Zuriel_cfc
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 4,096
- 9,074
Usikate tamaa..hujaipitia kipind ka hichi n shukuru napitia mimi pengine we ungejiua
Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi niliachishwa kazi ghafla na nilikuwa na deni benki marejesho 159.500 kwa mwezi, nililima matikiti eka moja yakaoza yote shambani (vyote hv vilitokea kwa wakati mmoja) hapo naishi nyumba ya kupanga kuna kulipa kodi na umeme na maji....kilikuwa kipindi kigumu mno katika maisha yangu lkn sikukata tamaa.
Nilipambana hivyo hvyo wakati mwingine nakosa hela ya kula nakula kwa baba mwenye nyumba. Sikutafuta ndg wala kuenda nyumbani ( wazazi wangu walishafariki so sina nyumbani) Lakini nilivuka. Nilikuwa namchotea mchanga mama mmoja jirani, alikuwa anajenga ndo alikuwa ananipa hela kidogo napeleka benki mpaka deni likaisha

