Muendelezo wa yaliyojiri kwenye kesi ya mwanangu, wazazi msiwabane sana watoto!

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,014
Niliwahi kuleta hapa hii maada takribani miezi miwili iliyopita ila mnisamehe bure nilisahahu kuleta mrejesho

kiufupi niliitwa shuleni kama mzazi mimi pamoja na wazazi wengine, mwanangu wakimsingizia kushawishi watoto zao waache kupanda schoolbus wawe wanatembea kama mwanangu na wenzake wachache wasiopanda school bus.

Naweza kusema kesi niliishinda kirahisi mno, maana hata watoto hao wanaodhaniwa wanashawishiwa kutopanda school bus, walikiri hawajashawishiwa ila ni wao tu hawataki kupanda school bus, wao wanataka wawe wanatembea.

Licha ya hivyo wazazi walifuka na kukandia hasara za kutopanda schoolbus, point zao zilikuwa ni usalama wa watoto, watoto kuwahi kufika shule, watoto kufika shuleni wakiwa hawajachoka, nk.

Mimi point yangu ya kwanza ilikuwa kama mwanangu hajawashawishi watoto wao wasipande school bus ila ni wenyewe tu wanataka kumwiga mwanangu je mwanangu anahusikaje 😂 😂

Kiufupi nilianza kutiririka sababu za mimi kuamua mtoto wangu kutopanda school bus ( ghaama ya school bus kwangu sio tatizo kabisa)

1. Afya ya mtoto huimarika kwa kufanya zoezi la kutembea, umbali wa nyumbani hadi shuleni ni dakika kama 20 tu kwa mwendo wa kawaida kabisa, mara chache chache mimi au mke wangu tunampa lifti ya gari tunapoenda kwenye shughuli zetu

2. Kuna mamilioni ya watoto wa shule za msingi hasa za serikali huwa wanatembea kwenda shuleni, shida iko wapi mwanangu kambatana na wenzake kwenye kutembea, kuna shule ipo karibu yao ni ya serikali, wenzake wengi tu huwa wanakutana njiani na hakuna tatizo.

3. Kwa sasa naweza nikawa na uwezo wa kulipia hiyo school bus, ila hali yangu ya kiuchumi ikibadilika mtoto wangu atapata shida.

hizo ndizo zilikuwa sababu zangu, ila zaidi ya hapo, kuna mtoto flani anajiamini sana hana uwoga akaelezea sababu zake

Yeye kwa niaba ya wenzake alisema walikuwa wanapenda wanavyoona mtoto wangu pamoja na wenzake wachache wasiopanda school bus pale wakitoka shuleni, kuna shule karibu sana ya serikali kuna uwanja wa mpira, hapo huwa wakitoka shuleni wanapata nafasi ya kujumuika na kucheza na wenzao wa hio shule, Sasa hawa wanaopandaga school bus huwa hawarusiwi kutoka nje ya geti la shule, huwa wanajisikia vibaya wanapoona rafiki zao wanacheza na watoto wa shule nyingine baada ya kutoka shule.

Lakini pia hapo uwanjani wanapokutana na watoto wengine, mwanangu na rafiki yake aliemzidi darasa moja ambae nae hapandi school bus, walijifunza sarakasi kadhaa na hata mimi nikiri tu kwamba kipaji cha sarakasi cha mwanangu si haba, sasa wakirudi hio shule yao wakianza kuruka ruka hizo sarakasi wenzao wanakusanyika kushangaa, hii nayo ndio ikawa inapelekea nao wengine wasitake kuoanda school bus ili wawe wanajifunza hayp mambo kuna sehemu ipo karibu na shule kuna watoto huwa wanaruka ruka sarakasi, basi huwa wanabaki kuwa wapenzi watazamaji tu wakiwa ndani ya school bus.

Kiufupi sababu ndizo zilikuwa hizo, lakini licha ya hivyo wazazi waliona watoto wao bado ni wadogo sana waliokuwa wakiongea utoto mwingi n.k kwa hio waliwakataza kabisa watoto zao kurudia tena kuibua upya haya mambo.

Leo nimeandika hii maada baada ya mtoto flani kuwa kiburi na kutaka kufosi nae asiwe anapanda school bus, wazazi wake wanamtandika sana lakini ikifika mida ya kutoka anakwepa school bus 😂😂 ila watoto bwana.

ni hayo tu ndugu zangu
 
Niliwahi kuleta hapa hii maada takribani miezi miwili iliyopita ila mnisamehe bure nilisahahu kuleta mrejesho

kiufupi niliitwa shuleni kama mzazi mimi pamoja na wazazi wengine, mwanangu wakimsingizia kushawishi watoto zao waache kupanda schoolbus wawe wanatembea kama mwanangu na wenzake wachache wasiopanda school bus.

Naweza kusema kesi niliishinda kirahisi mno, maana hata watoto hao wanaodhaniwa wanashawishiwa kutopanda school bus, walikiri hawajashawishiwa ila ni wao tu hawataki kupanda school bus, wao wanataka wawe wanatembea.

Licha ya hivyo wazazi walifuka na kukandia hasara za kutopanda schoolbus, point zao zilikuwa ni usalama wa watoto, watoto kuwahi kufika shule, watoto kufika shuleni wakiwa hawajachoka, nk.

Mimi point yangu ya kwanza ilikuwa kama mwanangu hajawashawishi watoto wao wasipande school bus ila ni wenyewe tu wanataka kumwiga mwanangu je mwanangu anahusikaje

Kiufupi nilianza kutiririka sababu za mimi kuamua mtoto wangu kutopanda school bus ( ghaama ya school bus kwangu sio tatizo kabisa)

1. Afya ya mtoto huimarika kwa kufanya zoezi la kutembea, umbali wa nyumbani hadi shuleni ni dakika kama 20 tu kwa mwendo wa kawaida kabisa, mara chache chache mimi au mke wangu tunampa lifti ya gari tunapoenda kwenye shughuli zetu

2. Kuna mamilioni ya watoto wa shule za msingi hasa za serikali huwa wanatembea kwenda shuleni, shida iko wapi mwanangu kambatana na wenzake kwenye kutembea, kuna shule ipo karibu yao ni ya serikali, wenzake wengi tu huwa wanakutana njiani na hakuna tatizo.

3. Kwa sasa naweza nikawa na uwezo wa kulipia hiyo school bus, ila hali yangu ya kiuchumi ikibadilika mtoto wangu atapata shida.

hizo ndizo zilikuwa sababu zangu, ila zaidi ya hapo, kuna mtoto flani anajiamini sana hana uwoga akaelezea sababu zake

Yeye kwa niaba ya wenzake alisema walikuwa wanapenda wanavyoona mtoto wangu pamoja na wenzake wachache wasiopanda school bus pale wakitoka shuleni, kuna shule karibu sana ya serikali kuna uwanja wa mpira, hapo huwa wakitoka shuleni wanapata nafasi ya kujumuika na wenzao wa hio shule wanacheza na kujumuika na watoto wa shule hio ya kata, si mnajua tena watoto wanavyopenda kucheza.

Lakini pia hapo uwanjani wanapokutana na watoto wengine, mwanangu na rafiki yake aliemzidi darasa moja ambae nae hapandi school bus, walijifunza sarakasi kadhaa na hata mimi nikiri tu kwamba kipaji cha sarakasi cha mwanangu si haba, sasa wakirudi hio shule yao wakianza kuruka ruka hizo sarakasi wenzao wanakusanyika kushangaa, hii nayo ndio ikawa inapelekea nao wengine kugoma

Kiufupi sababu ndizo zilikuwa hizo, lakini licha ya hivyo wazazi waliona watoto wao bado ni wadogo sana waliokuwa wakiongea utoto mwingi n.k kwa hio waliwakataza kabisa watoto zao kurudia tena kuibua upya haya mambo.

Leo nimeandika hii maada baada ya mtoto flani kuwa kiburi na kutaka kufosi nae asiwe anapanda school bus, wazazi wake wanamtandika sana lakini ikifika mida ya kutoka anakwepa school bus ila watoto bwana.

ni hayo tu ndugu zangu
Umenikumbusha mbali sana.

Tulikua tunatembea almost 10km per day
 
Vitu vingine kweli ni kujiendekeza,mi pia mtoto wangu anatembea tu baada ya kubadilishiwa ratiba ya school bus kuwekewa sa 12 kasoro. Saizi anaamka saa 12 na nusu kwa raha zake. Mwanzoni alikua anaona kama hatumpendi ila saizi humwambii kitu anaona school bus miyeyusho maana yeye anafika home nusu saa au lisaa ndio school bus inapita kushusha. Siku mojamoja namsindikiza nikijiskia kumpa kampani tunapiga mastory njia nzima maana kurudi kwangu night kali washalala. Na actually ni kama mwendo wa dakika 15 hadi 20. Vitu vingine tunajiendekeza.
 
mtoto usimpe kila kitu na wala usimnyime kila kitu, hio ndio kauli yangu :)
 
Ndoa yangu itavunjikankwa ajili ya watoto mke hataki watoto watembee shule iko km 1.2 toka home watoto wamenenepa ...mwaka unaisha sasa anawapeleka kwa gari anaogopa salaam geti watatekwa asahi mijasho na wanachoka .....anayetaka mrejesho artichoke January 17 nawatakia mapuNziko mema ya mwisho wa mwaka ....
 
Watatekwaa huyo mkeo ni limbukeni tu
 
Vitu vingine kweli ni kujiendekeza,mi pia mtoto wangu anatembea tu baada ya kubadilishiwa ratiba ya school bus kuwekewa sa 12 kasoro. Saizi anaamka saa 12 na nusu kwa raha zake. Mwanzoni alikua anaona kama hatumpendi ila saizi humwambii kitu anaona school bus miyeyusho maana yeye anafika home nusu saa au lisaa ndio school bus inapita kushusha. Siku mojamoja namsindikiza nikijiskia kumpa kampani tunapiga mastory njia nzima maana kurudi kwangu night kali washalala. Na actually ni kama mwendo wa dakika 15 hadi 20. Vitu vingine tunajiendekeza.
Hata sijui school bus hufananaje. Kule kwetu kijijini hakuna. Maisha yetu ni mguu to and flow. Halafu kwapani kuna daftari zangu na mgongoni nimening'iniza mpira wa kushonwa kwa matambara.

Wakati mwingine tunashindana kuwahi shuleni asubuhi ili mwalimu akutangaze huyu ndiye wa kwanza kutika shuleni kila siku.

Hakuna saa mkononi. Jogoo akiwika unaamka na kunawa chap unalianzisha. Siku moja jogoo kawika saa 6 usiku. Si nikajua muda tayari. Nilitimua mbio hadi shuleni. Niligonga kengele misifa nimewahi. Akaja mwalimu kuniambia niingie darasani nilale kwa kuwa muda bado. Kumbe ni saa 8 usiku.

Hakuna majuto.

Ikitokea hivyo siku hizi, wazazi wataandika kwenye vyombo vyote vya habari hadi youtube.
 
Ndoa yangu itavunjikankwa ajili ya watoto mke hataki watoto watembee shule iko km 1.2 toka home watoto wamenenepa ...mwaka unaisha sasa anawapeleka kwa gari anaogopa salaam geti watatekwa asahi mijasho na wanachoka .....anayetaka mrejesho artichoke January 17 nawatakia mapuNziko mema ya mwisho wa mwaka ....
Mwanamke ana tabia ya kumlinda sana mtoto.

Mkuu tumia nafasi yako hapo kufanya maamuzi.

Kuna mamilioni ya watoto wanatembea kila siku kwenda shule,
 
baba umechomoa betri kwenye mchongo wa watu, school bus ni sehemu ya biashara kwenye hizo shule ndio maana wanaitengenezea mazingira ionekane ni huduma muhimu hata kama mzazi unaweza kumpeleka na kumrudisha shule mwanao kwa wakati
 
Vitu vingine kweli ni kujiendekeza,mi pia mtoto wangu anatembea tu baada ya kubadilishiwa ratiba ya school bus kuwekewa sa 12 kasoro. Saizi anaamka saa 12 na nusu kwa raha zake. Mwanzoni alikua anaona kama hatumpendi ila saizi humwambii kitu anaona school bus miyeyusho maana yeye anafika home nusu saa au lisaa ndio school bus inapita kushusha. Siku mojamoja namsindikiza nikijiskia kumpa kampani tunapiga mastory njia nzima maana kurudi kwangu night kali washalala. Na actually ni kama mwendo wa dakika 15 hadi 20. Vitu vingine tunajiendekeza.
Mastory gani mnapiga na dogo? 🤣🤣
 
Wanawake wapo very insecured na over protective, mbaya zaidi ni kazi sana mwanamke peke yake kumkuza mvulana kuwa mwanaume,

Mi nawaambia watu mwanamke hajui kulea mtoto watu hawanielewi.

Watoto wengi wamefundishwa kuwa waoga waoga,hawajiamini na tabia nyingi za ajabu kwa mama zao kuliko baba zao.

Mwanamke anafanya mambo ambayo yeye anahisi upendo lakini sio upendo ni kumdekeza mtoto.Hata mwanamke akichukia anaongea maneno makali sana kwa mtoto mpk unashangaa.Kama mtoto kakuuzi sana si umchape ukae kimya.

Juzi kati nilikuwa naenda zanzibar sasa kuna mama wa kipemba alikuwa na watoto wawili mmoja ananyonyesha mmoja ndo huyo mda wote anataka kutembeatembea ‘Nikasikia wewe shetani si ukae utulie huoni nanyonyesha’mtoto katulia dakika 2 keshasahau anashuka kwenye kiti anataka kutembea ‘hivi we mbwa una laana au’.Angekuwa ni mwanaume asingeongea hivyo badala yake pale angeweza kutembeza kibao kimoja au viwili.

Sasa madhara ya maneno makali km yale na makofi mawili ni bora makofi mawili.

Pale tu mtoto anapolazimishwa kubehave km mtu mzima shida inaanza hapo.

Wamama kosa lao kubwa ni kumpangia maamuzi mtoto kila wakati kila anachofanya mtoto utasikia ACHA nimesema Acha utaumia yaani toto linakuwa limezubaa tu
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom