sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,033
Niliwahi kuleta hapa hii maada takribani miezi miwili iliyopita ila mnisamehe bure nilisahahu kuleta mrejesho
kiufupi niliitwa shuleni kama mzazi mimi pamoja na wazazi wengine, mwanangu wakimsingizia kushawishi watoto zao waache kupanda schoolbus wawe wanatembea kama mwanangu na wenzake wachache wasiopanda school bus.
Naweza kusema kesi niliishinda kirahisi mno, maana hata watoto hao wanaodhaniwa wanashawishiwa kutopanda school bus, walikiri hawajashawishiwa ila ni wao tu hawataki kupanda school bus, wao wanataka wawe wanatembea.
Licha ya hivyo wazazi walifuka na kukandia hasara za kutopanda schoolbus, point zao zilikuwa ni usalama wa watoto, watoto kuwahi kufika shule, watoto kufika shuleni wakiwa hawajachoka, nk.
Mimi point yangu ya kwanza ilikuwa kama mwanangu hajawashawishi watoto wao wasipande school bus ila ni wenyewe tu wanataka kumwiga mwanangu je mwanangu anahusikaje 😂 😂
Kiufupi nilianza kutiririka sababu za mimi kuamua mtoto wangu kutopanda school bus ( ghaama ya school bus kwangu sio tatizo kabisa)
1. Afya ya mtoto huimarika kwa kufanya zoezi la kutembea, umbali wa nyumbani hadi shuleni ni dakika kama 20 tu kwa mwendo wa kawaida kabisa, mara chache chache mimi au mke wangu tunampa lifti ya gari tunapoenda kwenye shughuli zetu
2. Kuna mamilioni ya watoto wa shule za msingi hasa za serikali huwa wanatembea kwenda shuleni, shida iko wapi mwanangu kambatana na wenzake kwenye kutembea, kuna shule ipo karibu yao ni ya serikali, wenzake wengi tu huwa wanakutana njiani na hakuna tatizo.
3. Kwa sasa naweza nikawa na uwezo wa kulipia hiyo school bus, ila hali yangu ya kiuchumi ikibadilika mtoto wangu atapata shida.
hizo ndizo zilikuwa sababu zangu, ila zaidi ya hapo, kuna mtoto flani anajiamini sana hana uwoga akaelezea sababu zake
Yeye kwa niaba ya wenzake alisema walikuwa wanapenda wanavyoona mtoto wangu pamoja na wenzake wachache wasiopanda school bus pale wakitoka shuleni, kuna shule karibu sana ya serikali kuna uwanja wa mpira, hapo huwa wakitoka shuleni wanapata nafasi ya kujumuika na kucheza na wenzao wa hio shule, Sasa hawa wanaopandaga school bus huwa hawarusiwi kutoka nje ya geti la shule, huwa wanajisikia vibaya wanapoona rafiki zao wanacheza na watoto wa shule nyingine baada ya kutoka shule.
Lakini pia hapo uwanjani wanapokutana na watoto wengine, mwanangu na rafiki yake aliemzidi darasa moja ambae nae hapandi school bus, walijifunza sarakasi kadhaa na hata mimi nikiri tu kwamba kipaji cha sarakasi cha mwanangu si haba, sasa wakirudi hio shule yao wakianza kuruka ruka hizo sarakasi wenzao wanakusanyika kushangaa, hii nayo ndio ikawa inapelekea nao wengine wasitake kuoanda school bus ili wawe wanajifunza hayp mambo kuna sehemu ipo karibu na shule kuna watoto huwa wanaruka ruka sarakasi, basi huwa wanabaki kuwa wapenzi watazamaji tu wakiwa ndani ya school bus.
Kiufupi sababu ndizo zilikuwa hizo, lakini licha ya hivyo wazazi waliona watoto wao bado ni wadogo sana waliokuwa wakiongea utoto mwingi n.k kwa hio waliwakataza kabisa watoto zao kurudia tena kuibua upya haya mambo.
Leo nimeandika hii maada baada ya mtoto flani kuwa kiburi na kutaka kufosi nae asiwe anapanda school bus, wazazi wake wanamtandika sana lakini ikifika mida ya kutoka anakwepa school bus 😂😂 ila watoto bwana.
ni hayo tu ndugu zangu
Walimu wanamsingizia kiuonevu mwanangu, je ni hatua gani nichukue kama mzazi?
Ipo hivi, mwanangu anasoma shule fulani English medium, mimi haya mambo ya schoolbus niliyakataa kabisa maana kuna wenzake wengi tu wanatembea na hata mimi baba yake siijui school bus maisha yangu ya elimu, ila pia niliona atembee tu ili kunyoosha miguu kwa afya yake. Sasa pale shuleni kwao...
www.jamiiforums.com