Kwanini Serikali isiweke utaratibu wa watoto wa nursery na daycare kuingia saa 3 asubuhi?

Mc2nyi

Senior Member
Nov 5, 2013
190
185
Imekuwa kawaida watoto wa Nursery na Day care shule za English Medium kuingia shuleni saa 1 asubuhi.

Ukiweka umbali wa kuchukuliwa na school bus, wengi huchukuliwa saa 12 kamili na dk chache. Hii umlazimisha mtoto kuamka saa 11 alfajiri.

Kwa nini wizara isiweke utaratibu umri wa watoto wadogo kuingia darasani saa 3 na kutoka hata saa 9, badala ya kuingia saa 1 kama watoto au watu wazima wa chuo.

Afya njema ya mtoto hujengwa kwa kulala muda mrefu zaidi.
 
Una hoja lakini tatizo ni la wazazi, hizi nursery mitaani kwetu Zipo, lakini mzazi nursery ya sh 50,000/= Kwa mwezi hataki mpaka akute nursery million Tatu Kwa Mwaka na pesa ya school bus laki Tatu hapo ndio roho yake inaridhika halafu shule iko kilometres kibao kutoka anapoishi.
 
Imekuwa kawaida watoto wa Nursery na Day care shule za international kuingia shuleni saa 1 asubuh.

Ukiweka umbali wa kuchukuliwa na school bus, wengi huchukuliwa saa 12 kamili na dk chache. Hii umlazimisha mtoto kuamka saa 11 alfajiri.

Kwa nini wizara isiweke utaratibu umri wa watoto wadogo kuingia darasani saa 3 na kutoka hata saa 9, badala ya kuingia saa 1 kama watoto au watu wazima wa chuo.

Afya njema ya mtoto hujengwa kwa kulala muda mrefu zaidi

Mkuu unamaanisha International schools kweli au ulitaka kusema English Medium?
 
Una hoja lakini tatizo ni la wazazi, hizi nursery mitaani kwetu Zipo, lakini mzazi nursery ya sh 50,000/= Kwa mwezi hataki mpaka akute nursery million Tatu Kwa Mwaka na pesa ya school bus laki Tatu hapo ndio roho yake inaridhika halafu shule iko kilometres kibao kutoka anapoishi.

Ukitaka kitu kizuri lazima ugharamie,sasa daycare ya 50k kwa mwezi inatofauti gani na chekechea.
 
Una hoja lakini tatizo ni la wazazi, hizi nursery mitaani kwetu Zipo, lakini mzazi nursery ya sh 50,000/= Kwa mwezi hataki mpaka akute nursery million Tatu Kwa Mwaka na pesa ya school bus laki Tatu hapo ndio roho yake inaridhika halafu shule iko kilometres kibao kutoka anapoishi.
wazazi wa namna hii tumekuwa tukiwaita ni malimbukeni na wapuuzi
 
Una hoja lakini tatizo ni la wazazi, hizi nursery mitaani kwetu Zipo, lakini mzazi nursery ya sh 50,000/= Kwa mwezi hataki mpaka akute nursery million Tatu Kwa Mwaka na pesa ya school bus laki Tatu hapo ndio roho yake inaridhika halafu shule iko kilometres kibao kutoka anapoishi.
I very much doubt kama wewe personally unapeleka au ungeweza kupeleka mtoto kwenye shule ya 50k.
 
Kama alivyosema Dr Matola PhD tatizo kuu ni wazazi, na waathirika ni watoto, sasa kama mzazi haoni shida yeye ndio ana shida zaidi. Option zipo, ila uchaguzi ni wao.
hivi Kwa nini wengi tunaopiga vita hizi shule za English medium or French medium or Chinese medium nk…ni sisi ambao hatuwezi kulipa hizo gharama? Kama mzazi anaweza kuhimili gharama, tatizo lipo wapi?
kila mtu apambane na matatizo yake. Tanzania itakuwa nchi salama.

It is either your business or non of your business. Simple.
 
Suala La Elimu hii nchi kila mmoja anajipigania.. serkali haina muda.
na sijui kwa nini serikali imeacha wananchi wajiamulie gharama za shule wakati ina uwezo wa ku regulate elimu na gharama sawa kwa wananchi wote. Mara shule ya milioni mbili, mara ya laki tano, ya elfu hamsini, mara ya elimu bure. Wazazi mentality yao ni mbovu wanaona kule kwenye gharama kubwa ndio kuna elimu
 
Hizi English medium hamna cha maana kiiivyoo sema bado watanzania wengi vichwani tupo zama za mawe, tunaamini mtoto akijuwa kuongea lugha ya kiingereza ana akili na wazazi wanaona wanapata sifa.Tunaanda taifa sijuwi la namna gani?swala la elimu tulipaswa kuwa na mfumo mmoja wa uendeshaji,haiwezekani mtoto chini ya miaka 5 ukamshindishe shule kuanzia saa 1 asubh hadi kumi na 9 au 10 jioni muda wote huo anajifunza nini kama siyo chaka la shule binafsi kupoteza muda Ii waonekane wanafanya kazi na kuweka adaa juu.Utaratibu wa shule za serikali ni mzuri nadhani watoto wa chekechea wanaingia saa moja na darasa la kwanza wanatoka saa tano au sita mchana wanarudi nyumba huu ndiyo ilitakiwa ufuatwe.Serikali ingeamua kuondoa janga hili kwa kuandaa walimu vizuri na mahiri kwenye lugha ya kiingereza na kuwalipa vizuri wakatumika shule hizi hizi za serikali naamini watoto watakuwa vizuri kwenye lugha hii."ENGLISH MEDIUM KWA SHULE ZOTE ZA SERIKALI BILA SCHOOL BUS NA ADA KUBWA INAWEZEKANA.
 
Imekuwa kawaida watoto wa Nursery na Day care shule za international kuingia shuleni saa 1 asubuh.

Ukiweka umbali wa kuchukuliwa na school bus, wengi huchukuliwa saa 12 kamili na dk chache. Hii umlazimisha mtoto kuamka saa 11 alfajiri.

Kwa nini wizara isiweke utaratibu umri wa watoto wadogo kuingia darasani saa 3 na kutoka hata saa 9, badala ya kuingia saa 1 kama watoto au watu wazima wa chuo.

Afya njema ya mtoto hujengwa kwa kulala muda mrefu zaidi
Serikali au Shule? Hii iko ndani ya uwezo wa shule
 
I very much doubt kama wewe personally unapeleka au ungeweza kupeleka mtoto kwenye shule ya 50k.
Kinachoangaliwa na mzazi sio ada pekee
1. Kuna suala la mazingira, linalohusiana na USAFI, mazingira ya kujifunzia, michezo, vyoo etc
2. Chakula. Mtoto anapaswa kula mara kwa mara kwa makuzi ya mwili na akili. Huko kwenye elfu 50,000 watajistretch vipi wampatie mtoto misosi?
3. Usalama.
Kuna nursery hazina hata mageti. Nyingine hazina usafiri. Nyingine zina usafiri, lakini hazina walimu wa kike wanaosindikiza magari kwa ajili ya pick ups and drop offs.
4. Mitaala. Kuna shule zinasifika kuwajenga watoto kuwa bold na confident, huku mitaala yake ikiwaacha watoto na kitu kichwani. Kuna nyingine mtoto anaenda kukaririshwa ABC. Kuna nyingine mtoto anakwenda tu na kurudi
MZAZI ANAPOCHAGUA SHULE HAANGALII UKARIBU PEKEE
 
Kuna changamoto kubwa sana ya watu kutofautisha kati ya International schools na English medium! Wengi wanasomesha watoto wao English medium wanahisi wapo International schools
tatizo wazazi hawajui mtaala ni kitu gani. Wanadhani shule zinajifundishia mambo yao bila muongozo, wakisikia english medium akili zao zinajengeka kuwa kule ni tofauti na kayumba kumbe masomo ni yaleyale tu kwa mujibu wa mtaala wa ufundishaji, jometri ndiyo jometry, aljebra ndiyo algebra/algebraic, tofauti ni lugha tu ila kukokotoa/calculation ni zilezile
 
Back
Top Bottom