo (vya amani) – kukataa kata-kata mpango wowote ule wa kura ya maoni kukhusu suala la muungano. Nnanukulu hapa yaliobainishwa kwenye tamko la Chama Cha Jahazi Asilia kukhusu suala la kurejea Dola ya Zanzibar bila ya shuruti yoyote ile na kuepukana na kura ya maoni kukhusu suala hili.
  “Chama Cha Jahazi Asilia kinadai kurejea Dola ya Zanzibar bila ya shuruti lolote. Chama Cha Jahazi Asilia, kinakataa kabisa mpango wowote ule wa kuleta kura ya maoni kuhusiana na suala la kurejea Dola ya Zanzibar; kwa sababu, kurejea Dola ya Zanzibar ni haki ya kimsingi ya Dola ya Zanzibar sawa na Dola yoyote ile ulimwenguni”.
  Maneno haya ya Chama Cha Jahazi Asilia ni maneno ya msingi na muhimu kabisa, juu yetu sisi Wazanzibari kuzidi kuyazingatia kila wakati na kuchukuwa kila hadhari.
  Kura ya Maoni Ipigwe Kutokana na Daftari la Wapiga Kura
  Hii kura ya maoni inayopangwa na watawala ni upotofu juu ya upotofu. Upotofu,
  Kwanza, ilipovamiwa Zanzibar na kumezwa Dola ya Zanzibar, jee Wazanzibari waliulizwa na kupatikana ridhaa yao? Hawakuulizwa. Natusome maandishi ya Mzee wetu, Al Haj Aboud Jumbe, maandishi ya Mhishimiwa Dorado, na wengi wengineo; wote hawa walieleza wazi kabisa kwamba Wazanzibari hawakuulizwa juu ya huu wenyekuitwa muungano, kama wanautaka.
  Pili, kura ya maoni kwa kutumia “daftari la kudumu la wapiga kura”!! Nani asiejuwa upungufu uliojaa katika daftari hili? Nani asiejuwa kuwa Wazanzibari wangapi wamenyimwa haqi zao na daftari hili? Nani asiejuwa wangapi waliokuwa si Wazanzibari wamepewa haqi na kuandikishwa kwenye daftari hii?
  Tatu, kuleta kura ya maoni kumuuliza Mzanzibari kama anataka au hataki kurejea Dola yake ni dharau, bali ni tusi kwa Mzanzibari. Kufanya hivyo ni kuuliza uwezo wake wa kiakili. Nani mwenye akili timamu atakubali suala hili?
  Muungano Hatuutaki!
  Maoni ya Wazanzibari ni yale waliompa Mhishimiwa Samuel Sita, nayo ni “Muungano hatuutaki”! Haya ndio yaliodhihirishwa na Wazanzibari na kufika kwa sauti moja kusisitiza hivyo.
  Wa Billahi Tawfiiq
  Farouk
  Mei 26, 2011
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ondokeni basi. Tumechoka kila siku kusoma yale yale yasiyo na tija kwa mtu wa kawaida.
   
 3. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wazanzibari mnaiba tu mali za Tanganyika, hasa mliovuka maji kuja Bara.
  Hamna ubavu hata siku moja ya kuvunja Muungano, ingekuwa furaha kama mngeweza tuonandokane na kundi la wahujumu uchumi wa Tanganyika, hebu tazama katika idara au wizara inayoshikiliwa na Mzanzibari Tanganyika ni unyama mtupu.
  Mnadeka mpaka mwisho wa Dunia
   
 4. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Kama sisi hatuwezi, vunjeni nyinyi msilalamike na kama sisi.

  Angalau sisi tunaoathirika tunaukataa lakini nyinyi mnafaidika na tena mnalalamika nini?

  Oh Mawaziri, Oh umeme hamna mgao, Oh umeme hawalipi, Oh Wapemba wamejazana.

  Mibaba mikubwa lakini mmejawa na woga.

  Vunjeni mfe njaa kwa kuendekeza ufisadi.
   
 5. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Mtakao athirika ni nyinyi,sisi tumeshatamka muungano hatutaki ondoeni wanajeshi wenu hapa zanzibar,tumechoka kutawaliwa na muungano,Na hao wapemba watarudi tu kwao huku zanzibar na hawajafukuzwa etii,,mutaathirika nyinyi.

  Hatutaki muungano tena,tumechoshwa na vikao vya kupeana posho kwa kutatua kero,kwani ni kero ? Ni haki yetu kudai yale ambayo yamo ndani ya muungo na sio kiro,mbona hamuelewi...........
   
 6. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  nani atamfunga paka kengele? tunataka kiongozi wa serikali ya mapinduzi asimame na atamke kwamba hamuutaki muungano...
  hapo tutaelewa ila kwa kelele za kwenye mablogu, mnazuga tu!!!
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  ...Hata leo vunjeni tu hatuutaki sisi
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  May 27, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Tutaondoaje majeshi kwenye nchi yetu wandugu? Mbona mnakuwa vichwa maji hivyo? Tutaendelea kuweka majeshi ili kulinda nchi dhidi ya wenye kutaka kuisambaratisha nchi yetu, Tanzania! Nyinyi endeleeni kulilia kiti kwenye Umoja wa Mataifa alichokiacha Sultani wa Oman!
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  May 27, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mbona unadai eti "Wapemba watarudi kwao Zanzibar!" Kama kweli wanachukia Muungano kwa nini wasifungashe virago sasa hivi kimyakimya? Unafiki wote wa nini? Mbona mkipewa post bara hata isiyo ya Muungano mnaichangamkia kiulaini? Wonder shall never end!
   
 10. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #10
  May 29, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  kweli nyerere alikuwa clever! kwani amewaprogram watanganyika kuwa wajinga! kivipi? hebu jiangalieni mna resourses nyingi lakini hamjijuwi nini mnafanya. malizenu wazungu wanazichukuwa kama zao nyie mmelala na wala hamjui lini mtaamka kwa upofu wenu. watanganyika ni watu pekee barani africa wasio faidika na rasilimali zao. hebu angalia makampuni ya kigeni yanavyo kusanya jasholenu na kuwalisha wananchi wa kwao! hivi unajuwa ni kiasi gani unalipa kwa kumlisha muingereza mmoja akiwemo mzanzibar aishie kule? hivi unajuwa kiasi gani unamplipia mjapani kwao kwa dimond yako? hivi unajuwa hiyo text msg yako unayotuma kwa ule ujuha waliokuleteeni wazungu wa tuma ujumbe utajirike kuwa inawalipia wazungu kiasi gani kwao kwa huduza kilasiki kwao?
  watanganyika mko ziro katika africa mmejaa madeni ya ilhali ni matajiri wa rasilimali. watanganyika mpaka leo mnasomeshana kwenye mabanda ya mbuzi ilhali ni matajiri mno wa rasilimali na eti mna wasomi wa ceconomics ! watanganyika hamjui kusoma mikataba na ndiyo maana wazungu wanakupateni hapo kwa u-sifuri wenu
  watanganyika mmejaa ujinga ndiyo maana mnauwana kwa imani za ushirikina eti albino ukipata limbs zake utakuwa tajiri! munauwana na kuchunanan ngozi kwa imani mtakuwa matajiri! mara leo vita vya anchari na wanchoki kwa bangi tu! nyinyi watanganyika hadi leo mnajidai mmesoma wakati mmejaa ujinga munauwa vibaka na munawaabudu wezi wa mamilioni ya walipa kodi !
  hebu juilize ile gesi ya songosongo nani anafaidika?
  watanganyika mhhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 11. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
Loading...