Mke wangu kaniambia wenye pesa ndio waliomchelewesha kurudi usiku

george aloyce

JF-Expert Member
Aug 22, 2017
1,177
1,822
Naitwa John niko kwenye ndoa mwaka wa 9 na tumejaaliwa na mke wangu watoto wawili. Nilikuwa muajiriwa lakini niliacha kazi na kuanza biashara zangu binafsi miaka miwili iliyopita. Kiukweli mke wangu ni muajiriwa wa Serikali na kipato chake ni kikubwa kuliko mimi.

Msema kweli mpenzi wa Mungu tangu nilivyoacha kazi mke wangu kwa asilimia kubwa ndiye amekuwa akiibeba familia kwa mambo mengi yanayohusu pesa kuanzia nyumbani mpaka kwenye ada za watoto shule.

Nilichogundua kwa miaka hiyo miwili amekuwa haniheshimu hata kidogo yaani amekuwa akionesha dharau kubwa saa nyingine mpaka mbele za watoto wangu lakini nimekuwa nikimvumilia.

Kilichoniudhi kuliko vyote ni Jumamosi hii alirudi nyumbani usiku akiwa amelewa na nilipomuhoji akaniambia nikae kimya kwani wanaume wenzangu wenye hela zao ndio waliomnunulia pombe na ndio wanaompa hela za kutunza familia nikiwemo mimi.

Jambo hilo liliniuma sana na naomba nikiri kusema nililia kwa masaa mawili peke yangu. Cha ajabu asubuhi nilipomkumbusha akaniambia nimsamehe kwani zilikuwa pombe tu na hatarudia tena.

Naomba ushauri nifanyeje? Natamani kuondoka nikapange nyumba nyingine lakini watoto wangu sijui watanichukuliaje.
 
Hivi watu huwa mko serious kabisa kwamba una-expose matatizo yako kama hivi unategemea kupata msaada au inakuwa changamsha genge tu

We mwenyewe tatizo umeshaona ni kibunda kupungua then unaomba ushauriwe nini man,tafuta kibunda taratibu kama alipangwa kuwa na wewe milele atabaki tu kama haikupangwa piga goti shukuru Mungu endelea na safari
 
Naitwa John niko kwenye ndoa mwaka wa 9 na tumejaaliwa na mke wangu watoto wawili. Nilikuwa muajiriwa lakini niliacha kazi na kuanza biashara zangu binafsi miaka miwili iliyopita. Kiukweli mke wangu ni muajiriwa wa serikali na kipato chake ni kikubwa kuliko mimi. Msema kweli mpenzi wa mungu tangu nilivyoacha kazi mke wangu kwa asilimia kubwa ndiye amekuwa akiibeba familia kwa mambo mengi yanayohusu pesa kuanzia nyumbani mpaka kwenye ada za watoto shule. Nilichogundua kwa miaka hiyo miwili amekuwa haniheshimu hata kidogo yaani amekuwa akionyesha dharau kubwa saa nyingine mpaka mbele za watoto wangu lakini nimekuwa nikimvumilia. Kilichoniudhi kuliko vyote ni jumamosi hii alirudi nyumbani usiku akiwa amelewa na nilipomuhoji akaniambia nikae kimya kwani wanaume wenzangu wenye hela zao ndio waliomnunulia pombe na ndio wanaompa hela za kutunza familia nikiwemo mimi. Jambo hilo liliniuma sana na naomba nikiri kusema nililia kwa masaa mawili peke yangu. Cha ajabu asubuhi nilipomkumbusha akaniambia nimsamehe kwani zilikuwa pombe tu na hatarudia tena. Naomba ushauri nifanyeje? natamani kuondoka nikapange nyumba nyingine lakini watoto wangu sijui watanichukuliaje.View attachment 2867312


"kwenye ada za watoto"

Uanaume wako upo wapi sasa? Huna la kumfanya, chakula mpaka ada alipe yeye?
 
Wewe unazingua bhana! Mara mumeo malaya, sasa hivi mkeo ndio shida. Wewe jinsia gani? Acha utoto na kuleta visa vya huko fb kwa kina iddi makengo
Ahahaha!! Bora Bro, umeamua kumlipua...!! Me nimejaribu kudadisi ID yake na nyuzi anazoleta, automatically, nikavundua jamaa ni story-teller tena wa vijiweni Kama wachambuzi wa Mpira bongo
 
Naitwa John niko kwenye ndoa mwaka wa 9 na tumejaaliwa na mke wangu watoto wawili. Nilikuwa muajiriwa lakini niliacha kazi na kuanza biashara zangu binafsi miaka miwili iliyopita. Kiukweli mke wangu ni muajiriwa wa Serikali na kipato chake ni kikubwa kuliko mimi.

Msema kweli mpenzi wa mungu tangu nilivyoacha kazi mke wangu kwa asilimia kubwa ndiye amekuwa akiibeba familia kwa mambo mengi yanayohusu pesa kuanzia nyumbani mpaka kwenye ada za watoto shule. Nilichogundua kwa miaka hiyo miwili amekuwa haniheshimu hata kidogo yaani amekuwa akionesha dharau kubwa saa nyingine mpaka mbele za watoto wangu lakini nimekuwa nikimvumilia.

Kilichoniudhi kuliko vyote ni Jumamosi hii alirudi nyumbani usiku akiwa amelewa na nilipomuhoji akaniambia nikae kimya kwani wanaume wenzangu wenye hela zao ndio waliomnunulia pombe na ndio wanaompa hela za kutunza familia nikiwemo mimi. Jambo hilo liliniuma sana na naomba nikiri kusema nililia kwa masaa mawili peke yangu. Cha ajabu asubuhi nilipomkumbusha akaniambia nimsamehe kwani zilikuwa pombe tu na hatarudia tena.

Naomba ushauri nifanyeje? Natamani kuondoka nikapange nyumba nyingine lakini watoto wangu sijui watanichukuliaje.
Mumeo ana kazi kweli kweli.
 
Hakuna wanaume wapuuzi kama nusu ya walio kwenye ndoa.
Japokua ndoa ni jambo jema, lakini wengi wao wanapelekeshwa na wanawake kwa kisingizo cha watoto na kupata pakukojoa ovyo.
Upumbavu wa kiwango kikubwa huu.
Nasubiri niskie umejinyonga au upo jela kwa kuua mtu.
 
Back
Top Bottom