Mume wa mtu ananitesa

Mume wa mtu ananitesa

Dada tulia kwenye Ndoa yako siku zote majuto ni Mjukuu.
Anataka abadili radha japo siku moja.
Maana amesema wanaishi na mume wake vizuri tu kila kitu kiko sawa. Sas m najiuliza kipi kinafanya azidi kutamani kwenda nje ya ndoa?
Nimegundua huenda ni radha. Ila namshauri asijaribu maana asali huwa haionjwi mara moja lazima atataman tena na tena!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za weekend wakuu

Miaka 7 iliyopita nilikutana na kaka mmoja Muheza Tanga alikuwa kikazi na mimi pia nilikuwa nipo pale kikazi. Tulikuwa marafiki sana nikajikuta nampenda sana ila yeye alikuwa na mahusiano yake.

Basi siku moja uzalendo ukanishinda nikamwambia M, nakupenda sana akasema hata yeye ana hisia na mimi ila ana mchumba wake anamsomesha so hawezi kumuacha. Basi niliumia lakini nilimuelewa tukabaki kuwa marafiki.

Baada ya mwaka nikapata mchumba nikaolewa, nikabahatika kupata watoto wawili na mume wangu ambae naishi nae mpaka sasa kwa kweli Mr ananipenda na wote tuna hofu ya Mungu hatujawahi kuumizana kwa namna yoyote miaka yote mitano tuliiishi wote.

Jamaa yangu yule wa Muheza naye mwaka juzi akaoa, lakini ndoa yao haina amani wanagombana kila siku.

Mwaka jana waligombana M, akanitafuta kuwa wife anamsumbua na wametengana basi tukajikuta tumefall in love tunatumiana picha mpaka za uchi nikajikuta nampenda sana kuliko hata mume wangu na hapo hatujawahi kusex hata siku moja.

Mwaka jana wakapatanishwa na wife wake, akaniambia nikamwambia sawa sababu hata mimi pia nina mume so sio big inshu.

Akaniambia, "Unajua nini V, tulia kwenye ndoa yako Mungu amekupa mume mzuri na mnaishi kwa amani acha mm nipambane na hali yangu. Nilikupoteza kwa ujinga wangu ingawa bado nakupenda lakini mumeo akija kuona chat zetu atakuua."

Niliumia nikamwambia okey lakini umeniteka akili yangu naumia sana juu yako, natamani tukutane hata siku moja tupeane raha halafu tuachane akasema sawa ila mawasiliano na mimi kapunguza anaogopa mke wa mtu na mimi nimeshadata kwake.

Sijawahi kuchepuka hata siku moja namuogopa Mungu, namuogopa mume wangu akijua itakuwaje sababu ananiamini sana.

Yule jamaa wa Muheza nampenda sana tena sana na yeye ananipenda lakini naogopa kuchepuka.

Naombeni ushauri, nifanyeje?



Sent using Jamii Forums mobile app
Kata, vunja tupilia mbali mawasiliano na huyo M.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka apo sifa ya uhaminifu ushaipoteza YESU alisema "ukimuona mke au Mme ukamtamani tayari ushazini naye".
Ushauri wa bure mweleze ukweli uyo X bandia wako kuwa unampenda mumeo nayeye ampende mke wake alafu mkate mawasiliano kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mke wangu nyumbani unanisumbua mara unaumwa tumbo nakula mara moja kwa miezi 2 hvi Tanga walikufanya nini. Ngoja nisubiri huu mchezo wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiolewa kumkomesha ex na mashosti jiandae kuhangaika ndoani aisee better marry when ur ready

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini watu wanapenda kuishi Jehanam wakiwa duniani kisa ndoa?? Mimi waolewe tu wote nitacheza kwaito ila ndoa ya kuonekana bado nipo nipo sana. Nikiolewa ni mapenzi hamna kingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini watu wanapenda kuishi Jehanam wakiwa duniani kisa ndoa?? Mimi waolewe tu wote nitacheza kwaito ila ndoa ya kuonekana bado nipo nipo sana. Nikiolewa ni mapenzi hamna kingine

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni kwa waliokomaa na kupevuka kiumri na kiakili.

Kwa umri alioolewa mleta mada sidhani kama mawazo haya yanaweza kuwa mujarabu na yakafanya kazi kwenye ubongo wake
 
Mleta mada alikua anataka ndoa. Labda alikua kwenye umri wa kukata tamaa akaona achukue chochote tu kilicho mbele yake.
Hii ni kwa waliokomaa na kupevuka kiumri na kiakili.

Kwa umri alioolewa mleta mada sidhani kama mawazo haya yanaweza kuwa mujarabu na yakafanya kazi kwenye ubongo wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom