Mume wake dada hataki kunipa mtaji

Mume wake dada hataki kunipa mtaji

Street College

Senior Member
Joined
Jun 1, 2012
Posts
151
Reaction score
430
Mimi ni kijana mdogo mwenye miaka 29, nimesoma diploma ya masuala ya afya, baada ya kuhitimu nilikaa sana kijijini bila ajira. Dada na mume wake wakaamua kuniita mjini nijaribu bahati yangu.

Ila huku nako hali imezidi kuwa mbaya, kazi hakuna. Cha ajabu siku hizi wamenianzishia visa, dada na mume wake wanataka na mimi niwe nafanya kazi za hapa nyumbani, wakati wafanyakazi wapo. Nilivyokataa kutumikishwa, mume wake dada anataka kunirudisha kijijini. Nimemwambia kijijini siendi, labda anipe mtaji. Amekataa kata kata, na sio kwamba hela hana. Hela anazo maana kila mwisho wa wiki anapendaga kutoka yeye na dada.

Wanashindwa kujibana hata mwezi ili mimi nipate mtaji? Leo tumezozana sana, walivyo na tabia mbaya, wameanzisha haya malumbano wakati wa kula. Hapa nipo na msongo wa mawazo, pia njaa ni kali maana nimegoma kula chakula chao usiku.

Naombeni ushauri, sielewi nifanye nini.
 
Mimi ni kijana mdogo mwenye miaka 29, nimesoma diploma ya maswala ya afya, baada ya kuhitimu nilikaa sana kijijini bila ajira . Dada na mume wake wakaamua kuniita mjini nijaribu bahati yangu.

.
Bro miaka 29 unajiita kijana mdogo looooh mpaka hapo ushafeli badilisha fikra zako mkuuu hio ni 30 yrs bado huna dira mbaya zaidi unaishi na nyoka 🐍 huyo dada na mmeo sio ndugu zako bro kaa chonjo mkuuu 💩💩💩 halafu kwanini hukuchukua degree na muda umesonga hivyo mpaka unafikisha 29 huo muda wote ulikuwa unafanya nini 🤔🤔🤔🤔

Daaah ila bro toka hapo toka hapo bro kabangaize chochote ila usikae kutwa hapo ndani

Ohoooo
 
Kijana mdogo 29 yrs?
Yani upewe hifadhi, ule na unye bure alafu kazi mpaka ufosiwe kufanya na bado hutaki?
Mkuu sikutukani ila wazazi wadai mahari ya pili, dada yako anakukataa kwa sababu anaona utafanywa mke wa pili.
Toka hapo katafute na ule kwa jasho lako 😬

Mtegemea cha nduguye hufa maskini.
 
Huu ndo ukweli mchungu huyu dogo hayupo serious aseee 🤔
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Wewe wa kutiwa bakora kabisa. Shemeji yako siyo baba yako wala mama yako, sio wajibu wake kukulea na kukupa mtaji, hata hapo unavyoishi ni hisani tu.

BTW najua hii ni chai, miaka 29 hauwezi kuwa na akili za kitoto kiasi hicho 😂.
 
Bro miaka 29 unajiita kijana mdogo looooh mpaka hapo ushafeli badilisha fikra zako mkuuu hio ni 30 yrs bado huna dira mbaya zaidi unaishi na nyoka 🐍 huyo dada na mmeo sio ndugu zako bro kaa chonjo mkuuu 💩💩💩 alafu kwann hukuchukua degree na muda umesonga hivyo mpaka unafikisha 29 huo muda wote ulikuwa unafanya nn 🤔🤔🤔🤔

Daaah ila bro toka hapo toka hapo bro kabangaize chochote ila usikae kutwa hapo ndani

Ohoooo
Acha aendelee kukaa hapo hapo. Mambo yatakaa sawa tu😅😅
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Wewe wa kutiwa bakora kabisa. Shemeji yako siyo baba yako wala mama yako, sio wajibu wake kukulea na kukupa mtaji, hata hapo unavyoishi ni hisani tu.

BTW najua hii ni chai, miaka 29 hauwezi kuwa na akili za kitoto kiasi hicho 😂.
wapo wa hivyo mkuu ila sio kwa shemeji
 
Bro miaka 29 unajiita kijana mdogo looooh mpaka hapo ushafeli badilisha fikra zako mkuuu hio ni 30 yrs bado huna dira mbaya zaidi unaishi na nyoka [emoji216] huyo dada na mmeo sio ndugu zako bro kaa chonjo mkuuu [emoji90][emoji90][emoji90] alafu kwann hukuchukua degree na muda umesonga hivyo mpaka unafikisha 29 huo muda wote ulikuwa unafanya nn [emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Daaah ila bro toka hapo toka hapo bro kabangaize chochote ila usikae kutwa hapo ndani

Ohoooo
Nilikuwa nafanya kilimo. sikuweza kusoma digree
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Wewe wa kutiwa bakora kabisa. Shemeji yako siyo baba yako wala mama yako, sio wajibu wake kukulea na kukupa mtaji, hata hapo unavyoishi ni hisani tu.

BTW najua hii ni chai, miaka 29 hauwezi kuwa na akili za kitoto kiasi hicho 😂.
Alafu jamaa badala ya Kusema shemeji, anasema mume wa dada 😅😅😅
 
Back
Top Bottom