Mtukufu Rais bora tu angeandika R.I.P

Mtukufu Rais bora tu angeandika R.I.P

Hata akisukumwa haendi kama Dr wa Unguja aligoma kurudi pemba yeye ndiyo atakubali tume yenyewe ya remote
Usiwe na hofu watakao muangusha uncle ni wana ccm wenzake tena na michongo ya kuiba kura ndio watakuwa wanaiongoza wameshamchoka kama tezi dume
 
Hii ni speech ya Hayati JK Nyerere aliyoitoa 1963 USA white house alipoenda kumtembelea rais JF Kennedy.

Nae aliongea kama rais magufuli kuwa on behalf of my self.Hebu iangalieni hiyo video pale nyerere alipoanza kuongea

 
Sidhani kama magufuli anaandika mwenyewe ktk mitandao ya kijamii, kutakua na tatizo ktk timu yake ya mawasiliaono tukianzia kwa Msigwa
 
Hii ni speech ya Hayati JK Nyerere aliyoitoa 1963 USA white house alipoenda kumtembelea rais JF Kennedy.

Nae aliongea kama rais magufuli kuwa on behalf of my self.Hebu iangalieni hiyo video pale nyerere alipoanza kuongea


Hoja yako ni nini?kwa kuwa aliongea Nyerere?
 
hiyo a/c sio ya rais wetu kuna mtu ana tumia hilo jina
 
Magufuli hajui Kiingereza na hilo halina ubishi ila nina wasiwasi kama hii akaunti ya Twitter huwa yeye ndiye mwandishi. Hii itakuwa inaandikwa na Msigwa au mtu mwingine sababu simuoni Magufuli akikaa na kuanza kutupia mambo humo kwa sababu ya wingi wa hekaheka za kazi yake.

Lakini vyovyote vile iwavyo ni kweli kuna ushamba mwingi sana
Sio un'gen'ge tu hata kiswahili chake pia mgogolo kimeathiriwa sana local language .Mahela, Balabala.nk
 
Wao Wanajua kiswahili hata broken?Jibu ni hapana,tatizo sisi tunahangaika na lugha ndio maana wakenya wanajidai wamesoma kwa kujua kiingereza tu hata kama hawana taaluma yoyote.Me sikusoma lakini naomba waliosoma kama kuna mtu anaorodha ya maraisi ambao hawajui hata neno moja la kiingereza awaorodheshe hapa.Wale ambao huwa wanaongea kikwao wanatraslentiwa!Wakati nipo form three nilikuwa nauwezo wa kumkosoa mwalimu wangu wa Geography,alikuwa hajui tenses na muda wa kuzitumia,lakini kitu muhimu alikuwa anatufundisha ili tuelewe Geograhy sio English.Na alikuwa trained teacher.
Sasa kama unajua ni hivo kiherehere cha kuandika kingereza ni cha nn?kwanini asingetumia tu lughahiyo anayoifahamu?ushamba mwingine bwana,kama kingereza haina umuhimu kaandika kwa kingereza kwanini?nijibu upesi PHD uchwara.
 
Hivi kwanini asitumie "editors" wakafanya kazi ya kupost "in his mind"?
 
On behalf of myself and the country,

ni sawa kabisa. What are you complaing of?

Nadhani ingekuwa bora kulalamika kuhusu mantiki ya rais,kuliko kulalamika kuhusu mambo petty.

Kwani yule mtu alipojifunza chemistry,ilikuwa inafundishwa kwa lugha gani?

Ni kama katika BBC utamsikia Alan Kasuja anasema 'fast' badala ya 'first' and such errors. Lakini inaeleweka katika context ilivyotumika.
Acha kutetea ujinga.
 
AIBU HII TUNAIFICHAJE, KWA MFANO???

Kuna ubishi mwingine haufai, lazima tuambizane ukweli.. Wakati wa kumpongeza Rais-mchaguliwa wa marekani, Rais Magufuli aliandika 'broken English' kwenye ukurasa wake wa Twitter kwa nia njema tu ya kupongeza, nikashauri kuwa Ikulu waandaliwe watu wa kuandika kwenye mitandao ya kijamii kwa niaba ya Rais Magufuli, ili yasijirudie tena yale yale, kwasababu ni kuiaibisha taasisi ya Urais, na nchi kwa ujumla.

Kufumba na kufumbua, sijui tatizo ni uelewa au misimamo isiyokuwa na tija, bado 'broken English' imeonekana katika post ya Rais Magufuli alipotoa pole kwa kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Cuba, hayati Fidel Castro.

Wakati ule wa mwanzo kuna watu walisema kwa kumtetea kuwa kiingereza sio 'issue' sana, na kumficha Rais Magufuli kwa mwamvuli wa uzalendo kwamba kiingereza sio lugha yetu.. Lakini niliwaambia, katika moja ya hotuba ya Mwl. Nyerere wakati wa uhai wake aliwahi kusisitiza juu ya matumizi ya lugha ya kiingereza kuwa; kama Ghana wanajifunza, Kenya wanajifunza, Uganda wanajifunza, Mozambique, Malawi, etc. iweje Tanzania tuwe nyuma tusijifunze kiingereza? Mwl. Nyerere akasisitiza kwa kusema kuwa; Kiingereza ndiyo kiswahili cha dunia, ni lazima tukipe mkazo tujifunze na tukitumie, pamoja na kuwa lugha yetu ni kiswahili.

Sasa hili la Rais Magufuli kuandika 'broken English' kwenye ukurasa wake wa Twitter unaosomeka dunia nzima, ni aibu, na mbaya zaidi Rais Magufuli anatambulika kama Dr. Magufuli J.P. kwa maana mtu mwenye shahada zaidi ya moja, na shahafa hizo amezisoma kwa lugha ya kiingereza, na moja wapo ni kwenye chuo kikuu chenye hadhi ya kimataifa, chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM.

Ninashauri tena, Ikulu iandae watu kwa kazi hii, yeye kama Rais awape mawazo yake, wao wajue wanaandikaje, lakini kwa utaratibu huu, kwenye nchi ambayo watoto wa darasa la sita kwenye international schools wanazungumza kiingereza kumzidi mhitimu wa chuo kikuu, ni aibu kubwa, kwa taasisi ya Urais na taifa kwa ujumla.

Wako katika demokrasia na maendeleo
View attachment 440130

Naona hata Nyerere alitumia on behalf of myself - nani bingwa hapo?
 
Wao Wanajua kiswahili hata broken?Jibu ni hapana,tatizo sisi tunahangaika na lugha ndio maana wakenya wanajidai wamesoma kwa kujua kiingereza tu hata kama hawana taaluma yoyote.Me sikusoma lakini naomba waliosoma kama kuna mtu anaorodha ya maraisi ambao hawajui hata neno moja la kiingereza awaorodheshe hapa.Wale ambao huwa wanaongea kikwao wanatraslentiwa!Wakati nipo form three nilikuwa nauwezo wa kumkosoa mwalimu wangu wa Geography,alikuwa hajui tenses na muda wa kuzitumia,lakini kitu muhimu alikuwa anatufundisha ili tuelewe Geograhy sio English.Na alikuwa trained teacher.
So point yako hapo ni nini?
 
Back
Top Bottom