Mtukufu Rais bora tu angeandika R.I.P

Mtukufu Rais bora tu angeandika R.I.P

Naona hata Nyerere alitumia on behalf of myself - nani bingwa hapo?

Ukijipa kazi ama ukikubali kufanya kazi ya kumshambulia Rais wa nchi yako ujue ni sawa na kujipa kazi ama kukubali kazi ya kumshambulia Baba yako Mzazi.
Ndugu zangu JPM ni Rais wetu sote na analiongoza taifa letu. Kwa nafasi yake anaweza kuamua kulivuruga taifa na wote tukaharibikiwa lakini yeye kachagua kutolivuruga.
Kumshambulia Kiongozi wa nchi kwa jambo hili ni utovu wa nidhamu wa kupigiwa mfano na ni kujenga Taifa lisilojitambua. Tukatae utumwa huu na tushikamane pamoja.
Kashikane na Akina Jesca sio sisi hapa.
 
Jamaa ni mmbishi sijapata kuona. Watu wanaogopa kumwambia wasije wakafukuzwa kazi
 
Wao Wanajua kiswahili hata broken?Jibu ni hapana,tatizo sisi tunahangaika na lugha ndio maana wakenya wanajidai wamesoma kwa kujua kiingereza tu hata kama hawana taaluma yoyote.Me sikusoma lakini naomba waliosoma kama kuna mtu anaorodha ya maraisi ambao hawajui hata neno moja la kiingereza awaorodheshe hapa.Wale ambao huwa wanaongea kikwao wanatraslentiwa!Wakati nipo form three nilikuwa nauwezo wa kumkosoa mwalimu wangu wa Geography,alikuwa hajui tenses na muda wa kuzitumia,lakini kitu muhimu alikuwa anatufundisha ili tuelewe Geograhy sio English.Na alikuwa trained teacher.

Hao wasiojua kiingereza pia hawaandiki kwa kiingereza, tafuta tweets za marais wa nchi kama poland, china, German na hata France japo wanafahamu kiingereza mara nyingi wanatumia lugha zao, na wasiojua kabisa pia hutumia lugha zao. Sasa kwanini JPM asitumie tu kiswahili ? kama atazidi kutumia kiingereza huku akikosea itakuwa ni aibu kwa taifa.
 
kujua kiingereza vizuri ni jambo LA msingi Kwa kiongozi yeyote WA nchi.
Mkuu Kama unaona kwenda British Council ni jambo LA aibu basi kajiunge na darasa LA Ras Simba
hana haja ya kwenda uko mbona walimu wapo na wazuri tu? so anamuita hapo anamfundisha hapo alipo? kwan sh, ngapi?
 
Aaa ukizaliwa USA au Uingereza moja kwa moja wewe ni nguli wa Kiingereza..au ukizaliwa Tanzania moja kwa moja wewe ni nguli wa Kiswahili....jibu ni hapana...Pia kumbukeni kuna utofauti kati ya kuandikan.a. kuongea...kuna sentensi unaweza kuitamka katika maandishi ikawa tofauti...Take note
 
AIBU HII TUNAIFICHAJE, KWA MFANO???

Kuna ubishi mwingine haufai, lazima tuambizane ukweli.. Wakati wa kumpongeza Rais-mchaguliwa wa marekani, Rais Magufuli aliandika 'broken English' kwenye ukurasa wake wa Twitter kwa nia njema tu ya kupongeza, nikashauri kuwa Ikulu waandaliwe watu wa kuandika kwenye mitandao ya kijamii kwa niaba ya Rais Magufuli, ili yasijirudie tena yale yale, kwasababu ni kuiaibisha taasisi ya Urais, na nchi kwa ujumla.

Kufumba na kufumbua, sijui tatizo ni uelewa au misimamo isiyokuwa na tija, bado 'broken English' imeonekana katika post ya Rais Magufuli alipotoa pole kwa kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Cuba, hayati Fidel Castro.

Wakati ule wa mwanzo kuna watu walisema kwa kumtetea kuwa kiingereza sio 'issue' sana, na kumficha Rais Magufuli kwa mwamvuli wa uzalendo kwamba kiingereza sio lugha yetu.. Lakini niliwaambia, katika moja ya hotuba ya Mwl. Nyerere wakati wa uhai wake aliwahi kusisitiza juu ya matumizi ya lugha ya kiingereza kuwa; kama Ghana wanajifunza, Kenya wanajifunza, Uganda wanajifunza, Mozambique, Malawi, etc. iweje Tanzania tuwe nyuma tusijifunze kiingereza? Mwl. Nyerere akasisitiza kwa kusema kuwa; Kiingereza ndiyo kiswahili cha dunia, ni lazima tukipe mkazo tujifunze na tukitumie, pamoja na kuwa lugha yetu ni kiswahili.

Sasa hili la Rais Magufuli kuandika 'broken English' kwenye ukurasa wake wa Twitter unaosomeka dunia nzima, ni aibu, na mbaya zaidi Rais Magufuli anatambulika kama Dr. Magufuli J.P. kwa maana mtu mwenye shahada zaidi ya moja, na shahafa hizo amezisoma kwa lugha ya kiingereza, na moja wapo ni kwenye chuo kikuu chenye hadhi ya kimataifa, chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM.

Ninashauri tena, Ikulu iandae watu kwa kazi hii, yeye kama Rais awape mawazo yake, wao wajue wanaandikaje, lakini kwa utaratibu huu, kwenye nchi ambayo watoto wa darasa la sita kwenye international schools wanazungumza kiingereza kumzidi mhitimu wa chuo kikuu, ni aibu kubwa, kwa taasisi ya Urais na taifa kwa ujumla.

Wako katika demokrasia na maendeleo
View attachment 440130

Yaani kurasa lote hill kujadili maneno yaliyo andikwa?

[emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35]
 
Wao Wanajua kiswahili hata broken?Jibu ni hapana,tatizo sisi tunahangaika na lugha ndio maana wakenya wanajidai wamesoma kwa kujua kiingereza tu hata kama hawana taaluma yoyote.Me sikusoma lakini naomba waliosoma kama kuna mtu anaorodha ya maraisi ambao hawajui hata neno moja la kiingereza awaorodheshe hapa.Wale ambao huwa wanaongea kikwao wanatraslentiwa!Wakati nipo form three nilikuwa nauwezo wa kumkosoa mwalimu wangu wa Geography,alikuwa hajui tenses na muda wa kuzitumia,lakini kitu muhimu alikuwa anatufundisha ili tuelewe Geograhy sio English.Na alikuwa trained teacher.
Tatizo siyo kujua au kutojua kiingereza. Nadhani tatizo ni kutumia lugha ambayo huna weledi nayo kwani hujazuiliwa kutumia lugha ambayo una weledi nayo. Tusipoteze muda wa kurejea mifano mingi isiyo na maana.
 
Wao Wanajua kiswahili hata broken?Jibu ni hapana,tatizo sisi tunahangaika na lugha ndio maana wakenya wanajidai wamesoma kwa kujua kiingereza tu hata kama hawana taaluma yoyote.Me sikusoma lakini naomba waliosoma kama kuna mtu anaorodha ya maraisi ambao hawajui hata neno moja la kiingereza awaorodheshe hapa.Wale ambao huwa wanaongea kikwao wanatraslentiwa!Wakati nipo form three nilikuwa nauwezo wa kumkosoa mwalimu wangu wa Geography,alikuwa hajui tenses na muda wa kuzitumia,lakini kitu muhimu alikuwa anatufundisha ili tuelewe Geograhy sio English.Na alikuwa trained teacher.
kama anajijua kuwa hajui si angeandika kiswahili...
 
On behalf of myself grammatically ni makosa Ila hata wazaliwa kwenye Kiingereza wengi tu wanafanya makosa hayo.

Kosa lingine huanzi na wewe, angeanza na on behalf of the people of Tanzania and me.

Mwisho hiyo our deepest ni makosa, ni my deepest.

Msaidieni rais asichapie sana.
 
Back
Top Bottom