Castle_Lite
JF-Expert Member
- Sep 10, 2016
- 4,505
- 9,964
Maelezo marefu sana.Qur'an si kama vitabu vya tamthilia ya kuwa kwa kila msomaji atatoka kwa namna alivyoelewa kulingana na uelewa wake. Kwenye Qur'an au kwenye hadithi hakuna "mimi ninavyoona" hiyo hakuna. Ni lazima utoke na makusudio husika kwa kila aya husika. Kwa kututahadharisha Mtume akatuambia: "Yeyote atakayetumia rai (yake) kwenye kitabu cha Mwenyezi Mungu, mapema makazi yake ajiandalie motoni". Kwa sababu ukitafsiri wewe utakuwa unafanya mzaha!
Na kwenye Qur'an Mwenyezi Mungu alishahukumu ya kwamba; kuna watu duniani wanajiona wanafanya mema kumbe kwa Mungu hawana lolote. Kwa sababu wao aya za Mungu na Mitume yake walichukulia mzahamzaha.
Ili usifanye mzaha inakubidi urudi kwa wanawazuoni wenye isnad iliyothabiti ambao wanafahamika, wao ndiyo wakufahamishe hiyo aya ina maana gani! Na vitabu vyao vya tafsiri vipo! Ukitafsiri wewe unafanya mzaha!
Maadamu unauhukumu uislamu inakubidi urudi katika misingi ya uislamu ya namna ya kuielewa aya husika unaielewa kwa namna gani ? Uislamu unasema Qur'an inatafsiriwa kwa nyezo tatu:
1) Qur'an bi Qur'an
2)Qur'an bi Sunna
3)Qur'an bi Swahaba
Tuambie wewe umetafsiri kwa namna gani?
----------------------------
Halafu tukusaidie: Jini si jina la kiumbe mmoja. Jini ni neno la uainishaji linalomaanisha viumbe hai kwenye kundi wenye sifa zinazofanana. Hawa viumbe hai kwa ujumla ndiyo wanaitwa jini/majini.
Ili urudi uelewe aliyekusudiwa ni jini yupi inakubidi urudi kwenye tafsiri na wala siyo ulichoelewa wewe.
Na sijaona point ya kuchukua.
Maana hujajibu hoja.
Umejikita kujua mtoa hoja katumia vigezo gan.
Hebu jikite kwenye hoja.