Mume wake dada hataki kunipa mtaji

Mume wake dada hataki kunipa mtaji

Mimi ni kijana mdogo mwenye miaka 29, nimesoma diploma ya masuala ya afya, baada ya kuhitimu nilikaa sana kijijini bila ajira. Dada na mume wake wakaamua kuniita mjini nijaribu bahati yangu.

Ila huku nako hali imezidi kuwa mbaya, kazi hakuna. Cha ajabu siku hizi wamenianzishia visa, dada na mume wake wanataka na mm niwe nafanya kazi za hapa nyumbani, wakati wafanyakazi wapo. Nilivyokataa kutumikishwa, mume wake dada anataka kunirudisha kijijini. Nimemwambia kijijini siendi, labda anipe mtaji. Amekataa kata kata, na sio kwamba hela hana. Hela anazo maana kila mwisho wa wiki anapendaga kutoka yeye na dada.

Wanashindwa kujibana hata mwezi ili mimi nipate mtaji? Leo tumezozana sana, walivyo na tabia mbaya, wameanzisha haya malumbano wakati wa kula. Hapa nipo na msongo wa mawazo, pia njaa ni kali maana nimegoma kula chakula chao usiku.

Naombeni ushauri, sielewi nifanye nini.
Endelea kukaza hadi mtaji utoke au sio man... Haiwezekani amfaidi sister yako halafu akunyime kamtaji😃
 
Tatizo lako unajiona wewe bado ni Mtoto kitu ambacho siyo kweli wewe ni Mtu mzima sasa, unaishi kwa Shemeji hutaki kufanya kazi yoyote hilo nalo ni kosa huenda ndiyo maana hawataki kukusaidia maana walishakuona kuwa hujitambui, fanya mchakato utoke hapo ulipo.
 
Nimemwambia kijijini siendi, labda anipe mtaji. Amekataa kata kata, na sio kwamba hela hana. Hela anazo maana kila mwisho wa wiki anapendaga kutoka yeye na dada.
huyo ni baba yako?
ni hiv hapo huna haki uondoke urudi kwenu, hapo sio kwako,
haya mazoea ndo yanatufanya tunazidi kuwa maskini!
 
Bro miaka 29 unajiita kijana mdogo looooh mpaka hapo ushafeli badilisha fikra zako mkuuu hio ni 30 yrs bado huna dira mbaya zaidi unaishi na nyoka 🐍 huyo dada na mmeo sio ndugu zako bro kaa chonjo mkuuu 💩💩💩 halafu kwanini hukuchukua degree na muda umesonga hivyo mpaka unafikisha 29 huo muda wote ulikuwa unafanya nini 🤔🤔🤔🤔

Daaah ila bro toka hapo toka hapo bro kabangaize chochote ila usikae kutwa hapo ndani

Ohoooo
Degree siyo ya kuchukua tu
 
Huna hela nakupa ushauri mzuri tu.
Kadange uwe marioo kusanya hela kutosha fungua biashara na ujenge pangoo acha undezi wamama wanahitaji upendo Tena wale weupe
 
Mimi ni kijana mdogo mwenye miaka 29, nimesoma diploma ya masuala ya afya, baada ya kuhitimu nilikaa sana kijijini bila ajira. Dada na mume wake wakaamua kuniita mjini nijaribu bahati yangu.

Ila huku nako hali imezidi kuwa mbaya, kazi hakuna. Cha ajabu siku hizi wamenianzishia visa, dada na mume wake wanataka na mimi niwe nafanya kazi za hapa nyumbani, wakati wafanyakazi wapo. Nilivyokataa kutumikishwa, mume wake dada anataka kunirudisha kijijini. Nimemwambia kijijini siendi, labda anipe mtaji. Amekataa kata kata, na sio kwamba hela hana. Hela anazo maana kila mwisho wa wiki anapendaga kutoka yeye na dada.

Wanashindwa kujibana hata mwezi ili mimi nipate mtaji? Leo tumezozana sana, walivyo na tabia mbaya, wameanzisha haya malumbano wakati wa kula. Hapa nipo na msongo wa mawazo, pia njaa ni kali maana nimegoma kula chakula chao usiku.

Naombeni ushauri, sielewi nifanye nini.
yaani una miaka 29 na bado unajiita kijana mdogo? hizo kazi za nyumbani sisi wenzio tumeoa tuna ndoa za miaka mingi na bado tunazifanya. unaamka tu na mzuka siku hiyo unamwambia waifu leo usipike ,nitapika mimi. pia, umri huo sio wa kukaa kwa dadako, unamnyima dadako raha ya ndoa.a takuwa anajibana anashindwa hata kupiga kelele na kujiachia na bwanake kisa limtu lenye 29 years lipo hapo linawasikiliza na kuwahesabia rounds.
 
Back
Top Bottom