Mungu hayupo? Atheist njooni mthibitishe

Mungu hayupo? Atheist njooni mthibitishe

unaongelea size unadhani nani anashindana na huyo mpumbavu na maskini
Elimu ya mjinga ni Majungu...mtu humjui una anzaje kumuita mpumbavu na maskini au kwa vile anaenda kinyume na imani yako na mawazo yako? Wewe ndio mjinga kudhani kila mtu anafikiria sawa na kichwa chako...Kama huna hoja tulia,nyamaza usikashifu watu kwa matusi si kwamba hatuwezi tumia hayo matusi ila tunataka Hoja fikirishi...wewe kama huna cha kusema toka humu jukwaani!

Sio kukashifu mawazo ya watu....ndio maana ya "JF where we dare to talk openly"....sasa Mawazo yako mgando acha huko huko njoo na Hoja......
 
Wanadamu na sayansi yetu ndogo hapa duniani ya Technology kama ya mtu aliyeanzishaa internet ni ndogo sana, ila sisi tumeona kubwa na kwavile tuliumbwa kwa mfano wa Mungu roho zetu basi tunajikuta wajuaji kama Shetani na kujiona miungu watu.

Kosa lile lile walilolifanya Israel na mataifa Mengine kuabudu miungu..

Na mwisho wa Dhambi hiyo ni mauti.

Athiest wanajikutaga wanajua kinoma na kutegemea akili zako ndio Mwanzo na Mwisho wa hekima hapa duniani hawajui wala kuamini Yupo mwenye hekima zaidi Yetu na Akili zake hazichunguziki.
Wewe baki na imani yako inavyo kuaminisha na Atheist pia wana Imani zao pia za kutokuwepo Mungu... usihalalishe imani zako kwa watu maana na wewe huna uthibitisho wa ku prove zaidi ya kuegemea maandiko yako ya KIDINI...
 
Elimu ya mjinga ni Majungu...mtu humjui una anzaje kumuita mpumbavu na maskini au kwa vile anaenda kinyume na imani yako na mawazo yako? Wewe ndio mjinga kudhani kila mtu anafikiria sawa na kichwa chako...Kama huna hoja tulia,nyamaza usikashifu watu kwa matusi si kwamba hatuwezi tumia hayo matusi ila tunataka Hoja fikirishi...wewe kama huna cha kusema toka humu jukwaani! Sio kukashifu mawazo ya watu....ndio maana ya "JF where we dare to talk openly"....sasa Mawazo yako mgando acha huko huko njoo na Hoja......
mkuu hili ni jukwaa huru hongera pia kwa uhuru wako
 
mkuu nimechagua kuwasilisha nilichowasilisha kwa uhuru kabsa bila kupangiwa na mtu kwa hyo ata ww usinipangie nisemeje
 
Mimi binafsi maongezi yangu niliyoyafanya JF miaka yote kuhusu uwepo wa Mungu hayajafikia hata 5% ya maongezi ninayoweza au ninayotaka kuyafanya.

Kwa sababu watu wengi wanajadili dhana hii kwa upeo finyu wa dini zao. Na inakuwa vigumu kuendeleza mazungumzo ngazi ya tatu wakati hata ya kwanza hatujamaliza. Inakuwa sawa kutaka kujadiliana hesabu za Poincare's Conjecture level ya Grigori Perelman na mtu ambaye hajui kujumlisha na kutoa.

Hivyo hatujafikia kuzungumzia hata dhana kama pantheism, deism, na nyingine nyingi.

Mara nyingi watu huanzia na Mungu anayetajwa kwenye dini kubwa. Maana huyo ndiye anayetajwa sana.

Mfano, mimi mara nyingi ninapopinga uwepo wa Mungu, humtambulisha kwa sifa kama kusema "Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote".

Huyu ndiye Mungu anayetajwa kwenye misahafu ya Uyahudi, Ukristo, Uislamu na mingine mingi tu.

Mungu huyu ni dhana tu, hayupo kwenye uhalisia.

Dhana ya kuwepo Mungu huyu inapingana na ulimwengu unaoruhusu mabaya. Ama una ulimwengu unaoruhusu mabaya na Mungu huyu hayupo, ama Mungu huyu yupo na ulimwengu unaoruhusu mabaya haupo.

Ulimwengu unaoruhusu mabaya upo.

Hivyo, Mungu huyo hayupo.

This is basic logical consistency.

Mungu huyo kuwepo ni contradiction kama kuwepo kwa pembetatu ambayo hapo hapo ni duara katika planes za Euclidian geometry.

Ni contradiction kama 10 kuwa square root ya 2 katika base 2 mathematics.
Kijana kila siku huwa nakwambia kadhia ya kumjadili Mola ishakushinda na hutawahi kuja kuwa na hoja.

Kila siku unarudia yale yale, maswali hujibu hapa unakuja kujifaragua kwamba tangu uanze kujadili hili ni 5% tu umetumia. Kwanini unaandika uongo ? Mara ngapi najadiliana na wewe unakimbia maswali.

Umeandika suala la dhana ambazo hujawahi kuziongelea hizo siyo hujawahi kuziongelea Bali hazi jibu hoja katika kadhia hii.

Uwepo wa Mola ni uhalisia, ndiyo maana mpaka unakufa hutaweza walau kuharibu tu kukana kutokuwepo kwa Mola.

Nilishakwambia siyo kila unachokiona kina uta (contradiction) basi kina uta kweli, utata mara nyingi husababishwa na ujinga wa Mtu husika. Mfano wako ni wewe kuwa mjinga na usiye tumia akili unaona utata ila kiuhalisia hakuna utata.

Mfano nikikuuliza swali, tuthibitishie ya kuwa Mola hayupo na kwamba hii ni dhana. Dhana tamko hili Lina maana zaidi ya Moja Kuna wakati humaanisha hakika ya jambo baada ya ithibati na maana nyingine ni wazo tu. Sasa tujadili kwa maana hii ya pili. Thibitisha ya kuwa Mola kuwepi kwake ni dhana. Kisha utuambie dhana hii ilianzishwa na nani na lini.

Kuwepo kwa mabaya kunathibitisha juu ya uwepo wa Mola mwenye uwezo wote ndiyo maana akaruhusu mabaya yawepo. Sasa unapo mfasili Mola kwa upande mmoja huo ni uchachefu wa akili na Mola hufanya kila jambo kwa hekima.
 
Unasema kikombe kipo na Mimi ninasema hakipo halafu unanitaka Mimi ninaesema hakuna kikombe ndio nithibitishe, badala ya wewe unaesema kipo.

Wewe unaesema mungu yupo thibitisha na sio athibitishe anaesema mungu Hayupo.
Sijawahi kuona mkana mungu ana hoja. Shida yenu huwa waoga na mnakimbia jukumu la kuthibibitisha na liacha jukumu Hilo kwa mwenye kusadili. Ukisoma vitabu vya Elimu ya mijadala husema hivi mara nyingi mwenye kukanusha hutangulizwa katika kuthibitisha jambo husika sababu hudhaniwa ya kuwa yeye ana Elimu zaidi ya yule anae sadikisha na mara chache mwenye kusadiki hutangulizwa.

Kwahiyo kwa hapa wewe unatakiwa uthibitishe ya kuwa Mola hayupo, sababu utakuwa na ujuzi zaidi ya yule anaye sadikisha.

Hapa jukumu hili hulikwepi labda ulikimbie. Tutakuuliza umejuaje kama Mola hayupo, sababu hatutegemei tu ukanishe pasi na kuwa na hoja na ubainifu.

Hili wakana mungu wote huwa mnalikimbia na huthibitisha ya kuwa mna uwezo mdogo sana wa kufikiri na kuyang'amua mambo.

Kwahiyo thibitisha kama kikombe hakipo.
 
Muelezee huyu na utuambie kwanini aitwe mungu au anaitwa mungu.

Kingine naombeni wakana mungu wote mniambie imekuwaje tukawepo na mtuambie kwa ushahidi usio na shaka kabisa uwepo na usiku na mchana na jua kuzama magharibi na kuchomoza mashariki ni jambo la bahati mbaya au ? Yaani kwa ufupi tu hakika ya ulimwengu na nidhamu yake ikoje ikoje ?
 
Nikiangalia namna mfumo wa Jua na sayari zote zinavyozunguka bila kufanya makosa, mfumo ambao hauna maintenance na service kwa mabillion ya miaka - naamini kuna uwepo wa Mungu.

NASA wenyewe wamegundua almost 3% tu ya mambo yaliyoko angani so far - na wanaamini uwepo wa Mungu - wewe ni nani ?

Juzi nimemsikiliza DR. Mmoja wa NASA akisema wanajitahidi sana kuhakikisha je ni sisi tu wanadamu wa kwenye sayari ya EARTH ndiyo tupo ama kuna wengine ila hatuwajui?
 
Kijana kila siku huwa nakwambia kadhia ya kumjadili Mola ishakushinda na hutawahi kuja kuwa na hoja.

Kila siku unarudia yale yale, maswali hujibu hapa unakuja kujifaragua kwamba tangu uanze kujadili hili ni 5% tu umetumia. Kwanini unaandika uongo ? Mara ngapi najadiliana na wewe unakimbia maswali.

Umeandika suala la dhana ambazo hujawahi kuziongelea hizo siyo hujawahi kuziongelea Bali hazi jibu hoja katika kadhia hii.

Uwepo wa Mola ni uhalisia, ndiyo maana mpaka unakufa hutaweza walau kuharibu tu kukana kutokuwepo kwa Mola.

Nilishakwambia siyo kila unachokiona kina uta (contradiction) basi kina uta kweli, utata mara nyingi husababishwa na ujinga wa Mtu husika. Mfano wako ni wewe kuwa mjinga na usiye tumia akili unaona utata ila kiuhalisia hakuna utata.

Mfano nikikuuliza swali, tuthibitishie ya kuwa Mola hayupo na kwamba hii ni dhana. Dhana tamko hili Lina maana zaidi ya Moja Kuna wakati humaanisha hakika ya jambo baada ya ithibati na maana nyingine ni wazo tu. Sasa tujadili kwa maana hii ya pili. Thibitisha ya kuwa Mola kuwepi kwake ni dhana. Kisha utuambie dhana hii ilianzishwa na nani na lini.

Kuwepo kwa mabaya kunathibitisha juu ya uwepo wa Mola mwenye uwezo wote ndiyo maana akaruhusu mabaya yawepo. Sasa unapo mfasili Mola kwa upande mmoja huo ni uchachefu wa akili na Mola hufanya kila jambo kwa hekima.
Kama asili ya Mungu ni Upendo kwa nini tena aruhusu mabaya yawepo? Maandiko ya kidini yanadai Mungu asili yake ni mwenye upendo, huruma, mwingiii wa Rehema...iweje tena aruhusu ubaya na uovu u exist duniani? Huo upendo wake na huruma viko wapi?

Binafsi nasema hivi: Kama Mungu ame ridhia na alikubali uwepo wa uovu na ubaya duniani halafu tena awe mwema na mwenye upendo...Basi, Conclusion ni kwamba Mungu ni shetani na Shetani ni Mungu....ni sawa na kusema "Two sides of the same Coin".... Haiwezekani Mungu mwenye uwezo wa kuumba Dunia isiyo na ubaya na uovu ashindwe kufanya hivyo.

Lakini dunia ya leo ina ubaya na uovu ina maanisha kama Mungu yupo aliridhia na kukubali mwenyewe ubaya na uovu uwepo hivyo Mungu ni mwema na mbaya vile vile katika pande zote mbili...huwezi sema Mungu ana upendo na huruma afu uovu useme ni wa shetani!..Hizi nguvu za shetani nani alimpa na kwa nini Mungu alishindwa kumzuia huyo shetani ashindwe kufanya uovu kwa hiyo Mungu pia ni shetani....
 
Umejuaje kama hayupo ? Kitu ambacho hakipo unajuaje kama hakipo ? Je ni lazima kitanguliwe na kutokuwepo kwake ? Au si lazima ? Kama si lazima umejuaje Mola hayupo ?
Unajua ubaya uko wapi? Upo brainwashed toka mdogo, kwaiyo ubongo wako umeshalishwa sumu hutaweza kuchambua kiyakinifu,

Je unafahamu mwaka 1633 galileo galilei alihukumiwa kifungo cha maisha na kanisa katoliki kwa sababu alitoa fact kuwa dunia inazunguka jua, fact ambayo leo hao wakatoliki wanaikubali,

kwa iyo na wewe unless utaruhusu ubongo kufunguka na ku chambua mambo, hata uambiwe nini hutaelewa.
 
Sawa.

Tuseme napenda kukubaliana na wewe. Mimi pia kimsingi ningependa sana Mungu awepo. Ulimwengu ambao una Mungu ungenipunguzia matatizo mengi sana, hivyo ningefurahi sana kujua kwamba fikra zangu kwamba Mungu hayupo zina makosa, na kiukweli Mungu yupo.

ila nina tabia ya kuhakiki mambo kabla ya kuyakubali.

Hivyo, sina tatizo kukukubalia, ila nataka kuhakikisha mambo tu kabla sijakubali.

Unajuaje uwezo huo upo kweli, na si kitu ulichokifikiria tu mawazoni kwako wewe na watu mnaoamini uwepo wa Mungu, aghalabu kwa kurithishana kwenye hadithi, mapokeo, vitabu, uvivu wa kufikiri unaofanya kutojua jibu kufanywe kuwa ni kujua jibu, kuwa jibu la kisichojulikana ni Mungu huyo, wakati kiukweli uwezo huo haupo na hata huyo Mungu hayupo?
Najua kupitia vitu vya asili alivyoumba. Uwezo huo bado haujawahi kufanywa na mwingine,huo ndio upekee wake
 
Najua kupitia vitu vya asili alivyoumba. Uwezo huo bado haujawahi kufanywa na mwingine,huo ndio upekee wake
Unazunguka palepale.

Hili dai la "alivyoumba" unathibitishaje kuwa ni la kweli?

Unathibitisha vipi hivyo vitu unavyoviita vya asili vimeumbwa na Mungu kweli na kwamba dhana hiyo si hadithi tu uliyorithishwa na watu na wewe ukaikubali bila uthibitisho?
 
Kama asili ya Mungu ni Upendo kwa nini tena aruhusu mabaya yawepo?
Kwanza nani amekwambia asili ya Mungu ni upendo ? Haya mambo mlitakiwa myasome na myajue kwanza Kisha myakanushe.

Mola ukisema au ukimnasibisha na asili, maana yake ana chanzo wakati hii si sifa yake. Yes ni wa mwanzo ambaye hakuna Cha mwanzo kabla yake.

Mola wetu ana upendo kamili na ghadhabu Bali ni mkali kamili.

Kuwepo kwa mabaya ni katika matakwa yake na hekima zake.
 
Back
Top Bottom