McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 889
- 2,863
Wakuu,
Inaonekana kama Musiba baada ya kukatwa na CCM akili zimeanza kumrudi.
Leo akiwa anaongea na waandishi wa habari ameomba radhi watu wote ambao aliwakosea kipindi hicho na akaongeza kuwa kipindi kile alikuwa kijana tu.
Nadhani msamaha huu unawahusu sana wakina Fatma Karume na wengineo ambao walichafuliwa sana na huyu baba kipindi cha mwendazake
Mwanaharakati huru Cyprian Musiba amechutama na kuwaomba radhi wote aliowakosea na kuwafanyia mabaya siku za nyuma akidai kuwa yote aliyoyafanya ulikuwa ni ujana huku akiwasisitiza waafrika kutokuwa na visasi na kuacha kuweka vitu moyoni.
"Watu wananisema eti wewe ulikuwa unawaombea wenzako mabaya. Inawezekana nilikuwa kijana sana. Sasa hivi nimekuwa mtu mzima - akili zinakua, unabadilika, unakuwa na busara. Unajua kadri unavyozidi kukua, ndivyo unavyopata hekima, busara na utu. Wakati mwingine ujana sio mchezo.
"Kwahiyo waafrika tuna tatizo la visasi na sijui tutaacha lini, visasi sio vizuri, visasi pia vinasababisha nchi haiendi mbele inarudi nyuma tu, sasa msipende kuweka kitu moyoni, ni kitu kibaya sana kwasababu nchi hii ni yetu sote, mtu akikukosea kasirika hapo hapo mmalizane tu msameheane maisha yaendelee," amesema Cyprian Musiba.