Kuna uwezekano wa Mungu kuwa na nguvu sawa kitu alichokiumba (shetani)?

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
2,556
2,995
Ramadhani njema wanajamvi!

leo naleta hoja lakini hoja yangu ni ya kiimani nataka kujua kupata kujifunza kutokana na fikra zangu hazinishawishi pia,nifahamike mimi imani yangu ni muislamu hivyo siyo kama nakebehi kuhusu hoja yangu na ikiwa nimekosea mungu anisamehe.

Qur'an na bibilia vinamtambua ibilisi ni kama malaika aliyeasi (rejea surat baqarah pale aibilisi alipoambiwa kuwa amsujudie mwanaadamu hakika yeye ni kiumbe bora,ibilisi aliasi na mungu akamlaani,lakini pia hata upande wa bible katika kurasa na sura ya mwanzo mungu ameongelea uumbaji wa dunia pamoja na mwanadamu na akampa ibilisi sura ya nyoka ambae amemdanganya Eva na mungu alipogundua hilo baadae akawalaani wote akamwambia hawa atazaa kwa uchungu,ibilisi atatembelea tumbo lake na adamu atatafuta kwa shida.

Hoja yangu ipo hapa je,inawezekana mungu akaumba kiumbe kinachomzidi nguvu?rejea maandiko ya ujenzi wa mnara wa babeli mungu aliposhuka chini na kuwasikia watu wake wakisemezana kwamba wajenge mnara mkubwa ili kuacha historia ya vizazi ndipo mungu akaona kuwa hawa wanadamu wanaongelea lugha moja na utaifa mmoja akituacha hivyo huenda tukafanya makubwa zaidi,na tukapata kutafuta ule mti mkuu wa uzima akaogopa na kutufautisha lugha pamoja kututawanya.

Swali ni kweli mungu hakujua anachokiumba kina nguvu kiasi gani?au alijua mwanadamu ataishi atakavyo yeye lakini je hakujua uwezo wa sauti na akili?

Swali fikirishi kuna nguvu ya wema ambayo ni mungu na nguvu ya ubaya ni shetani ni kwamba unapotenda wema basi imetekeleza maandiko ila ubaya umekengeuka maamrisho inakuwaje?kuwe na nguvu mbili wakati mmoja (wema na ubaya).

Uhalisia upo hivi mimi mfanyabiashara mdogo siwezi kulinganishwa au kujilinganisha na mfanyabiashara mkubwa kama bakhresa inakuwa upande wa hizi nguvu mbili zinashabiana?

NAWASILISHA
 
NDIO KWA SABABU YEYE NI MUNGU MWENYE HAKI.

YEYE ANA MAAMUZI YA KI MUNGU SIO YA KIBINADAM KAMA WEWE UNAVYO FIKIRI HAPA.

KWA MAWAZO YAKO HAYA INAMAANA WEWE AMBAE ANGEKUWA ANAKOSEA UNAMUUA MDA HUO HUO!! MUNGU NI MUNGU TU YEYE NI MUNGU ATENDAYE KWA HAKI
 
sawa lakini vitabu vya dini vinaonesha mungu mda mwengine alikasirishwa na matendo yetu na mpk kutaka kutufuta katika uso wa dunia rejelea historia na vizazi vya NOAH/NUH.
NI KWELI LAKINI KWA KUWA SIO MWINGI WA HASIRA NA AMEJAA REHMA NDIO MAANA AKATUNUSURU, YEYE AKIAMUA KUANGAMIZA DUNIA YOTE NI SUALA LA SEKUNDE TU, VIVYO HIVYO KWA SHETANI
 
HOW IS THIS POSSIBLE?
Yakobo 1:13-16

"Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.

Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.

Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.

Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike."
 
Yakobo 1:13-16

"Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.

Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.

Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.

Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike."
KWA HIYO MAANDIKO YANAKINZANA

MUNGU KUMJARIBU IBRAHIMU , AYUBU, YESU SIKU 40 JANGWANI? KUPIMWA IMANI
 
Shetani sio Kiumbe ni sifa!
Hivyo kuna mashetani wa Kijini na mashetani wa Kibinadamu (kwa mujibu wa Dini)
Nakumbuka Yesu alipotembelewa na MERRY MAGDALENA ambae alikuwa amemiliki pepo 7 mwilini mwake na alitengwa na jamii yake ila alipofika kwa yesu ndipo aliombewa na hao wadudu wakamtoka hivyo mashetani yapo ndani yetu ndiyo maana zamani ilikuwa kazi yao kuwatia watu uchizi,miaka ya juzi wakawa wanawapa watu magojwa ila now days wanakuja ndotoni ndiyo maana manabii wamekuwa wengi mno kumbe hawajui kuwa wao ni waganga kama waganga wengine.

tukitumia hoja za kisayansi ndiyo tunaweza kutengeneza parametors za kumuindicate shetani kitabia,ila kidini shetani ni kiumbe.
 
Kwanza kuna vitu inaonekana umevielewa vibaya.
Moja ni asili ya Ibilisi, Ibilisi sio malaika alie asi, Sifa ya malaika hawezi kuasi kwa sababu hawana uhiari wa kufanya mambo(willing) bali hufanya kadri wanavyoelekezwa na Mungu.
Viumbe wenye sifa ya uhiari ni binadamu na majini, Ibilisi ni katika majini. Ningekueleza asili yake kwa undani ila time is very limited kwa sasa.
Unaposema shetani ni sifa na sio kiumbe kwa maana kila chenye kuasi kati ya mwanadamu au majini hupewa sifa hii ya shetani japokuwa wengi umkusudia Ibilisi kama shetani.
Kuhusu Mungu kuzidiwa na kiumbe alichokiumba nadhani umeshajijibu kwenye maelezo yako kwamba Mungu akawa wabadilishia lugha watu wa Babeli hii inaonyesha Mungu ana nguvu kuwazidi ndio maana akaweza kuwabadilishia lugha.
Any questions so far.?
 
Mtoto anayebalehe akianza kurudi usiku kila mtu akiwa amelala huwa anaona hakuna wa kumfanya kitu, hata mzee wake huwa anaona kama anammudu. Sasa mzee anaweza mchukua akamweka ndani polisi siku mbili tatu ili ajifunze na kumkumbusha kuwa hayupo in control kama anavyodhani.

Kiimani Sisi akiwemo Shetani ni viumbe vya MUNGU. Nadhani kuna muda MUNGU anatukumbusha tu kuwa hatupo in control kama tunavyodhani.
 
Back
Top Bottom