Suala la Mtwara sio kama linavyopotoshwa na viongozi akiwemo JK na waziri wake wa Nishati. Kuna timu ya waandishi wa habari wameletwa leo asubuhi Mtwara na TPDC ,Jerry Muro yupo kwenye hiyo team. Navyosikia wameletwa kutengeneza documentary ili kupaka rangi kinachoendelea Mtwara. Wanataka waihadae dunia kama walivyofanikiwa kuaahadaa watz wachache waliyopo nje ya Mtwara.
Kwa kuwafahamisha kiuchache ni kwamba suala la GAS Mtwara halijaibuliwa na wana Mtwara. Hili suala limeibuliwa na baadhi ya Mawaziri waliovujisha siri za vikao vya siri vya Baraza la Mawaziri, ambapo wamechoshwa na uhuni wa Baba Riz wa kuvutia miradi kwa lazima Bagamoyo.
Baazi ya wazungu wanaofanya kazi kwenye GAS wameshaanza kuvujisha siri kwenye mataifa yao jinsi Mradi wa kujenga Plant ya kusafisha Gas Mtwara ulivyohamishwa kinyemela kupelekwa Mkoa wa Pwani. Baazi ya Wataalamu wa Gas (ngozi nyeupe) wamekiri wazi mradi huu hautakamilika kama serikali itaendelea na ubabe. Ikumbukwe wataalamu hawa wana uzoefu na maeneo kama Angola ,Ivory Cost , Nigeria ambapo pia wamefanya kazi kama hizi na madhara wameyaona pale serikali ilipokaidi matakwa ya wananchi.
Kwenye suala la Gas Mtwara ni Dhahiri hata watumishi wa Serikali Mtwara hawamuungi Mkono JK. Hivyo hujuma kwenye mradi atakapoulizimisha kufanyika kimabavu ipo wazi.
Kilichotokea jana kwa Mbatia ni ishara kuwa hili suala sio la kisiasa kama mwanzo walivyokuwa wanawahadaha Watanzania. Lingekuwa ni suala la kisiasa wangemsitiri Mbatia kwani chama chake kimeshiriki tokea mwanzo.
Sulla la msingi ni Watanzania kuamka kwamba tunahitaji kuwa na majiji mengine zaidi ya Dar, yenye mipango ya kisasa kwa kila kitu.Mtwara ilikuwa ndio moja ya miji ya mifano Africa kwa mpango wa UN Habitat. Hilo limefichwa kwa makusudi kwa sababu ya Ubagamonism, Watanzania tunaonekana ni majuha kwamba mikoani hatana mchango kwa pato la taifa (asilimia 80 ya pato la taifa linatoka Dar) huu ni uvivu wa kufikiri na matusi kwa Wanzania. Watu wanatoa takwimu za kuwahadaha wananchi ili kuhalalisha ubadhilifu wa fedha za uma(Ufisadi).
Nawasilisha.