Naomba niongezee majibu ya nyongeza kama alivyotanguliza mkuu
Home First kwenye post # 26.
Mkuu
Kisusi Mohammed
1. Kabla ya kufikia hatua hii ya mualiko wa wadau kwenye kikao hiki cha pili...awali kabisa tulianza na wazo la kuwepo kwa 'wing' yetu na bandiko lilikuwepo hapa jamvini, na baada ya wazo hili ndipo tukawa na kikao chetu cha kwanza kabisa kama wing. Mengi tuliyoyajadili, yatabaki kuwa ni haki za members wa wing yetu na si busara kuanika jukwaani kwa kile tulichojadili zaidi ya kukuomba nawe ujumuike katika wing yetu hii nasi kupata mitazamo/maono yako.
2. Zipo ajenda ambazo sisi kama wing tunajadili kuziona kama zitatufaa zaidi, kutudumisha na hata kutunufaisha kama 'wing'. Ajenda hizo hutokana na members wenyewe kushirikishana kwa oppenness zaidi, hatuna wamiliki wa wing ya JF Rock City zaidi ya members wenyewe.
3. Minutes za kikao kilichokwisha zipo, na zitagawiwa tena kwa members kabla ya kuanza kwa kikao cha pili mwishoni mwa wiki hii.
NB:
Ni vema ukatambua kuwa, kwa yote tunayofanya kama wing yatabaki kuwa ni haki za wing yetu. Ku-expose tunayokusudia kufanya kama wing na kuyabandika hapa jukwaani...inaweza kupelekea wings zingine kutekeleza yale tunayoyakusudia kufanya.
Karibu sana JF Rock City wing.