Mume wa mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Nigeria (Osinachi Nwachukwu) akamatwa

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Polisi wamemkamata mume wa mwimbaji nyota wa nyimbo za Injili nchini Nigeria, Osinachi Nwachukwu, baada ya kufariki siku ya Ijumaa Aprili 8, 2022 katika hospitali ya Abuja.

Ripoti za awali zilisema kuwa msanii huyo mwenye umri wa miaka 42 alikuwa akiugua saratani ya koo, lakini familia yake inakanusha hilo, ikidai kuwa alikuwa mwathirika wa unyanyasaji wa nyumbani.

Mumewe Peter Nwachukwu bado hajatoa maoni yake. Msemaji wa polisi alisema uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha kifo chake.

Osinachi Nwachukwu alikuwa mmoja wa wasanii maarufu wa injili wa Nigeria, na sauti yake ikielezewa kama ya "malaika".

Alishiriki katika wimbo wa injili wa 2017 wa Ekwueme, ambao umetazamwa mara milioni 71 kwenye YouTube. Wanigeria wengi, hasa Wakristo, wamekipokea kifo chake kwa huzuni na hasira.

Baadhi wameingia mtandaoni kuwataka viongozi wa dini kutowashauri waumini wa kanisa hilo kusalia katika mahusiano mabaya. Vurugu za majumbani pia zimekuwa zikivuma kwenye mitandao ya kijamii.

Kanisa maarufu ambalo hapo awali lilimwajiri Nwachukwu kama mwimbaji mkuu, Dunamis International Gospel Centre, bado halijatoa maoni yoyote kuhusu kifo chake, lakini linasema litatoa tamko hivi karibuni.

Kanisa hilo lilishiriki video fupi na BBC ambayo ilisema ilifunza waumini wake kwamba ni bora kuwa mseja na kuwa hai kuliko kufa katika ndoa yenye dhuluma.

Osinachi Nwachukwu ameacha watoto wanne.
 
1683243749284.jpg
 
Back
Top Bottom