Kama zako zilipoishia kwenye familia ya Mtei. Kwa kudhani kwamba ukipiga sana kelele na bandiko yako mengi kuhusu Mtei you can make people believe kwenye siasa zenu za pwani au Unazani Mtei ni mwislamu wa pwani naye!!?
Utabandika sana mabandiko hapa, kama akili zako fupi zinavyokutuma, na sisi tutaendelea kukubandua tu!!
Kama zako zilipoishia kwenye familia ya Mtei. Kwa kudhani kwamba ukipiga sana kelele na bandiko yako mengi kuhusu Mtei you can make people believe kwenye siasa zenu za pwani au Unazani Mtei ni mwislamu wa pwani naye!!?
Utabandika sana mabandiko hapa, kama akili zako fupi zinavyokutuma, na sisi tutaendelea kukubandua tu!!
Mwasisi huyo mwenye mvuto na heshima kubwa ndani ya Chadema amesema kamwe hawezi kupingana na maamuzi ya Kamati Kuu na kutoa wito chama kuendelea kuwafuatilia na kuwatimua mara moja wasaliti kila wanapobainika.
Ahsante Mzee kwa Busara!! Waondoke si tu kwenye uongozi bali UANACHAMA!! wasiandikiwe nyaraka na TISS ili kutuzuga ovyo wakitutega watukomoe!! NO WAY ZZK you must go to your father JACK ZOKA na JK!!
Ni vema tukajadili uzi husika kuliko kutoa personal attacks,mimi kama junior lawyer sina shaka na uwezo wa ndugu msomi mwenzangu lissu. Lazima tufahamu ya kwamba kila chama kina katiba/sheria na malengo yake kisiasa.
Ni vema tukajadili uzi husika kuliko kutoa personal attacks,mimi kama junior lawyer sina shaka na uwezo wa ndugu msomi mwenzangu lissu. Lazima tufahamu ya kwamba kila chama kina katiba/sheria na malengo yake kisiasa.
Na hilo ndio tatitizo kubwa. Na hata wengi wanaochangia hapa wanashindwa kulielewa, Ni tatizo ambalo wanasiasa dezaini ya ZZK na wengineo kutoka vyama mbalimbali wanaingia katika migogoro na vyama vyao simply kwa kushindwa kulitambua jambo hilo.
Kila chama kina mikakati na malengo yake. Kina Katiba, taratibu na Sheria zake. Pamoja na uwepo wa demokrasia ndani ya chama/ Vyama lakini bado ni muhimu kwa wanasiasa kukumbuka kuwa malengo na "ambitions" ya mwanasiasa haiwezekani ziwe juu (on top) ya malengo makubwa ya Chama. Kwa maneno mengine ikigharimu Chama chako kwa njia yeyote (exploit party efforts) bila kujali athari nyingnezo kwa chama chako.
Leo Chadema ingekuwa na uongozi juu legelege na hovyo hovyo unaorubunika kwa vipande vya fedha kingebakia historia tu kama ilivyokuwa kwa NCCR Mageuzi, TLP au CUF. Lakini uongozi wa juu umekuwa haurubuniki kwa mamlaka za serikali na leo tunaona Chadema imekuwa taasisi imara na upinzani unaotoa mwanga wa matumaini.
Naamini Uongozi wa Chadema utaendela kuwa imara kwa kutompa mtu yeyote asiye makini nafasi yeyote ya juu katika uongozi wa Chama kuepuka balaa.
Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edwin Mtei amesema kuwa chama hicho kitaendelea kuwafukuza wote wanaokihujumu huku akieleza kwamba, anaunga mkono kuvuliwa uongozi kwa Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo.
Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edwin Mtei
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili, nyumbani kwake jana, Mtei aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu (BOT) na Waziri wa Fedha katika utawala wa awamu ya kwanza wa Mwalimu Julius Nyerere, aliweka wazi kuwa daima ataunga mkono dhamira ya kukisimamia chama hicho aliyoitaja kuwa ni safi.
Naunga mkono uamuzi wote wa Kamati Kuu, kuwasimamisha na kuwavua uongozi Naibu Katibu Mkuu wetu Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo. Na kwa sababu Chadema inataka kusonga mbele, lazima iwafukuze mafisadi na wezi wanaoshirikiana kukihujumu chama, alisema Mtei.
Bila kufafanua zaidi au kutaja majina, mwenyekiti huyo wa kwanza wa Chadema alisema: Hatuwezi kuendesha chama wakati viongozi wengine wanapokea pesa na kuzihifadhi kwenye akaunti za siri. Alisisitiza kwamba kwa nafasi yake akiwa mwasisi wa Chadema ni lazima ahakikishe anaunga mkono dhamira safi ya kukisimamia chama.
Kuhusu Arfi kujiuzulu
Akizungumzia hatua ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Saidi Arfi kujiuzulu, Mtei alisema kuwa inafaa kiongozi huyo ajitazame upya na kujisahihisha badala ya kuwa mlalamikaji kila siku.
Aache kulalamika kwa sababu, wakati alipochaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti mimi nilisimamia uchaguzi. Kama alikuwa na ndoto kwamba siku moja atakuwa mwenyekiti wa Chadema taifa alipaswa kujichunguza kwanza, alisema.
Mtei aliongeza kuwa iwapo kuna watu wanadhani Chadema itakufa hiyo ni dhana potovu, lakini kwa sasa chama hicho kimejipanga kuchukua dola na tayari wamejiimarisha kimkakati.
Katika suala la kushughulikia watu wanaokihujumu chama hakuna compromise (mjadala), alihitimisha Mtei. Juzi Chadema ilitangza uamuzi wa Kamati Kuu yake kuwavua uongozi Zitto Kabwe na Dk Kitila, huku Arfi akitangaza kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tanzania Bara.
Mtei amewahi kumkemea na kumwonya Zitto katika mambo mbalimbali aliyofanya ndani ya Chadema, moja ikiwa Oktoba mwaka jana ambapo mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, alipotangaza kuwania urais mwaka 2015.
Alisema kuwa hatua hiyo itasababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama, huku akiongeza kwamba amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana-Chadema na siyo kuwagawa au kuwavuruga.
Hakuna shida kuonyesha hisia, lakini unatengeneza mzozo mkubwa sana ukitangaza sasa. Mimi nimeshamshauri sana Zitto, ahakikishe anakiunganisha chama na siyo kukigawa wala kukivuruga, alisema Mtei.
Mtei alisema hatua ya mbunge huyo kutangaza kutogombea tena ubunge na badala yake kujipanga kuwania urais mwaka 2015, imekuja mapema mno na kuonya kuwa itaibua mzozo ndani ya Chadema, akiweka wazi kuwa wakati ukifika chama hicho kitafanya uchaguzi sahihi.
Siyo vibaya kwa Zitto kuonyesha hisia zake, lakini ndani ya Chadema kwa sasa, kuna watu mbalimbali wanaopenda kuwania urais, lakini hawajatangaza. Dk Slaa (Willbrod) anataka, Freeman (Mbowe) anataka, Zitto anataka, hata mimi huenda nikataka kugombea. Hapa hakuna upendeleo, sifa ndizo zitakazoamua, alisema.
Hata hivyo, Zitto alipinga kauli hiyo akisema: Demokrasia haileti mizozo kwenye vyama vya siasa hata siku moja, bali humaliza mizozo. Udikteta, kuminya fikra huru na mawazo huru, ndivyo huleta mizozo kwenye vyama vya siasa.
Alisema ni muhimu wazee wakawaacha vijana wawe huru kusema wanachofikiri, kwa kuwa uhuru wa fikra na mawazo ni moja ya haki za msingi na moja ya nguzo za demokrasia.
Ninarudia, nitaomba kupeperusha bendera ya chama changu kwenye uchaguzi wa urais mwaka 2015.
Naamini kwamba ninaweza kuwezesha chama chetu kushinda na kuongoza dola na Chadema kutoa rais wakati baadhi ya waasisi wetu wakiwa hai na kuona vijana wao tunavyobadili maisha ya Watanzania na kutimiza ndoto zao, alisema Zitto.
Alisema ana uwezo, uadilifu na uzalendo wa kutosha kuwa Amiri Jeshi Mkuu na kuunganisha Watanzania kuwa wamoja bila kujali rika, dini wala makabila yao... Nimejiandaa kisaikolojia kukabili changamoto za ufukara wa nchi yetu.
kwa jinsi ilivyokuwa kweli siachi mkumbuka...Zenji kuna wakristu.wazenj hawakutaka usawa na hivyo jumla ya nchi nzima haikuwa sawa.NA hata dini km uhindu, za jadi,etc hazikuwa na uwakilishi km dini ya dola.
Haya Zito kesha kataa kuwa haujui huo waraka na ukweli aliwashinda kwa hoja za awali ndio mkakurupuka na waraka na kumhusisha mkidai ni MM mlisahau kuweka C mwanzo ,na kwa kutumia waraka huo ndio mkatimiza lengo lenu ,yule Lissu nilikuwa nikimuona wa maana sana lakini kwa jinsi alivyohukumu amepoteza sifa aliyokuwa nayo ,inawezekana amekubali kutumika au ndio yupo kundi flani ,eti nae wakili !
chama kichanga hiki...wakati hakina majukumu ya kuongoza nchi kinapigana chenyewe na kuonyesha mipasuko ya wazi wazi mapema kabisa je wakikabidhiwa na majukumu mazito na complex ya JMT watafanya nini hawa wapuuzi
Pamoja na hayo yote ni vizuri to solve these differences diplomatically wala sio kuwavua vyeo maana kwa sasa mambo yanavyoonesha ni kama Zitto ana watu ambao ni supporters na wako ndani ya chama.sasa ccm hiyo ndo furaha kwao kumbuka kuna kauli raisi aliwahi kuisema kwamba Zitto ni kijana wake na atamlea kama mtoto wake.but lastly kwani Chadema kuhojiwa kuhusu kupanga....................!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.