Mungu hayupo? Atheist njooni mthibitishe

Mungu hayupo? Atheist njooni mthibitishe

Si kwa ukali, halafu nani alisema ni lazima uwe na upande? (HILI NIJIBU)
Sijaelewa why umereply kwa ukali hivyo. Ila ni kawaida, ukianzisha mada lazima wewe uwe na upande, na huo upande lazima uwe na hoja zako ambazo zitafungulia mada, huwezi anzisha mada kwa heading tu

Pengine kama hukuelewa msingi wa huu uzi si kubishana, laa. Nimeufungua nikitaka kuwasikiliza ndugu zetu Atheists juu ya hoja zao za kukana uwepo wa Mungu wala sikuwaita nije kubishana nao.

Nililenga hilo ili nipata jifunza kitu toka kwao, na si habba kuna mambo kadhaa nayafahamu sasa.
 
Kuwepo na kutokuwepo kwa Mungu pia ni Mungu..Mungu ni kila kitu na kila kitu ni Mungu, Atheist pia ni Mungu...imani pia Mungu.. shetani ni Mungu na Mungu ni shetani..mwanzo ni Mungu na mwisho ni Mungu.
😂
 
Hivi unaweza kusibitisha kitu kisichowepo ??!
M nahisi kama tuwepo jangwani halafu usibitishe kwmba hmna msitu
 
Sasa unataka tuongelee muumba vyote wakati hata hatujui vyote ni nini?

Tutaongeleaje hilo?
Hivi si nimeipunguza upeo dhana ya “Vyote”? Nimeifafanua maana niliyoikusudia kusema hivyo tena kimahususi kabisa sijui kwanini hujanielewa.

Rejea maana ya “vyote” kama nilivyokusudia.
Yani hivi vichache tunavyoviona na kuvifahamu tu vinakanusha kuwepo kwa convergence kutokea Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, halafu unataka kuviongeza vyote ambavyo hatuvijui?
Twende na hivi vichache tunavyovijua…
Je, tunaweza hitimisha kuwa kwako wewe Bwana Kiranga dhana ya Mungu (IKIMAANISHA Muumba WA HIVI VICHACHE UNAVYOVIJUA, tuachane na Mungu wa hizo sifa unazozikataa twende na hii sifa ya Uumbaji) ni batili na kiumbe, nguvu, mtu au chochote kinachinasibishwa na dhana hiyo ya kuumba si halisi ila uzushi???
Let's talk about time.

Do you understand that the concept of time is not fundamental and absolute, and that it is relative and not absolute, and that your question of "before, now, and after" is rather anthropic?

Wewe ni kama mtu uliye katika gari linalokimbia kwa kasi, unafikiri kila mtu yupo katika gari anakwenda kwa mwendo wa kasi.

Hujui kwamba hilo gari kwenda kwa mwendo wa kasi ni a derivative of a still background that does not necessarily move.

Time is neither fundamental nor absolute.

Sasa utasemaje kilichopita, kilichopo na kinachokuja wakati dhana nzima ya sasa inategemeana na mtizamaji ni nani?
Msingi huo mtazamaji ni wanaadamu wa zama hizi za sasa… kwetu yaliyopita ni yaliyopita tu au una maana nyingine ya yaliyopita?
Kilichopita kwa nani? N nakwa nini kwa huyo?
Kwetu sisi wanaadamu wa zama za sasa.
Unajua kwamba baba yako aliyekuzidi miaka 40 anaweza kukuacha hapa leo akafanya safari na kurudi yuko kijana kwa miaka mingi kuliko wewe, kwa sababu ya effects za time dilation at near relativistic speeds?
Hapana sijui, vyema uthibitishe hili, na kama kuna mfano hai wa mtu aliyefanya hivyo itakuwa vizuri zaidi mkuu.
Time is relative, neither fundamental, nor absolute.

Why are you making it fundamental and absolute?
Wapi nimeifanya “fundamental” na “absolute”?
 
Hivi unaweza kusibitisha kitu kisichowepo ??!
M nahisi kama tuwepo jangwani halafu usibitishe kwmba hmna msitu
Mkuu habari za asubuhi,

Mfano wako wa Jangwani hauendani na dhana ya MUNGU kama inavyofafanuliwa na Waumini.

Jangwa ama misitu ni vitu vipo tu
Mungu, kama anavyofafanuliwa na waumini, si kitu kama Jangwa, yeye ndiye aliyeumba Jangwa na Misitu, akaumba macho na kuyapa uwepo aidha yaone ama yasione kama huo msitu au jangwa vipo au havipo, juu ya yote Mungu hathibitiki kwa kuonekana maana hakuna aliyewahi muone tofauti na jangwa au misitu ambavyo iila mtu huweza vione ila vipofu na wafu.

Karibu,
 
Hivi si nimeipunguza upeo dhana ya “Vyote”? Nimeifafanua maana niliyoikusudia kusema hivyo tena kimahususi kabisa sijui kwanini hujanielewa.

Rejea maana ya “vyote” kama nilivyokusudia.

Twende na hivi vichache tunavyovijua…
Je, tunaweza hitimisha kuwa kwako wewe Bwana Kiranga dhana ya Mungu (IKIMAANISHA Muumba WA HIVI VICHACHE UNAVYOVIJUA, tuachane na Mungu wa hizo sifa unazozikataa twende na hii sifa ya Uumbaji) ni batili na kiumbe, nguvu, mtu au chochote kinachinasibishwa na dhana hiyo ya kuumba si halisi ila uzushi???

Msingi huo mtazamaji ni wanaadamu wa zama hizi za sasa… kwetu yaliyopita ni yaliyopita tu au una maana nyingine ya yaliyopita?

Kwetu sisi wanaadamu wa zama za sasa.

Hapana sijui, vyema uthibitishe hili, na kama kuna mfano hai wa mtu aliyefanya hivyo itakuwa vizuri zaidi mkuu.

Wapi nimeifanya “fundamental” na “absolute”?
Unakubali au unakataa logical consistency kama msingi wa kutupeleka kwenye kujua ukweli?
 
Mungu ni mfano wa kila kitu na Kila kitu ni Mungu... shetani ni Mungu na Mungu ni shetani.. mwanzo ni Mungu mwisho ni Mungu... Atheist pia ni Mungu...Imani ya Mungu yupo au hayupo pia Mungu..maana yeye ndio chanzo cha kila kitu.
 
Unakubali au unakataa logical consistency kama msingi wa kutupeleka kwenye kujua ukweli?
Mbona hujibu swali badala yake unauliza swali?

Kama huna majibu hakuna ubaya kusema hauna maana hakuna ajuae kila kitu.
 
wakija kudhibitisha ni kutaka kujengea watu imani flani tu bila udhibitisho unaoingia akilin , hyo imani ya kuamn Mungu hayupo haina tofauti na iman ya din flan tu, waulize ni nguvu gani ilipangilia mifumo mbalimbali kiustadi bila kuathiri viumbe hai , wanasema wanaamni sayansi waulize sayansi inaweza simama bila kutegemea rawmaterial iliyokuwepo tu bila ufundi kutoka kwa binadamu? waulize ni nguvu gani na intelligence ipi inayofanya kazi ndani sperm kuunda kiumbe kilicho na mifumo na mipangilio maalumu ? ni kitu gan kiliweka sukari ndan ya muwa na kwa dhumuni lipi je ilitokea tu bila nguvu na inteligence yoyote?
Asee nimekuelewa sana mkuu,hii mada imeisha tayari
 
Unaposema Mungu unamaanisha nini?

Maana hata Beyonce mke wa Jay-Z kuna watu wanamkubali kama Mungu wao.

Na kwa definition yao ya Mungu siwezi kuwakatalia na kusema kwamba Beyonce mke wa Jay-Z hayupo.

Mungu ni nini? Na unathibitishaje hilo jibu lako?
Mungu ni mtu yeyote mwenye nguvu za kipekee, Mungu ni uwezo wa juu yaa...
 
Mbona hujibu swali badala yake unauliza swali?

Kama huna majibu hakuna ubaya kusema hauna maana hakuna ajuae kila kitu.
Maswali yote uliyouliza na utakayoweza kuuliza yanarudi kwenye swali hili la msingi.

Sasa mimi napunguza mazungumzo marefu ambayo yana matatizo mengi ya tafsiri, levels za uelewa wa physics na hesabu na mambo mengi sana, nakwenda kwenye swali la msingi kuliko yote.

Kama hujui logical consistency ni nini unaruhusiwa kunijibu kwa swali pia, mimi sina tatizo kujibiwa swali kwa swali as long as swali liko relevant.

Na pia, ukushangaa mtu kujibu swali kwa swali inaonekana hujajua the Socratic Method.

Which troubles me.
 
Mungu ni mfano wa kila kitu na Kila kitu ni Mungu... shetani ni Mungu na Mungu ni shetani.. mwanzo ni Mungu mwisho ni Mungu... Atheist pia ni Mungu...Imani ya Mungu yupo au hayupo pia Mungu..maana yeye ndio chanzo cha kila kitu.
Hapo ni sawa na unafanya hesabu kwa kusema kila namba ni sawasawa na kila namba nyingine.

Huna hesabu hapo, una vurugu tu.
 
Mungu ni mtu yeyote mwenye nguvu za kipekee, Mungu ni uwezo wa juu yaa...
Uwezo wa kipekee ni nini? Kila mtu ana uwezo wa kipekee wa kujijua yeye kama yeye ambao mtu mwingine yeyote hana, je, hilo linamfanya kila mtu awe Mungu?
 
Hapo ni sawa na unafanya hesabu kwa kusema kila namba ni sawasawa na kila namba nyingine.

Huna hesabu hapo, una vurugu tu.
Sawa mkuu, sasa tupe maoni na mawazo yako ni yapi, kwa nini tuna exist? Kama huamini Mungu yupo ni kitu gani kilipeleka Existence ya dunia na vitu vilivyomo na binadamu kuwepo..?? Na kama Mungu hayupo kwa nini binadamu hatuna Ukuu na nguvu kwa baadhi ya mambo mfano majanga ya asili Earthquakes,floods,vimbunga... tunashindwa kuyazuia yasitokee...sasa nani msababishi wa hivi vitu kama Mungu hayupo?

Hizi Sayansi zetu na nguvu zetu wanadamu mbona zinashindwa kwa baadhi ya mambo?
 
Uwezo wa kipekee ni nini? Kila mtu ana uwezo wa kipekee wa kujijua yeye kama yeye ambao mtu mwingine yeyote hana, je, hilo linamfanya kila mtu awe Mungu?
Ndio,watu kama Pele,Ronaldo, Messi,Maradona n.k walikuwa na uwezo wa kipekee kwa hiyo tunaweza kuwaona ni miungu wa soka.
 
Ndio,watu kama Pele,Ronaldo, Messi,Maradona n.k walikuwa na uwezo wa kipekee kwa hiyo tunaweza kuwaona ni miungu wa soka.
Hujajibu swali la msingi, linalouliza uwezo wa kipekee ni nini?

Umetoa mifano tu.

Kutoa mfano si kutoa definition, unaelewa hilo?

Uwezo wa kipekee ni nini?

Unajuaje huyu ana uwezo wa kipekee, na huyu hana, hususan kama huyo unayemtahini ni mtu pekee ambaye ndiye yeye katika ulimwengu mzima na hivyo kila atakachokifanya ni cha kipekee kwa sababu hakuna yeye mwingine!
 
Sawa mkuu, sasa tupe maoni na mawazo yako ni yapi, kwa nini tuna exist? Kama huamini Mungu yupo ni kitu gani kilipeleka Existence ya dunia na vitu vilivyomo na binadamu kuwepo..?? Na kama Mungu hayupo kwa nini binadamu hatuna Ukuu na nguvu kwa baadhi ya mambo mfano majanga ya asili Earthquakes,floods,vimbunga... tunashindwa kuyazuia yasitokee...sasa nani msababishi wa hivi vitu kama Mungu hayupo?? Hizi Sayansi zetu na nguvu zetu wanadamu mbona zinashindwa kwa baadhi ya mambo????
Kwa nini unafikiri unaweza kuelewa kwa nini tuna exist, au hata kuwa suala zima la kitu kimoja kusababisha kingine - linaloleta hoja ya kwa nini tuna exist- ni suala la msingi na lenye mantiki?

Unaelewa nini kuhusu "the anthropic principle" na tatizo la watu kuangalia mambo makubwa sana yaliyowapita scale au madogo sana waliyoyapita scale kwa scale yao?

Umechunguza vipi suala la cause and effect kujua matatizo yako kwa kiwango cha msingi kabisa?

Unaelewa ukikazia swali la kwa nini hiki kipo hapa, na hiki kipo hapa kwa hivyo kiliwekwa hapa na kingine, utaishia kuhitimisha kwamba hakuna Mungu? Kwa sababu hata Mungu naye atahitaji kutoka kwingine na kuanzishwa na kingine, na hapo ikishakuwa hivyo, Mungu huyo atakuwa si Mungu tena?

Unauliza kama Mungu hayupo kwa nini ukuu na nguvu kwa badhi ya mambo mfano majanga ya asili? Hatuna nguvu kwa sababu ulimwengu huu ambao hauna Mungu na ambao sisi watu hatuna upekee wowote haulazimiki kutupa nguvu juu ya mambo hayo.

Unauliza kwa nini huyu mtoto yatima ambaye hana baba wala mama amekosa chakula, kama hana baba na mama si angekuwa na chakula? Hapana, swali lako unauliza kinyume, mtoto yatima hana chakula kwa sababu hana mzazi wa kumpa chakula, huko kukosa chakula kunaendana na mtoto kukosa wazazi, angekuwa na wazazi tungehoji kwa nini mtoto mwenye wazazi kakosa chakula, ila huyu ambaye hana wazazi kukosa chakula si jambo la ajabu.

Kwenye ulimwengu ambao hauna Mungu, watu kukosa nguvu juu ya majanga ya asili hakuna kitu cha ajabu, asili haishurutishiki kutupa nguvu juu ya majanga ya asili, Mungu hayupo, angekuwepo angeweza kutupa nguvu juu ya majanga ya asili. Kwa hivyo ulimwengu huu hauna cha ajabu. Cha ajabu ni pale una[posema kuna Mungu, mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, halafu kaumba ulimwengu wenye majanga ya asili yanayoumiza sana viumbe wake anaowapenda, na viumbe hao hawawezi kunusurika, hapo tiunaona hiyo story ina mushkeli, ina logical inconsistency, ina contradiction.

Ukimuondoa huyo Mungu, ukasema Mungu hayupo, habari nzima inaweza kueleweka bila logical inconsistency, bila mushkeli, bila contradiction.

Kwa nini unauliza nani anasababisha vimbunga? Kwa nini swali lako linakuwa "nani" badala ya "nini"?
Huoni kwamba swali lako lenyewe lishalenga jibu fulani? Unajua tofauti ya "nani" na "nini"?

Unaposema sayansi zinashindwa kwa baadhi ya mambo, unaelewa sayansi ni nini? Kwani sayansi ilisema wapi kwamba ina jibu la kila kitu? Na sayansi isipokuwa na jibu, hilo linathibitisha nini? Je, hilo linathibitisha Mungu yupo?

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
 
Back
Top Bottom