Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Ahsante kwa kuongezea maelezo mujarab mkuu, majaribu na vishawishi vipo na vitaendelea kuwepo. Ukishajua umeingia kwenye taasisi ya ndoa ni jukumu letu kama wanaume kuamua kukataa dhambi na mbaya zaidi kuwaumiza wake zetu kana kwamba tuna haki ya kuchepuka.

Mungu atusaidie katika hili, tunaishi kwenye kipindi ambacho watu wanaona kawaida ndoa kuvunjika, kutokua waaminifu kwa wenzi wao na kutokusimama kwenye nafasi zao. Si laumu lakini nimesikitishwa na baadhi ya michango inayotaka kuhalalisha uchepukaji wa wanaume kama jambo LA kawaida kwenye jamii.

Ubarikiwe mkuu.
Aaah Mungu aendelee kukutetea mpendwa
 
Kumpa nafasi mdogo wako wa kumtendea mambo ya kimahaba mumeo huku ukiwa umebweteka kama yeye ndo kaolewa huwa mnachangia kwa kiasi kikubwa. Chukua nafasi ya mke na wajibika kama mke. Mtalia lia sana kwa wadogo zenu na mahausi geli kupigwa ukuni.
 
Aah uzuri mimi mwenyewe ni mswahili wa unyakyusani, si Nakubaliana na hubby jamani[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Hahah...hapo sawa na wakijifanya wanaongea sana,
wewe unafungulia taarabu sauti 100
huku unapaka zako hina[emoji23]
 
Nyie cheating inaumiza jamani. Na ni kazi sana mke kuanza upya after knowing kwamba mumewe anamcheat (na hapo ni mume kaomba msamaha). Kila mtu anaweza kutenda dhambi, lakini kufanya dhambi afu unaijustify tu, yani easy daaah. Anyway waache tu wafikiri bado tupo enzi za uwimbombo na ulindi
Umeona eee!!
 
Habari za asubuhi wanajamvi,

Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.

Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.

Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.

Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.

Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.

Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.

Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.

Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.

Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.

Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.

Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.

Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..

Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.

Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.

Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.

Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..

Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.

Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.

Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.

Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?

Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.

Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.

Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.

Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.

Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..

Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.

Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,

Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.

Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..

Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.

Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.

Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.

Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..

Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.

Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.

Wameondoka na sijui walipo kwenda.

Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.

Najiuliza heshima yangu iko wapi?

Jamii inanionaje?

Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?

Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.

Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.

Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.

Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.
Kwanza nikupongeze kwa hekima kubwa uliyonayo.Pili kwa maoni yangu hiyo ndoa imeshaingia balaa.Sioni mantiki ya kuendelea kuishi na mzinifu,tena hatua ya kuzini na ndugu yako.Mwenye kuzini na ndugu wa mwanandoa mwenziwe,huyo ni mzinzi wa degree ya juu kabisa.Sisi ni washauri tu,uamuzi ni wako.
 
Japo nimechelewa kujibu lakini kiukweli, kuna hali ambayo haiwezi kuvumilika. Wapo walotoa maoni yao kuwa wewe ndo una makosa kwa kutomzalia mumeo hadi umalize masomo yako, lakini hili c Kosa, kama angehitaji mtoto bas acngemwambia shemeji yake atoe mimba hiyo.

Wengne pia wamesema samehe 7 Mara 70, ni vzuri kufanya hivyo. Lakini hata Yesu alisema mume asimpe mke talaka ila kwa habari ya uasherati. Bila shaka mumeo amevunja ahadi ya ndoa. Kudai talaka ni haki yako halali hata Biblia imeruhusu kwa Kosa kama hilo.

Ni kweli waweza kuhic n rahc kusamehe lakini hata ningekua mm, nisingeishi na mwanaume yule.
Weka moyo wako huru, ufanye kile kitakachokupa Furaha. Yawezekana huyo hakuwa ubavu wako pengine wako halali yupo..
 
Pole sana dada Leah 2,

ushauri wangu, kama yeye ameshavunja masharti nawe hauna bud ya kuendelea nae, kaa pebeni,. Endelea kumuomba Mungu akusaidie upate mme mwenye busara na anae jitambua.,
hapana, msamehe na mdogo wako arudi kwa wazazi wake.
 
una haki ya kukosewa mwanaume hakataliwag kitu shida yenu nyie mlosoma mnajifanya mnapangia wanaume muda wa kuwapa watoto jaribu kumsamehe coz chanzo ni ww mwenyewe
 
Japo nimechelewa kujibu lakini kiukweli, kuna hali ambayo haiwezi kuvumilika. Wapo walotoa maoni yao kuwa wewe ndo una makosa kwa kutomzalia mumeo hadi umalize masomo yako, lakini hili c Kosa, kama angehitaji mtoto bas acngemwambia shemeji yake atoe mimba hiyo.

Wengne pia wamesema samehe 7 Mara 70, ni vzuri kufanya hivyo. Lakini hata Yesu alisema mume asimpe mke talaka ila kwa habari ya uasherati. Bila shaka mumeo amevunja ahadi ya ndoa. Kudai talaka ni haki yako halali hata Biblia imeruhusu kwa Kosa kama hilo.

Ni kweli waweza kuhic n rahc kusamehe lakini hata ningekua mm, nisingeishi na mwanaume yule.
Weka moyo wako huru, ufanye kile kitakachokupa Furaha. Yawezekana huyo hakuwa ubavu wako pengine wako halali yupo..
Asante kwa ushauri na kujaribu kuvaa uhusika.
 
wabongo baana mnatakaga ushaur akat mshaamua yenu kichwan
 
Yani wanaume mnanisikitishaga mnavyojuaga kujustify uzinzi. Hivi mfano mnaishi ndani na mdogo wako wa kike au binti yako, na yeye ungelala naye kwa sababu tu mmepewa huo uhuru? Mnatafutaga tu kanafasi kajitokeze Mfanye uzinzi vizuri. Huwezi kuwaheshimu wadogo wa mke wako kama wadogo zako wa tumbo moja? Mbona hamna aibu wala heshima kwa wake zenu? Yani akija mdada ambaye si tumbo moja na wewe nyumbani kwako, lazima ulale naye au?

Mbona kuna wadada wamekuzwa na mashemeji zao hadi wanaolewa na walitreatiwa kama watoto wa nyumba hiyo?. Haya mambo ya Kuendekeza mkojo ndo unakuta mtu anatembea hadi na watoto wake wa kuwazaa. Mnazaa lakini, I hope mnayoyafanya kwa mabinti za watu mnaomba watoto wenu waje kufanyiwa the same. Maisha mzunguko, kesho hujui watoto wako watakuwa mikononi mwa nani. Mnaishi maisha gani kama majogoo, Kila mtetea unaubakua tu!!. Msitembelewe na mgeni wa kike nyumbani kwenu, zipu zinakatika, wake zenu wasitembelewe wala kuishi na ndugu zao wa kike!!!. Disgusting
Wamelogwa hao na aliyewaloga ameshakufa. Yaani binafsi nimewashiba wanaume kbsa
 
Wanaume katika uhalisia wao wanafanana vitu vingi sana,si ajabu ukamuacha huyo ukaenda kwasababu ya kutoweza kua mwenyewe ukaangukia kwa mwingine anaye shabihina Na huyo au zaidi kimatendo.
Ushauri wangu,Kama bado nichanga mshauri mdogowako muitoe,hii nikatika kuhakikisha ile existence ya doa haiwi ya kudumu.
Pili,mke afunge japo kwa week moja akiiombea ndoa yake huku akiomba hekima Na roho wa kusamehe akae pembeni yake wakati wote.
Ombasana kwa Mungu akujalie hekima ya kusamehe maana bila hivo unaweza kusamehe/ku endelea Na ndoa Na ukaishia kuwa mchepukaji maalufu.
Note:a woman without history lacks wisdom
 
Back
Top Bottom