Mungu nisifikie kukata tamaa

Mungu nisifikie kukata tamaa

Usikate tamaa..
Mimi niliachishwa kazi ghafla na nilikuwa na deni benki marejesho 159.500 kwa mwezi, nililima matikiti eka moja yakaoza yote shambani (vyote hv vilitokea kwa wakati mmoja) hapo naishi nyumba ya kupanga kuna kulipa kodi na umeme na maji....kilikuwa kipindi kigumu mno katika maisha yangu lkn sikukata tamaa.
Nilipambana hivyo hvyo wakati mwingine nakosa hela ya kula nakula kwa baba mwenye nyumba. Sikutafuta ndg wala kuenda nyumbani ( wazazi wangu walishafariki so sina nyumbani) Lakini nilivuka. Nilikuwa namchotea mchanga mama mmoja jirani, alikuwa anajenga ndo alikuwa ananipa hela kidogo napeleka benki mpaka deni likaisha
I heart it!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom