Natafuta Ajira
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 12,272
- 33,912
Iyo nguvu ina ufahamu na mipango yoyote juu ya matendo na hatma yetu?Mungu ni ile nguvu ya uhai iliyopo ndani yetu na kwenye kila maumbile .
Iyo nguvu ina ufahamu na mipango yoyote juu ya matendo na hatma yetu?Mungu ni ile nguvu ya uhai iliyopo ndani yetu na kwenye kila maumbile .
Kutoamini kuhusu uwepo wa Mungu nayo ni IMANI.Dini zilikuwepo tangu enzi na enzi, jamii za wanaadamu zimekuwa zikiabudu vile wanavyoviita Mungu kwa miaka mingi sana hili halina ubishi.
Uwepo wake miaka mingi haina maana ni sahihi kuwepo wake maana hata uongo usipodhihirika huonekana ukweli miaka yote mpaka ukweli utakapofahamika.
Ila kuna sehemu ya watu kwenye jamii wamekuwa wakitilia mashaka na kukosoa wazo lenyewe la kuwepo kwa huyo anaeitwa Mungu. Wanaoamini (imani yoyote tu ‘as long as’ wanamuabudu wanachokiita Mungu) wanasistiza kuwa yupo na uwezo wake ni Mkuu sana.
Hoja za waumini nazifahamu baadhi, ila hoja za Atheist sijazielewa.
Ningependa kuwaelewa zaidi Atheists, Karibuni hapa Atheist walau mthibitishe (kama mtaweza) kuwa huyo wa kuitwa Mungu hayupo.
Lakini kwanza ni lazima tufafanue nini maana ya MUNGU, kwa maana kukurupuka kujibu swali ilhali hatujui maana ya dhana ya msingi wa swali itakuwa ni uhayewani wa kiwango cha juu sana.
Karibuni sana!
View attachment 2355249
ukishasema nguvu tayari kila kitu kimejitosheleza tayari uwezo na intelegensia ya hali ya juu ipo ndni ya nguvuIyo nguvu ina ufahamu na mipango yoyote juu ya matendo na hatma yetu?
Mkuu tulia wacha pupa, soma uzi taratiibu, uelewe kisha njoo ‘u-edit’ ulipoandika hapa.Siku akili zako zitakapokurudia ili utambue uwepo wa Mungu basi itakuwa too let sana kwako!
Unaposema Mungu unamaanisha nini?Dini zilikuwepo tangu enzi na enzi, jamii za wanaadamu zimekuwa zikiabudu vile wanavyoviita Mungu kwa miaka mingi sana hili halina ubishi.
Uwepo wake miaka mingi haina maana ni sahihi kuwepo wake maana hata uongo usipodhihirika huonekana ukweli miaka yote mpaka ukweli utakapofahamika.
Ila kuna sehemu ya watu kwenye jamii wamekuwa wakitilia mashaka na kukosoa wazo lenyewe la kuwepo kwa huyo anaeitwa Mungu. Wanaoamini (imani yoyote tu ‘as long as’ wanamuabudu wanachokiita Mungu) wanasistiza kuwa yupo na uwezo wake ni Mkuu sana.
Hoja za waumini nazifahamu baadhi, ila hoja za Atheist sijazielewa.
Ningependa kuwaelewa zaidi Atheists, Karibuni hapa Atheist walau mthibitishe (kama mtaweza) kuwa huyo wa kuitwa Mungu hayupo.
Lakini kwanza ni lazima tufafanue nini maana ya MUNGU, kwa maana kukurupuka kujibu swali ilhali hatujui maana ya dhana ya msingi wa swali itakuwa ni uhayewani wa kiwango cha juu sana.
Karibuni sana!
View attachment 2355249
Vizuri Mkuu, kati ya wachangiaji wote wewe umenielewa nilipolenga.Unaposema Mungu unamaanisha nini?
Maana hata Beyonce mke wa Jay-Z kuna watu wanamkubali kama Mungu wao.
Na kwa definition yao ya Mungu siwezi kuwakatalia na kusema kwamba Beyonce mke wa Jay-Z hayupo.
Mungu ni nini? Na unathibitishaje hilo jibu lako?
Mimi binafsi maongezi yangu niliyoyafanya JF miaka yote kuhusu uwepo wa Mungu hayajafikia hata 5% ya maongezi ninayoweza au ninayotaka kuyafanya.Vizuri Mkuu, kati ya wachangiaji wote wewe umenielewa nilipolenga.
Binafsi lengo la kuandika uzi huu ni kufungua fikra zangu na za wasomaji, khabari za kukariri uwepo wa Mungu naona inatosha, ningependa kuelewa ili kama nitachagua kuamini niamini kwa sababu naelewa na si kuamini sababu sina chaguo.
Mkuu ninyi atheists mnaposema Mungu hayupo huwa mna maana ya Mungu gani?
Ama nini maana ya Mungu kwa mujibu wa atheists (kama ipo).
Yes, nilikua nikikusoma na nikaona unapinga uwepo wa Mungu kwa sifa mahususi ulizozitaja, binafsi nilikuelewa sana.Mimi binafsi maongezi yangu niliyoyafanya JF miaka yote kuhusu uwepo wa Mungu hayajafikia hata 5% ya maongezi ninayoweza au ninayotaka kuyafanya.
Kwa sababu watu wengi wanajadili dhana hii kwa upeo finyu wa dini zao. Na inakuwa vigumu kuendeleza mazungumzo ngazi ya tatu wakati hata ya kwanza hatujamaliza. Inakuwa sawa kutaka kujadiliana hesabu za Poincare's Conjecture level ya Grigori Perelman na mtu ambaye hajui kujumlisha na kutoa.
Hivyo hatujafikia kuzungumzia hata dhana kama pantheism, deism, na nyingine nyingi.
Mara nyingi watu huanzia na Mungu anayetajwa kwenye dini kubwa. Maana huyo ndiye anayetajwa sana.
Mfano, mimi mara nyingi ninapopinga uwepo wa Mungu, humtambulisha kwa sifa kama kusema "Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote".
Huyu ndiye Mungu anayetajwa kwenye misahafu ya Uyahudi, Ukristo, Uislamu na mingine mingi tu.
Mungu huyu ni dhana tu, hayupo kwenye uhalisia.
Dhana ya kuwepo Mungu huyu inapingana na ulimwengu unaoruhusu mabaya. Ama una ulimwengu unaoruhusu mabaya na Mungu huyu hayupo, ama Mungu huyu yupo na ulimwengu unaoruhusu mabaya haupo.
Ulimwengu unaoruhusu mabaya upo.
Hivyo, Mungu huyo hayupo.
This is basic logical consistency.
Mungu huyo kuwepo ni contradiction kama kuwepo kwa pembetatu ambayo hapo hapo ni duara katika planes za Euclidian geometry.
Ni contradiction kama 10 kuwa square root ya 2 katika base 2 mathematics.
Mfano wa kikombe na dhana ya Mungu ni tofauti sana,Unasema kikombe kipo na Mimi ninasema hakipo halafu unanitaka Mimi ninaesema hakuna kikombe ndio nithibitishe, badala ya wewe unaesema kipo.
Wewe unaesema mungu yupo thibitisha na sio athibitishe anaesema mungu Hayupo.
Mkuu karibu sana, ila unaonaje tukaanza na kufafanua dhana ya Mungu yenyewe?Jukumu la kutoa uthibitisho lipo kwa mtoa madai sio mpinga mdai. Mimi nimekwambia nimesoma harvard wewe umeangalia kwenye CV yangu ujaona popote ambapo panaonesha nimesoma harvard hapo ni mimi ndio nitapaswa kukuthibitishia nimesoma harvard kwa kukuonesha cheti nitaoneka wa ajabu nikitaka wewe ndo unithibitishie sijasoma harvard.
Ambao hawaamini uwepo wa Mungu hawakuja tu madai hayo, waliikuta iyo nadharia ya uwepo wa Mungu kwenye jamii walizoishi walifundishwa baada ya kuchanganya za kuambiwa na zao ndio wakaja na hitimisho hizi habari sio kweli. Kwaiyo unaona hapo madai yalianza kutolewa wao ndio wakaja kuyapinga na moja ya vigezo vyao vya kupinga ni kukosekana kwa uthibitisho juu ya uwepo wa Mungu., waumini wengi wanapoombwa uthibitisho wa uwepo wa Mungu wanachukulia ufinyu wao wa maarifa kama uthibitisho wa uwepo wa Mungu kitu ambcho sio sahihi, ndipo wanakuja na maswali kama ulimwengu ulitokea wapi, pumzi unayovuta imetokea wapi n.k lazima tuelewe kwamba ulimwengu ulkwepo miaka mingi sana kama yetu binadamu kwaiyo hatuwezi kujua kila kitu kirahisi rahisi tu kuna mambo mengi hatuyajui kutokana na ugeni wetu kwenye huu ulimwengu na inawezekana kabisa hakuna kizazi kitakachokuja kuwa na majibu yote kuhusu ulimwengu kwaiyo pale ambapo maarifa yako yamefika mwisho ni vyema ukakiri haujui ukitaka kumweka Mungu katika iyo point ambayo maarifa yako yamefika mwisho basi onesha ushaidi wa kimahusiano kati ya Mungu na suala husika... kwa msingi huo mimi nafikiri wanaoamini uwepo wa Mungu ndio wanapaswa kutoa uthibitisho wa uwepo wake
MUNGU ni suala la kiimani na huwezi thibitisha suala la kiimani nje ya imani. Tunaamini MUNGU yupo sababu hakuna mbadala wa concept isiyo na shaka ya uwepo wa ulimwengu.
Sawa Mkuu, lakini Atheists husema Mungu ni nini?Hii imani ni zao la kutokewepo kwa facts zisizo na shaka za sababu za uwepo wetu na vyote tuvionavyo. Ukisema tuachane na imani ya uwepo wa MUNGU njoo na hitimisho la yote tuliyoyakuta duniani. Siku tukipata jibu kuwa ss ni nn na ulimwengu ni nn basi hiyo imani itafutika. Kwa sasa yoyote apingaye uwepo wa MUNGU bila ushahidi timilifu wa kutokuwepo kwake ni mfuasi wa adui wa MUNGU aitwaye shetani, ibilisi. Hii kutaka kubatilisha uwepo wa MUNGU kwa njia ya kushindwa kuthibitisha uwepo wake nje ya imani haipo sawa sababu imani ya uwepo wake ni matokeo ya uwepo wetu pasipo kuwa na ushahidi usio na shaka wa sababu za uwepo. Hii sababu ya uwepo wetu tusiyoweza kuithibitisha ndiyo iliyozaa imani ya uwepo wa MUNGU.
Soksi na dhana ya Mungu kama ielezwavyo na Waumini haviendani.Mimi sina Soksi....Njoo uthibitishe kuwa sina Soksi
Imani, imani imani.Mungu Hayupo, Mungu Yupo
N.b: Imani
Hii dhana ya Mungu ni nini? Atheists wao husema ni nini?Wanadamu na sayansi yetu ndogo hapa duniani ya Technology kama ya mtu aliyeanzishaa internet ni ndogo sana, ila sisi tumeona kubwa na kwavile tuliumbwa kwa mfano wa Mungu roho zetu basi tunajikuta wajuaji kama Shetani na kujiona miungu watu.
Kosa lile lile walilolifanya Israel na mataifa Mengine kuabudu miungu..
Na mwisho wa Dhambi hiyo ni mauti.
Athiest wanajikutaga wanajua kinoma na kutegemea akili zako ndio Mwanzo na Mwisho wa hekima hapa duniani hawajui wala kuamini Yupo mwenye hekima zaidi Yetu na Akili zake hazichunguziki.
Siwezi kuvielezea sana hivyo vitu kwa sababu sijavipa nafasi katika maisha yangu .Imani, imani imani.
Sina shaka imani hiyo hukuzwa na sababu fulani fulani, hiyo ndiyo ‘focus’ yetu.
Kipi kinakufanya UAMINI YUPO?
au
Kipi kinakufanya UAMINI HAYUPO?
Ila kabla hatujafika huko tuanze na maana ya dhana yenyewe ya MUNGU.