Duniani kuna starehe, ila moja ya starehe bora duniani ni kumpata mke mwema

Mohamedex121

JF-Expert Member
Jan 27, 2022
1,688
3,142
Asalam aleykum.

Ndugu zangu hakika mke mwema ni starehe moja bora kabisa duniani hata ukiwa huna hela ila mke mwema ni kama tulizo la nafsi.

Image una maisha magumu, pesa unaipata kwa shida ila Mwenyezi Mungu akakujaalia mke mwema mwenye kufahamu qadari za Allah (S.W) akakuliwaza na magumu unayoyapita, akakutii na kujishusha mbele yako bila kujali kipato chako wala hadhi yako katika jamii, akawalea watoto wako katika misingi ya dini, akawa sababu ya yeye kukupatia kizazi chenye kukuombea dua hata ukifa leo wanao watakuwa msaada mkubwa kwako pindi utakapo kuwa kaburini.

Hivi Mungu akupe nini tena kingine? Hakika ukibahatika kuoa mke mwema mwenye hofu ya Mungu walahi umeyapatia maisha kwa 100% wala huitaji kitu kingine bali furaha na amani utakayo ipata kutoka kwa mwanamke mwema inatosha.

Namuomba Mwenyezi Mungu anijalie mke mwema pamoja na magumu ninayopitia ila kwa hakika nikipata mke mwema kwangu mimi inanitosha.

#Natanguliza shukurani wakuu
View attachment 2761215
 
Hilo liko wazi kabisa.

Ukipata mke mwema, dunia yoote unaona ya kwako, unaweza kujiuliza hawa mapimbi mbon hawaoi.

Subiri upate kivuruge, unaona jehanamu duniani.
Ni kuzidisha Dua katika maombi, Mungu akupe mtu sahihi kwenye mahusiano. Ili kumpata mtu sahihi wa kuwa naye katika ndoa ni kuamua kumpenda mtu kwa ajili ya Allah
 
Asalam aleykum.

Ndugu zangu hakika mke mwema ni starehe moja bora kabisa duniani hata ukiwa huna hela ila mke mwema ni kama tulizo la nafsi.

Image una maisha magumu, pesa unaipata kwa shida ila Mwenyezi Mungu akakujaalia mke mwema mwenye kufahamu qadari za Allah (S.W) akakuliwaza na magumu unayoyapita, akakutii na kujishusha mbele yako bila kujali kipato chako wala hadhi yako katika jamii, akawalea watoto wako katika misingi ya dini, akawa sababu ya yeye kukupatia kizazi chenye kukuombea dua hata ukifa leo wanao watakuwa msaada mkubwa kwako pindi utakapo kuwa kaburini.

Hivi Mungu akupe nini tena kingine? Hakika ukibahatika kuoa mke mwema mwenye hofu ya Mungu walahi umeyapatia maisha kwa 100% wala huitaji kitu kingine bali furaha na amani utakayo ipata kutoka kwa mwanamke mwema inatosha.

Namuomba Mwenyezi Mungu anijalie mke mwema pamoja na magumu ninayopitia ila kwa hakika nikipata mke mwema kwangu mimi inanitosha.

#Natanguliza shukurani wakuu
Amiiin
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom