Mufti afungua rasmi dua kubwa ya kimataifa

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,209
4,706
Hatimaye siku adhimu na tukio muhimu, nyeti na lenye kupendeza kwa Allah na mtume wake, Muda wa kuanza dua kubwa umewadia.

Samaha Mufti wa Tanzania, Mujaddidul Asri, amefungua Dua Kubwa ya Kimataifa leo Alhamisi Alfajiri kwenye msikiti mkuu Bakwata makao makuu, msikiti wa Mfalme Mohammed VI

Tukio hilo adhimu na Muhimu ambalo limesubiriwa kwa hamu kubwa kwa muda mrefu limefanyika leo likiratibiwa vyema na kamati maalum inayofanya kwazi kwa weledi mkubwa inayoongozwa na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Mama mchapa kazi aliye macho muda wote Mh. Mwantumu Mahiza na katibu Msomi wa ndazi ya juu alhaj Imamu Swedi Twayyib (ambaye alitunukiwa shahada ya Uimamu na Mufti almarhoum Sheikh Hemed Bin Jumaa bin Hemed)

Katibu Mkuu wa Bakwata Alhaj Nuhu Jabir Ibnu Mruma Ashighatiiniy AlMwangawiy akiwa mtendaji mkuu wa Bakwata naye ameendelea kuhakikisha kula jambo linakwenda vyema

Wajumbe kadhaa wa Baraza la Ulamaa, Viongozi wa kitaifa na mikoa na waumini wengi wamehudhuria ufunguzi huo ambao ni mwanzo wa mfululizo wa matukio mbalimbali yaliyopangiliwa kwa ustadi mkubwa yatakayofanyika siku tatu mfululizo.

Wadau na watafiti wabobezi wa masuala ya dini wa kitaifa na kimataifa wamemwambia Mwandishi maalum wa Mufti kwamba kitendo cha Waumini na viongozi kujihimu kuamka usiku manane na kumiminika msikitini hapo mapema Alfajiri kutoka maeneo mbalimbali ya mbali na ya karibu kwenye jiji hili Kubwa na lenye Amani La Dar es salaam na mikoani ni ishara wazi sana ya Utii mkubwa, Umoja uliokomaa, mabadiliko chanya na makubwa sana yanayokuja, utendaji makini wa kamati uliotukuka sana na mapenzi makubwa na uzalendo wa hali ya juu wa waislamu na viongozi wao kwa taifa lao tukufu.

Aidha imeelezwa kwamba Waislamu wameonyesha kivitendo kwamba wanatambua kwa kina sana na wanathamini mno kazi njema na kubwa za dini zilizofanywa na wakale wao ambao walitumia ipasavyo nguvu, elimu, vyeo na mali zao kuendeleza dini

Leo pamoja na mambo mengine Waumini na viongozi hao watatembelea maeneo ya makaburi pamoja na kufanya maombi/Dua ndefu na mambo mengine mema.

Viongozi wakuu wa Serikali yetu tukufu ya Tanzania na serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Viongozi wakuu wa kiislamu kutoka nchi zaidi ya kumi na idadi kubwa ya mabalozi watajumuika na waumini kwenye hizi siku tatu za dua ambayo pia itawaombea Viongozi wa Dini wakiongozwa na Samaha, Fakhama, Saada, Assayyyid, Almuhtaram, kipenzi cha waislamu na mwanamapinduzi, mbunifu anayeona mbali, Mufti na sheikh Mkui wa Tanzania Dr. Abubakar Zubeir Ali ibnu Mbwana Almukarram pamoja na viongozi wa Serikali yetu wakiongozwa na jemedari mahiri, makini, mchapa kazi kipenzi cha wananchi mama Yetu Samia binti Suluhu Ibnu Hassan.

Uchunguzi wa kitaalamu uliofanywa na jopo la wanahabari wa ngazi ya juu na wakongwe wanaoripori tukio hili wakiongozwa na mtaalamu nguli Alhaj Said ibnu Mpeta umebaini kwamba tukio hili linafuatiliwa hatua kwa hatua na viongozi wa taasisi za kiislamu, vyama vya siasa, jumuia za kiraia na waumini wa dini zote Kote Afrika Mashariki na Kati.

Aidha misafara inaendelea kuelekea jijini Dar es salaam kutoka mikoa mbalimbali kuhudhuria tukio hili.

Kwa niaba ya Ofisi ya Mufti tunawatakia Utulivu wote waliofika na kuwatakia hatua zisizo na vikwazo wote ambao wapo njiani kuja kujumuika na Wabaji.
....

Dr. Harith Nkussa
Mwandishi Maalum wa Mufti
Mtumishi Wenu Mtiifu
Saa moja na dkk 12 Asubuhi
Alhamisi 22.2.2024

1708616317129.jpg
1708616328520.jpg
1708616337321.jpg
 
Back
Top Bottom