Mungu nisifikie kukata tamaa

Mungu nisifikie kukata tamaa

Pole sana kwa kipindi unachopitia naamini ni wakati mgumu sana na sio tu kwa sababu huna pesa lah hasha unaweza ukawa na Pesa lakini bado ukapitia hali hiyo nakushauri nenda Kanisani utapata amani na pia omba sana uwe na amani Mungu ni mwema na mwaminifu atakusaidia.
ubarikiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rudi hom hujaua
Hiki kipindi napitia maisha magumu sana

Nimefukuzwa kazi

Nadaiwa kodi ya miezi mitatu

A 5000 ya umeme

Sina hela

Ndani nina unga tu mboga na hata mchele sina

Nipo mikoa ya mbali na nyumbani

Nimejifungia ndani nashindwa kutoka coz mama mwenye nyumba ni kivuruge na ananidai 5000

Nina mpenzi ambaye anajitahidi kufahamu kipindi ninachopitia ila bado hapati jibu coz i act as if sina matatizo

Nina siku mbili sijala kwa ridhaa yangu yaani nakula kwa kuibia

Natamani kurudi home nauli sina na naona ni udhaifu mkubwa kurudi kukaa na mama na am 24yrs old

Akili inachoka nahisi kuanguka

EEE MUNGU PAMOJA NA MAPITO HAYA NISIFIKIE KUKATA TAMAA

HAYA NI MADOGO KULINGANISHA NA WENZANGU

NISITAMANI KUJIUA

KWA AKILI YA KIBINADAMU UWEZO UNANISHINDA

NAKUOMBA MUNGU UTIMIZE HAJA ZA MOYO WANGUView attachment 1062423

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rudisha mpira kwa kipa, nakumbuka kipindi hiki kilinikuta nilimpoteza mchumba wangu hivihivi nikarudi home wazazi wakanitia nguvu nikarudi town tena kupanga mashambulizi huwa ni nyakati za mpito tu kuna neema yaja mbele usikate tamaa.Kuna wimbo wa Psquare (jina siukumbuki) ulikuwa unanifariji sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bring it on

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usikate tamaa..
Mimi niliachishwa kazi ghafla na nilikuwa na deni benki marejesho 159.500 kwa mwezi, nililima matikiti eka moja yakaoza yote shambani (vyote hv vilitokea kwa wakati mmoja) hapo naishi nyumba ya kupanga kuna kulipa kodi na umeme na maji....kilikuwa kipindi kigumu mno katika maisha yangu lkn sikukata tamaa.
Nilipambana hivyo hvyo wakati mwingine nakosa hela ya kula nakula kwa baba mwenye nyumba. Sikutafuta ndg wala kuenda nyumbani ( wazazi wangu walishafariki so sina nyumbani) Lakini nilivuka. Nilikuwa namchotea mchanga mama mmoja jirani, alikuwa anajenga ndo alikuwa ananipa hela kidogo napeleka benki mpaka deni likaisha


Ukisikia uanaume ndo huu...kikubwa ni kutokuwa a woga au aibu..hongera sana best
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom