Mungu hayupo? Atheist njooni mthibitishe

Kwa nini unafikiri unaweza kuelewa kwa nini tuna exist, au hata kuwa suala zima la kitu kimoja kusababisha kingine - linaloleta hoja ya kwa nini tuna exist- ni suala la msingi na lenye mantiki?

Unauliza kama Mungu hayupo kwa nini ukuu na nguvu kwa badhi ya mambo mfano majanga ya asili? Hatuna nguvu kwa sababu ulimwengu huu ambao hauna Mungu na ambao sisi watu hatuna upekee wowote haulazimiki kutupa nguvu juu ya mambo hayo.

Unauliza kwa nini huyu mtoto yatima ambaye hana baba wala mama amekosa chakula, kama hana baba na mama si angekuwa na chakula? Hapana, swali lako unauliza kinyume, mtoto yatima hana chakula kwa sababu hana mzazi wa kumpa chakula, huko kukosa chakula kunaendana na mtoto kukosa wazazi, angekuwa na wazazi tungehoji kwa nini mtoto mwenye wazazi kakosa chakula, ila huyu ambaye hana wazazi kukosa chakula si jambo la ajabu.

Kwenye ulimwengu ambao hauna Mungu, watu kukosa nguvu juu ya majanga ya asili hakuna kitu cha ajabu, asili haishurutishiki kutupa nguvu juu ya majanga ya asili, Mungu hayupo, angekuwepo angeweza kutupa nguvu juu ya majanga ya asili. Kwa hivyo ulimwengu huu hauna cha ajabu. Cha ajabu ni pale una[posema kuna Mungu, mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, halafu kaumba ulimwengu wenye majanga ya asili yanayoumiza sana viumbe wake anaowapenda, na viumbe hao hawawezi kunusurika, hapo tiunaona hiyo story ina mushkeli, ina logical inconsistency, ina contradiction.

Ukimuondoa huyo Mungu, ukasema Mungu hayupo, habari nzima inaweza kueleweka bila logical inconsistency, bila mushkeli, bila contradiction.

Kwa nini unauliza nani anasababisha vimbunga? Kwa nini swali lako linakuwa "nani" badala ya "nini"?
Huoni kwamba swali lako lenyewe lishalenga jibu fulani? Unajua tofauti ya "nani" na "nini"?

Unaposema sayansi zinashindwa kwa baadhi ya mambo, unaelewa sayansi ni nini? Kwani sayansi ilisema wapi kwamba ina jibu la kila kitu? Na sayansi isipokuwa na jibu, hilo linathibitisha nini? Je, hilo linathibitisha Mungu yupo?

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Siwezi kuthibitisha uwepo wa Mungu..kama sayansi haiwezi kuthibitisha uwepo wa kila kitu..Ni kitu gani kinasababisha majanga ya asili yatokee ni nini hicho?????
 
Labda tuligeuze swali ili kulichambua vizuri.

Kwa nini majanga ya asili yasitokee?

Katika ulimwengu ambao unaenda kwa kanuni za kifizikia tu, ambazo zinaruhusu majanga ya asili yaweze kutokea, kwa nini majanga ya asili yasiweze kutokea?

Majanga ya asili yote yanaweza kuelezewa kisayansi. Hakuna janga la asili linalovunja kanuni za kiasili za kisayansi.

Sasa kwa nini yasitokee?

Hiyo asili yenyewe haioni hayo majanga kama majanga, hayo unayoyaita majanga ya asili ni sehemu ya asili tu, wewe ndiye unayaita majanga kwa sababu yanakuumiza.

Sasa swali linakuja, katika ulimwengu huu unaoenda bila kukuheshimu wewe kama mtu, ulimwengu unaofuata sheria za asili tu, kwa nini haya unayoyaita majanga yakuheshimu wewe yasikutokee?

Yani unataka mtu akudondoshee jiwe kutoka juu, halafu jiwe likuogope lisikuangukie na kupinga kanuni za physics?

Unataka kimbunga kikupishe wewe na kupindisha kanuni za physics?

Unaelewa ulimwengu wenye majanga unaonesha Mungu hayupo, hauoneshi Mungu yupo?
 
Sasa ulimwengu ulijiumba wenyewe na binadamu wakafuatia ama nini kilianza kabla ya mwenzake?
 
Unapoandika "ulimwengu ulijiumba wenyewe" unamaanisha nini?

Kwa kufuatisha sayansi inayojulikana, watu - si binadamu- wametokea muda mfupi tu uliopita.

Kama historia ya dunia - wala si ulimwengu, dunia tu- mpaka sasa, tukiifanya kuwa sawa na siku moja yenye masaa 24, watu wamekuja kutokea kwenye sekunde ya mwisho kabisa, yani saa 5 na dakika 59 na sekunde 59 ya siku hiyo.

Yani katika historia hiyo ya dunia ambayo tumeifanya iwe sawa na masaa 24, masaa 23 na dakika 59 na sekunde 59 dunia haikuwa na watu.
 
Hujajibu swali la msingi, linalouliza uwezo wa kipekee ni nini?

Umetoa mifano tu.

Kutoa mfano si kutoa definition, unaelewa hilo?

Uwezo wa kipekee ni nini?

Unajuaje huyu ana uwezo wa kipekee, na huyu hana, hususan kama huyo unayemtahini ni mtu pekee ambaye ndiye yeye katika ulimwengu mzima na hivyo kila atakachokifanya ni cha kipekee kwa sababu hakuna yeye mwingine!
Kipekee: uwezo usioweza kufikiwa na mwingine.
Mungu ana uwezo wa kipekee sababu hakuna mtu alieweza kufanya aliyofanya yeye
 
Unapoandika "ulimwengu ulijiumba wenyewe" unamaanisha nini?

Kwa kufuatisha sayansi inayojulikana, watu - si binadamu- wametokea muda mfupi tu uliopita.

Kama historia ya dunia - wala si ulimwengu, dunia tu- mpaka sasa, tukiifanya kuwa sawa na siku moja yenye masaa 24, watu wamekuja kutokea kwenye sekunde ya mwisho kabisa, yani saa 5 na dakika 59 na sekunde 59 ya siku hiyo.

Yani katika historia hiyo ya dunia ambayo tumeifanya iwe sawa na masaa 24, masaa 23 na dakika 59 na sekunde 59 dunia haikuwa na watu.
Sasa mkuu..Nieleze maoni na mtazamo wako juu ya hii Dunia...moja dunia ilianza vipi? Wanadamu wali anza vipi? Kwa nini tunakufa na hatuwezi kuzuia kifo?
 
Kipekee: uwezo usioweza kufikiwa na mwingine.
Mungu ana uwezo wa kipekee sababu hakuna mtu alieweza kufanya aliyofanya yeye
Sawa.

Tuseme napenda kukubaliana na wewe. Mimi pia kimsingi ningependa sana Mungu awepo. Ulimwengu ambao una Mungu ungenipunguzia matatizo mengi sana, hivyo ningefurahi sana kujua kwamba fikra zangu kwamba Mungu hayupo zina makosa, na kiukweli Mungu yupo.

ila nina tabia ya kuhakiki mambo kabla ya kuyakubali.

Hivyo, sina tatizo kukukubalia, ila nataka kuhakikisha mambo tu kabla sijakubali.

Unajuaje uwezo huo upo kweli, na si kitu ulichokifikiria tu mawazoni kwako wewe na watu mnaoamini uwepo wa Mungu, aghalabu kwa kurithishana kwenye hadithi, mapokeo, vitabu, uvivu wa kufikiri unaofanya kutojua jibu kufanywe kuwa ni kujua jibu, kuwa jibu la kisichojulikana ni Mungu huyo, wakati kiukweli uwezo huo haupo na hata huyo Mungu hayupo?
 
Sasa mkuu..Nieleze maoni na mtazamo wako juu ya hii Dunia...moja dunia ilianza vipi? Wanadamu wali anza vipi? Kwa nini tunakufa na hatuwezi kuzuia kifo?
Kwa nini unafikiri nina majibu haya au hata ninaweza kuwa na majibu ya maswali haya?

Kwa nini mtazamo wangu uwe muhimu kuliko utaalamu uliokubalika na kuchunguzwa na mchakato mzima unaorejewa na kuthibitishwa na dunia ya kisayansi?

Mimi ni atheist. Atheism ni kukataa uwepo wa Mungu. Si kusema kwamba tunajua dunia imeanzaje, maisha yameanzaje.Sijawahi kusema najua majibu ya maswali haya nje ya kusema kwamba najua Mungu si jibu sahihi, kwa sababu hayupo.

Ninachojua ni kwamba hatumhitaji Mungu kuelezea yote hayo, in fact theory ya Mungu inakuwa contradicted na dunia tunayoiona, watu wanavyoishi na kufa.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo, wote tungekuwa na uelewa mzuri na hata mjadala juu ya uwepo wake usingekuwepo na kusingekuwepo na kifo.

Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao kumjua yeye tu ni jambo lenye utata mwingi sana na ugomvi mwingi sana, mpaka watu wanauana kwa vita vya kidini? Kwa nini hajafanya dunia yote imjue kiukweli na usawa bila utata wala kuhitaji kitabu, mahubiri, tafsiri, mijadala ya JF, na kadhalika?

Kifo kibaya, kinatenganisha wanaopendana.Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aruhusu ulimwengu ambao unaweza kuwa na kifo na kutengenisha viumbe wake anaowapenda na wanaopendana? Huyo Mungu anayeachia viumbe wake wafe wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao hauwezi kuwa na kifo ana upendo gani?

Wewe Baba yako akiwa na uwezo wa kufanya familia yenu mtu asife, wote muishi vizuri tu miaka yote, ana uwezo wa kutatua tatizo lolote, halafu akaruhusu ndugu zako wote wafe, utasema huyo Baba yako ana upendo kweli?

Dunia ilianzaje?

Tunakufa na hatuwezi kuzuia kifo kwa sababu seli zetu zinakufa kwa kufuata second law of thermodynamics

Jumuiya ya sayansi inachunguza chanzo cha maisha bado, lakini kuna ushahidi mkubwa kwamba maisha yalianza baada ya replication ya RNA au molecule kama RNA.

Habari zote hizo hazimuhitaji Mungu, ukimuingiza Mungu hapo unalazimisha tu.
 
Duuuuh!! Salute kwako mkuu[emoji119][emoji119]Hoja zako zina fikirisha sana...sina cha zaidi..[emoji1666][emoji2]
 
mkuu ingekua hoja zako zinamashiko watu wangeshazifuata, unafikiri waamin Mungu hawazijui
Unadhani kwa nini ni maarufu humu jukwaani?

Unadhani amewafumbua macho watu wangapi kutoka kwenye huo utopolo?

Kiranga si saizi yako?

Watu wengi wanamfatilia na kukubaliana na kile anachokiandika ila hawakomenti.
 
tatua changamoto zako za kimaisha kwanza then ujibu comment zangu.
 
Unadhani kwa nini ni maarufu humu jukwaani?

Unadhani amewafumbua macho watu wangapi kutoka kwenye huo utopolo?

Kiranga si saizi yako?

Watu wengi wanamfatilia na kukubaliana na kile anachokiandika ila hawakomenti.
unaongelea size unadhani nani anashindana na huyo mpumbavu na maskini
 
Haya Tajiri
Inaonekana upo kwenye mabilionea kumi wanaoongoza Afrika.
Naona mbwata zimeitika? simjui na wewe pia sikujui ila inaonyesha ulivyo mjinga
 
Kwa nini unadhani nina changamoto za maisha?
Kwa nini hudhani nimeshindwa kutatua?
Akili kisoda.
mim na ww nan kisoda? ni binadamu gani asie na changamoto? tz tuna vijana wa ovyo ndo maana tunapitwa na wakati kwenye soko la dunia.
 
Dini zilikuwepo tangu enzi na enzi, jamii za wanaadamu zimekuwa zikiabudu vile wanavyoviita Mungu kwa miaka mingi sana hili halina ubishi.

Uwepo wake miaka mingi haina maana ni sahihi kuwepo wake maana hata uongo usipodhihirika huonekana ukweli miaka yote mpaka ukweli utakapofahamika.

Ila kuna sehemu ya watu kwenye jamii wamekuwa wakitilia mashaka na kukosoa wazo lenyewe la kuwepo kwa huyo anaeitwa Mungu. Wanaoamini (imani yoyote tu ‘as long as’ wanamuabudu wanachokiita Mungu) wanasistiza kuwa yupo na uwezo wake ni Mkuu sana.

Hoja za waumini nazifahamu baadhi, ila hoja za Atheist sijazielewa.

Ningependa kuwaelewa zaidi Atheists, Karibuni hapa Atheist walau mthibitishe (kama mtaweza) kuwa huyo wa kuitwa Mungu hayupo.

Lakini kwanza ni lazima tufafanue nini maana ya MUNGU, kwa maana kukurupuka kujibu swali ilhali hatujui maana ya dhana ya msingi wa swali itakuwa ni uhayewani wa kiwango cha juu sana.

Karibuni sana!
View attachment 2355249
kwa ufup tu ni kuwa maana ya neno Mungh ni cheo like Rais or wazili ndo maana hata Wachaw wanamtaja mungu wanao mjua so hata wq unawza chonga jiwe ukaliita mungu wako kwa sababu mungu ni jina la cheo tu.

Ila Jina la Mungu ambaye ni muweza yotw anaitwa Yehova. Isaya 42:8
na jina hilo ndo linamtofautsha na miungu mingne.
 
Haya Tajiri
Inaonekana upo kwenye mabilionea kumi wanaoongoza Afrika.
Naona mbwata zimeitika? simjui na wewe pia sikujui ila inaonyesha ulivyo mjinga
huyu Mungu unaemkashfu kanipa utajiri ww utaniambia nn mm?
 
Tajiri huwa hajisemi,
Ila mlamba chunvi mmoja, mwenye pesa ya kubadilishia mboga unajiona tajiri?
Embu zitaje amali zako hapa ili tujue?
 
mim na ww nan kisoda? ni binadamu gani asie na changamoto? tz tuna vijana wa ovyo ndo maana tunapitwa na wakati kwenye soko la dunia.
Tatizo umekariri dogo?
Sio kila mtu ana changamoto au anapitia changamoto
Kama unazo hizo za kwako akili kisoda
 
Back
Top Bottom