Agnamkwili
New Member
- Jun 22, 2022
- 4
- 10
Kutokana na Biblia, "Mwz: 1:27 ....... Mungu alimwumba mwanamume na mwanamke aliwaumba". Kwa maana aliwafinyanga.
Vilevile "Mwz: 2:21, Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito nae akalala, kisha akatwaa ubavu wake mmoja akafunika nyama mahali pake. 22 na ule ubavu alioutoa kwa Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke akamleta kwa Adamu. 23 Adamu akasema SASA huyu ni mifupa katika mifupa yangu na nyama katika nyama yangu basi ataitwa mwanamke kwasababu ametwaliwa katika mwanamume".
Hapa inaonekana wazi kuwa uumbaji wa wanawake hawa 2 ulikuwa tofauti. Wakwanza ambaye anajulika kwa jina la Lilith (kwa mujibu wa waandishi mbalimbali kutoka kwenye Google) huyu aliumbwa kwa kufinyangwa sawa na Adamu.
Hivyo hakumtii Adamu kwakuwa walikuwa sawa hakuona sababu ya kuwa chini ya Adamu.
Usawa unaodaiwa na wanawake siku hizi ulianzia hapo. Baada ya kuto kuelewana Lilith liondoka na kumuacha Adamu. Alikwenda kuolewa na Malaika Mkuu aliyeasi Mbinguni na kutupwa Duniani. Hivyo walizaa watoto (uzao wa uasi) Majitu.
Kipindi hicho Adamu alibaki peke yake Bustanini. Ndipo Mungu hakuona vyema akamtengenezea mwanamke kutoka katika ubavu wake.
Pia tunaona neno alilolitamka Adamu baada ya kupewa mwanamke "SASA" linaonyesha wazi kuwa kulikuwa na mwanamke wakwanza ambaye hakuridhika nae ila huyu wa SASA ndiye aliridhika nae.
Baadae ndipo walipo danganywa na Ibilisi (Nyoka) wakafukuzwa Bustanini. Wakaenda kuanzisha familia ambapo walimzaa Kaini na Abili na wengine Kaini alimuua Abili baada sadaka yake kukataliwa na Bwana Mungu. Nae Mungu alimlaani akatoka katika familia ya Adamu.
Ndiyo baadae alienda kuoa. Alimuoa binti kutoka kwa mwanamke Lilith na Ibilisi, Uzao wao ni wa uasi maana wao walimuasi Mungu. Uzao huu ni mwingi na umembatana na Mambo kama mauaji, ngono, wizi, choyo, ubinafsi kutawaliwa na fedha badala ya kuitawala fedha, dhuluma, uonevu n.k uzao huu ni zao wa laana, ambao ni wengi hata sasa.
Na uzao wa Adamu na Hawa ni uzao wenye Baraka za Mungu. Umejaa upendo, kuheshimiana, uvumilivu, kuchukuliana, staha yaani mambo yote mema yaliambatana na uzo huu wa Adamu na Hawa, ambao ni wachache hata sasa.
Sasa hebu tujingalie sisi tupo kwenye uzao gani wa Lilith na Ibilisi au Adamu na Hawa? Maana DNA zao tunzo na zitaendelea vizazi kwa vizazi.