Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Futa machozi anza maisha upya bila huyo mume, mwache alee mimba na kulea mtoto wa mdogo wako.
Hutakuwa na raha kuona mdogo wako kazaa na mume, na afadhali hamjapata mtoto nae.
* ila maamuzi ni yako. Binafsi nisingeweza kuvumilia situation kama hiyo.
 
Imeandikwa samehe saba mara sabini, sisi wanaume ni mbwa.
Hapana si kwa uzinzi mungu ameruhusu taraka kama pana zinaa hata iwe ndoa ya kikristo pia wanaume sisi ni kichwa cha nyumba sio mbwa
 
Futa machozi anza maisha upya bila huyo mume, mwache alee mimba na kulea mtoto wa mdogo wako.
Hutakuwa na raha kuona mdogo wako kazaa na mume, na afadhali hamjapata mtoto nae.
* ila maamuzi ni yako. Binafsi nisingeweza kuvumilia situation kama hiyo.
alishafariki huyo mdogo wake soma post ya leo ,alifariki kwenye ajali akienda kwenye harusi yake.
 
JF imebadilika au kuna moderator ameingili kati huu uzi? Maana post ya 1 hadi 20 ni madini matupu hamna dhihaka kabisa! Nona narudi JF 2010.
 
Pole sana kwa kunyanyasika na tukio hilo mungu akutie nguvu uvumilie tu ila ndoa imevunjika haipo labda kama mtafunga upya imeandikwa ndoa itatenganishwa kwa kifo tu kama mtu akiingilia ndoa ya mtu basi yeye ndio kifo.nafsi itakapo tulia utampata mwenye nia ya ndoa hiyo imekufa ukiilazimisha unasubili sumu utese wazazi wanao taraji matunda ya elimu yako achana nayo kabisa mungu atakupa kwa wakati wake huyo hakuwa wako ulilazimisha ndio maana mmetetenganishwa
 
Habari za asubuhi wanajamvi,

Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.

Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.

Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.

Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.

Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.

Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.

Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.

Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.

Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.

Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.

Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.

Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..

Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.

Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.

Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.

Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..

Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.

Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.

Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.

Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?

Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.

Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.

Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.

Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.

Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..

Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.

Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,

Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.

Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..

Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.

Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.

Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.

Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..

Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.

Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.

Wameondoka na sijui walipo kwenda.

Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.

Najiuliza heshima yangu iko wapi?

Jamii inanionaje?

Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?

Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.

Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.

Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.

Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.
Pole dada, ndoa ni furaha, amani, upendo, kuendelea kuishi nae hivi vyote utayari wako wa kusamehe na mume kuonyesha toba ya kumaanisha, nikiwa na maana kuwa akuombe radhi wewe, wazazi na Mungu ambae amemkosea, nawe utahitaji ushauri wa kiroho kuliweka hili sawa, omba amani ya Mungu ndani yako, na Mungu akusemeshe nini chakufanya,narudia kusema mume akionyesha toba ya kweli toka rohoni! Msamehe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndoa ya kikristu huwa haivunjwi hata kwa zinaa ww endelea na mume wako akina Abrahamu walichepuka sembuse mume wako? Simtetei mumeo pengine makosa unaweza ukawa unachangia nyie wasomi mnakuwa bookish sana na kusahau majukumu ya msingi pili epuka kuleta ndugu zako wa kike kwako wengine wanaona wivu kwako wanaamua wakuibie tu ndugu lawama jamani mume anaweza kuwa alitegeka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom