Sakayo
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 56,368
- 161,463
JamaniJamaniiiii acheni atafunwe, mtu gani huyu kila ushauri anaupanguamtu, mzima huyu mnamuelekeza nini achane akatafunwe moyo wake ufurahie
JamaniJamaniiiii acheni atafunwe, mtu gani huyu kila ushauri anaupanguamtu, mzima huyu mnamuelekeza nini achane akatafunwe moyo wake ufurahie
halafu anajinadi kwamba ana hofu ya Mungu, imagine kwa mtu ambaye hana hofu ya Mungu hali itakuajeKuna vitu vingine hata si vyakuomba ushauri,unaabisha wanawake wenzako,wanaume watuone punguani
Hata aiingii akilini,hivi kweli mlikuwa marafiki ukamtamkia unampenda akakuambia anamchumba,hamjawahi sex bado ukampenda hivyo hivyo
Wakati mi mwanaume akinijibu kama hivyo nashukuru kuujua ukweli kuwa ana mtu wake kupenda naacha hapohapo,nabaki kuheshimu mahusiano ya MTU,afu siwezi kusharehuku najua.
Tuachane na hayo umeolewa mnaishi kwa amani,bado unatafutana na huyo rafiki mnarushiana picha za uchi serious??!!
Afu zikija kuvuja utasema shetani alikupitia,badilika unajua kuna mambo mengine hata shetani atawakana
So sad,namuonea huruma Huyo mume alokuweka ndani afu unakipiga picha kitumbua chake unamtumia mwanaume mwingine si ajabu Mr katoka kukishave mwenyewe ajionee kinavutia
Aisee ushauri wangu badilika,mapepo ya ngono na usaliti mnayataka wenyewe kwa kutokulidhika na mlivyo navyo siku vikipotea ndo mtajua thamani yake.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani mbona kama ulisema umeshaolewa?Kwanini watu wanapenda kuishi Jehanam wakiwa duniani kisa ndoa?? Mimi waolewe tu wote nitacheza kwaito ila ndoa ya kuonekana bado nipo nipo sana. Nikiolewa ni mapenzi hamna kingine
Sent using Jamii Forums mobile app
Ohhh kumbe, nimemshauri sidhani kama nimekosea kumpa ushauri wangu, achague kunyoa ama kusukaUmeguswaaaaa
Utakuwa wale wanaojitangaza kumbe feki.
Kuna kimwalimu humu cha chekechea utasikia kinasema umechapia, watu hawakosi vitukoBabu nakusalimia
I'm the girl from nowhere,... the one no one will miss .... that's why they choose me...![]()
Wewe unajua kwamba kuchepuka ni nini?Habari za weekend wakuu
Miaka 7 iliyopita nilikutana na kaka mmoja Muheza Tanga alikuwa kikazi na mimi pia nilikuwa nipo pale kikazi. Tulikuwa marafiki sana nikajikuta nampenda sana ila yeye alikuwa na mahusiano yake.
Basi siku moja uzalendo ukanishinda nikamwambia M, nakupenda sana akasema hata yeye ana hisia na mimi ila ana mchumba wake anamsomesha so hawezi kumuacha. Basi niliumia lakini nilimuelewa tukabaki kuwa marafiki.
Baada ya mwaka nikapata mchumba nikaolewa, nikabahatika kupata watoto wawili na mume wangu ambae naishi nae mpaka sasa kwa kweli Mr ananipenda na wote tuna hofu ya Mungu hatujawahi kuumizana kwa namna yoyote miaka yote mitano tuliiishi wote.
Jamaa yangu yule wa Muheza naye mwaka juzi akaoa, lakini ndoa yao haina amani wanagombana kila siku.
Mwaka jana waligombana M, akanitafuta kuwa wife anamsumbua na wametengana basi tukajikuta tumefall in love tunatumiana picha mpaka za uchi nikajikuta nampenda sana kuliko hata mume wangu na hapo hatujawahi kusex hata siku moja.
Mwaka jana wakapatanishwa na wife wake, akaniambia nikamwambia sawa sababu hata mimi pia nina mume so sio big inshu.
Akaniambia, "Unajua nini V, tulia kwenye ndoa yako Mungu amekupa mume mzuri na mnaishi kwa amani acha mm nipambane na hali yangu. Nilikupoteza kwa ujinga wangu ingawa bado nakupenda lakini mumeo akija kuona chat zetu atakuua."
Niliumia nikamwambia okey lakini umeniteka akili yangu naumia sana juu yako, natamani tukutane hata siku moja tupeane raha halafu tuachane akasema sawa ila mawasiliano na mimi kapunguza anaogopa mke wa mtu na mimi nimeshadata kwake.
Sijawahi kuchepuka hata siku moja namuogopa Mungu, namuogopa mume wangu akijua itakuwaje sababu ananiamini sana.
Yule jamaa wa Muheza nampenda sana tena sana na yeye ananipenda lakini naogopa kuchepuka.
Naombeni ushauri, nifanyeje?
Sent using Jamii Forums mobile app
you have said it all my dear! yaani umeniponya mpk mimi, nakushukuru sana.Wewe wala huna pepo wala nini ni katabia tu ambako kalikuwa introduced sasa kamekuwa ni mazoea sasa ndo yanakutesa, katika jamii yetu ya kimahusiano kitu kinachoitwa chatting ni kibaya sana sana yaani kinapenya mpka uvunguni mwa moyo, mahusiano yanajengwa sana kwa asilimia kubwa na mawasiliano, na hasa sisi wanawake ugonjwa wetu upo hapo kwenye mawasiliano,the more mtu anavyokuweka karibu sana unajikuta unampenda unampenda mpka basi,unapigwa upofu haswaa mpka yule aliyekaribu nawe unamuona si lolote na utaanza kuona madhaifu yake kama wewe hapo ushaanza kuona kama hulizishwi,Mara kama mrefu utamuona mrefu sana,kama mfupi utamuona mfupi Sana yaani utatafuta vitu kibao vya kukupa uhalali wa wewe utoke nje. Dhambi huanza mawazoni kama tamaa,kisha wazo lile ukiendelea kulilisha linakupa nguvu ya kusema,nguvu ya kuongea inaenda kuzaa tendo.
Huyo jamaa kiukweli humpendi kabisa basi tu mawasiliano yamekufanya udate na inavyoonekana jamaa ana maneno matamu kama asali,mpaka hapa ulipofika uko kwenye mstari wa 0.9999 Kuanguka,so unanafasi ya 0.1 tu kujiokoa, kama kweli jamaa kakushauri hivyo ujue amesoma kitu kwako kashindwa kukuambia ukweli wako kwamba hufai akaona tu akwambie kwa uzuri stick na mume wako.
Cha kufanya kama kweli unataka kujiokoa na una hofu ya Mungu kweli na unampenda Mume wako kidhati na unajipenda mwenyewe na unawapenda watoto wako,fanya yafuatayo block jamaa huyo katika njia zote mnazowasiliana,Utateseka wiki moja tu baada ya hapo utakaa sawa. ule muda uliokuwa unatumia kuchat na huyo jamaa utumie kuchat na mumeo na Ibada,yale maneno matamu uliyokuwa unamwambia jamaa yako mwambie Mume wako na Mungu wako. kama mume mzito kujibu mwambie tu vile unavyojiskia ukiwa unachat naye. Jikite zaidi kwenye ibada na ujipe ubize haswaaa jitahidi usiwe idle,kila wakati uwe na jambo la kukupa ubize,tumia muda wako zaidi na Mungu na familia yako na kazi zako, mwili usipoupa kazi wenyewe utakupa kazi,wazo chafu likiingia akilini mwako la kumkumbuka jamaa crash hilo wazo haraka Sana waza vitu vingine,anza kuliona hilo lijamaa libayaaaa likosoe uwezavyo,lina mke,limekutumia dudu fake,yaani tafuta yote mabaya vile utakavyoilisha akili yako juu yake ndivyo itakuwa ni wiki 2 tu utakuwa sawa hadi utajiona jinsi gani ulivyokuwa mjinga ukataka kujiangamiza. Mwisho jikite kwenye ibada kama wewe ni Mkristo soma zaidi Biblia,nenda kanisani,kaa na wanao wape story za Biblia na fanya nao ibada na ufatilie mambo yao ya shule,nenda kafanye huduma kanisani,toka out na mumeo si unafanya kazi bana siku moja msuprize,tafuta marafiki wapya wazuri wakukujenga kiroho, Hayo mawazo machafu yote yanayokunyemelea utayashinda. Kila la heri.
Sent using Jamii Forums mobile app