Mume ana gari tatu, natembea kwa miguu

Mume ana gari tatu, natembea kwa miguu

Sijui nicheke, dah kumbe sisi wanaume tuko wa aina nyingi duniani
 
Naona VIGIMBI viko around the corner.
 
Kuna tatizo lililojificha. kwa nini magari matatu halafu mwendeshaji awe mmoja pekee wakati wote ni wamoja?
 
Kwani huyo mwanamke akijifunza gari itakuaje? Mleta mada anamkera sana mumewe. Laiti angejua, kesho angeamkia shule ya udereva. Kumbuka hajaongelea lolote kuhusu funguo kufichwa so ni mapema sana kumwita mumuwe mbinafsi.

nimemwona mbinafsi hata pale wanapotoka kazini pamoja jamaa bila aibu kwenye gari kapandisha vioo na AC juu mkeo bodaboda shame on him...............unaona taabu gani kwa upendo kumwambia mkeo nimenunua gari nenda kajifunze baada ya hapo unamwonyesha litakalokuwa lake si ndio upendo kwani lazima umjaribu kwa kuangalia atafanya nini.....wakati mwingine mwanaume anakuwa mbogo kiasi mwanamke athubutu kuuliza wala kufanya kitu
 
tafuta sehemu ujifunze driving,

siku ya siku akukute tu automatically kwenye usukani...

It may happen a problem at home where an emergence drive is needed. Imagine you are only you at home...

Take that tip.
 
hili swala hata mimi nimelishuhudia kwa shemeji zangu wa kichaga zaidi ya watatu wana hii tabia tena wengine mke anakata hadi majani ya ng'omne wakati vibaruwa wamejaa jijini.
 
nimemwona mbinafsi hata pale wanapotoka kazini pamoja jamaa bila aibu kwenye gari kapandisha vioo na AC juu mkeo bodaboda shame on him...............unaona taabu gani kwa upendo kumwambia mkeo nimenunua gari nenda kajifunze baada ya hapo unamwonyesha litakalokuwa lake si ndio upendo kwani lazima umjaribu kwa kuangalia atafanya nini.....wakati mwingine mwanaume anakuwa mbogo kiasi mwanamke athubutu kuuliza wala kufanya kitu

Kurudi kazini mwanamke ndo anawahi kutoka ili akafanye tena mawili ma3 kama nimemwelewa. Sawa na anavyochelewa kwenda..... Dadaangu, mpaka mumewe afikie kumwacha tu (na huyu dada hajasema mengi kumhusu), alishaonyesha tangu mapema kutojiongeza kwenye madogomadogo. Na hii inakeraga sana! Mwanaume inabidi uwe mbogo manake atakuangusha tu huyu. ni mzito sana!!

Aniwie radhi ila kanikumbusha visa vingi sana vya wanawake kupenda mteremko as if hawakupewa akili, maarifa na utashi (kama vinatofautiana) 🙁
 
Dah!!!! Yaani yaliyomo ndani ya baadhi ya hizi ndoa yanasikitisha sana. Njemba mmoja alikuwa anamdate mrembo ambaye alikuwa UDSM, baada ya kumaliza njemba hakutaka afanye kazi eti atatongozwa basi akawa mama wa nyumbani lakini mke akangangamara ili akasome Masters kwa kuwa mumewe alikuwa ana uwezo wa kumsomesha. Mume akamzungusha hatimaye akakubali mrembo akamaliza vizuri lakini bado mume hakutaka atafute ajira. Mume kapoteza kazi maisha yakawa magumu sana maana wote wakati huo hawana kipato, ndiyo mume kukubali mke naye aanze kutafuta kazi na hatimaye yeye akaanza kupata na hivyo kuiwezesha familia kupata mahitaji yao muhimu ya maisha.

Kuna baadhi ya wanaume wana akili finyu sana. Huyu hajui siku moja usiku wa maanane anaweza akawa hoi bin taabani inabidi awahishwe hospitali, kama mke anafahamu kuendesha basi ni kiasi cha kuingia tu ndani ya gari na kuwahi hospitali vinginevyo ni kuanza kutafuta taxi na usiku wa maanane inaweza kuchukua muda mpaka kuja kuipata. Muda ambao unaweza kuwa muhimu sana kwa mgonjwa.


Kuna mmoja ashaambiwa instructors watamtongoza, sijui watamshika mapaja excuse kibao zisizokuwa na msingi. Akapatikana mwalimu wa kike akaenda shule 2yrs now huyo dada hajawahi kuendesha gari la nyumbani.
 
Hata mi nisikufundisha, ujue kuendesha gari ili ukawabebe wauza sura mi nikiwa safari? Eboooo

Most of women ni careless sana tv zenyewe wanaharibu je gari si ndio mtaliua kabisa.
 
aaaah huna bado nia ya kutak kujua nadhan maan km mzee yuko bzee unadhan kuna tme atakuja aanze hay mke wang njoo n kufundishe wap kaa chin ongea naye drivng school kibao mitaan
 
Back
Top Bottom