Bundakwetu
JF-Expert Member
- Nov 18, 2022
- 551
- 1,006
Habari zenu wakuu poleni na shughuli, Niende moja kwa moja kwenye mada mwaka jana mwishoni baada ya kushindwa kuvumilia visa na dharau kwa aliyekuwa mke wangu pamoja na vikao vingi vya usuruhishi kugonga mwamba, Niliamua kuchukua uamuzi wa kumuachia mji mwanamke na mimi kwenda kuanza maisha mapya, roho iliniuma sana pale nilipoondoka na kuwaacha watoto wangu wakibugujikwa na machozi lakini niliwaahidi ipo siku nitakuwa nao tena, na siku ya leo Mungu amebariki nimetoka kuwapokea watoto wangu na nitaishi nao kwa shida na raha, Pongezi ziende kwa wote walionipa ushauri na wote walio nitia moyo, pia nampongeza Mwalim mkuu wa Shule ya walipokuwa wanasomea watoto wangu kwa kufanikisha zoezi la uhamisho wa watoto wangu toka Mwanza hadi kufanikisha kuhamia hapa Morogoro Mungu akulinde sana mwalim, Uhamisho umekamilika na wanangu wataanza maisha ya shule hapa morogoro ikumbukwe mimi niliondoka nikamuachia jukumu hilo Ubarikiwe sana Mwalimu, Mungu ni mwema sana. Kingine yule mwanamke nasikia pale kwangu imekuwa kama Danguro vijana wanapishana Usiku kwa mchana kupata huduma binafsi sina kinyongo nae wala wivu nae kwakuwa tumeshaachana na kila mtu na maisha yake na nyumba hiyo nimemuachia sina changu tena na hapa nilipo namshukuru Mungu nafanya kazi kwa bidii sana na mwanga nauona na ninaimani Mungu ataniwezesha kujenga makazi yangu mapya tena, Furaha niliyonayo leo kuwaona wanangu tena ni kubwa mno Asante Mungu bariki Kazi ya Mikono yangu.