Domo Kaya
JF-Expert Member
- May 29, 2007
- 531
- 59
Story na Uwazi,
Mwandishi Elvan Stambuli.
Mwandishi Elvan Stambuli.
' Mufti wa Tanzania shehe Shaabani Simba alialikwa katika kalamu ya Sikukuu ya Idd ya Rais Jakaya Kikwete Ikulu na kumtuma msaidizi wake Naibu Mufti wa Tanzania Shehe Abubakar Zuberi akiwa na mashehe wengine walijikuta wakitimuliwa Jumamosi iliyopita.
Habari zilizofikia gazeti hili siku ya tukio zinasema wakati wa kwenda Ikulu jijini Dar Es Salaam, Naibu Mufti Shehe Zuberi alifuatana na viongo wa ngazi ya juu wa baraza kuu la waislam Tanzania (BAKWATA) akiwemo katibu wa baraza la Ulamaa na kamishna wa Tume ya kudhibiti Ukwimwi (TACAIDS) sheikh Hassan Chizenga na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa, shehe abdallah Nyasi.
Naibu mufti alimuruhusu Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Ali Nguruko kuzungza na Uwazi ambapo alisema wamefedheheshwa sana na waliyofanyiwa Ikilu.
Alifafanua zaid sheikh Nguruko alisema Kikwete aliswali swala ya Iddi katika msikiti wa Al Farouk, makao makuu ya Bakwata na kuwaagiza waende Ikulu ktk karamu aliyoiandaa bila kukosa.
Tuliondoka baada ya kuagana na Rais mstaafu Ali Hassani Mwinyi ambaye pia aliwasili hapa tulipofika getini Ikulu tulipekuliwa kwa kufunuliwa kanzu zetu, hata Naibu Mufti alifunuliwa tilisikitika sana tulijiuliza hawa hawajui kuwa Mashikh hawa ndio waliomswalisha Rais leo.
Aliongeza kuwa kilichowasikitisha zaidi ni kuona raia wa kigeni wakipita na kuingia Ikulu bila ya kupekuliwa kama tulivyofanywa sisi. Kibaya zaidi alisema ni jopo zima la Bakwata kutoruhusiwa kuingia Ikulu kama alivyoagiza Rais Kikwete.'