uliuuliza hao ambao hawajui neno hata moja la kingereza wanatumia lugha gani katika masomo yao?Wao Wanajua kiswahili hata broken?Jibu ni hapana,tatizo sisi tunahangaika na lugha ndio maana wakenya wanajidai wamesoma kwa kujua kiingereza tu hata kama hawana taaluma yoyote.Me sikusoma lakini naomba waliosoma kama kuna mtu anaorodha ya maraisi ambao hawajui hata neno moja la kiingereza awaorodheshe hapa.Wale ambao huwa wanaongea kikwao wanatraslentiwa!Wakati nipo form three nilikuwa nauwezo wa kumkosoa mwalimu wangu wa Geography,alikuwa hajui tenses na muda wa kuzitumia,lakini kitu muhimu alikuwa anatufundisha ili tuelewe Geograhy sio English.Na alikuwa trained teacher.
Mkuu angekuwa ameshawatumbua, mzee hayuko busy kama unavyofikilia, juzi alivyopiga simu live kwenye mkutano wa makonda nikajiuliza kumbe mheshimiwa naye anafuatilia ziala za makonda live.Magufuli hajui Kiingereza na hilo halina ubishi ila nina wasiwasi kama hii akaunti ya Twitter huwa yeye ndiye mwandishi. Hii itakuwa inaandikwa na Msigwa au pimbi mwingine sababu simuoni Magufuli akikaa na kuanza kutupia mambo humo kwa sababu ya wingi wa hekaheka za kazi yake.
Lakini vyovyote vile iwavyo ni kweli kuna ushamba mwingi sana Ikulu sababu ya kujaza v-i-l-a-z-a.
me nnahamini haya yote ni matunda ya uongozi wa awam ya 4 kwani urais uligeuzwa km ujumbe wa nyumba 10 ndio maana leo watu mnadiliki kumkejeli rais ila wewe uliyepost jua vitu vichache,,ukitoa kuwa rais wako bal pia na mzazi wako,,je babaako hakosei na akikosea unamkosoa mbele za watu?kuwa na heshima kwa viongozi na wakubwa,,hata ajue kiingereza au hasijue,,tulimchagua na tutamchagua kwani anatoa suluhu ya matatizo yetu tena kwa wkt,,,huyo mtu wenu anayejua kiingereza yupo wapi???hacheni watu wafanye kazi!!!AIBU HII TUNAIFICHAJE, KWA MFANO???
Kuna ubishi mwingine haufai, lazima tuambizane ukweli.. Wakati wa kumpongeza Rais-mchaguliwa wa marekani, Rais Magufuli aliandika 'broken English' kwenye ukurasa wake wa Twitter kwa nia njema tu ya kupongeza, nikashauri kuwa Ikulu waandaliwe watu wa kuandika kwenye mitandao ya kijamii kwa niaba ya Rais Magufuli, ili yasijirudie tena yale yale, kwasababu ni kuiaibisha taasisi ya Urais, na nchi kwa ujumla.
Kufumba na kufumbua, sijui tatizo ni uelewa au misimamo isiyokuwa na tija, bado 'broken English' imeonekana katika post ya Rais Magufuli alipotoa pole kwa kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Cuba, hayati Fidel Castro.
Wakati ule wa mwanzo kuna watu walisema kwa kumtetea kuwa kiingereza sio 'issue' sana, na kumficha Rais Magufuli kwa mwamvuli wa uzalendo kwamba kiingereza sio lugha yetu.. Lakini niliwaambia, katika moja ya hotuba ya Mwl. Nyerere wakati wa uhai wake aliwahi kusisitiza juu ya matumizi ya lugha ya kiingereza kuwa; kama Ghana wanajifunza, Kenya wanajifunza, Uganda wanajifunza, Mozambique, Malawi, etc. iweje Tanzania tuwe nyuma tusijifunze kiingereza? Mwl. Nyerere akasisitiza kwa kusema kuwa; Kiingereza ndiyo kiswahili cha dunia, ni lazima tukipe mkazo tujifunze na tukitumie, pamoja na kuwa lugha yetu ni kiswahili.
Sasa hili la Rais Magufuli kuandika 'broken English' kwenye ukurasa wake wa Twitter unaosomeka dunia nzima, ni aibu, na mbaya zaidi Rais Magufuli anatambulika kama Dr. Magufuli J.P. kwa maana mtu mwenye shahada zaidi ya moja, na shahafa hizo amezisoma kwa lugha ya kiingereza, na moja wapo ni kwenye chuo kikuu chenye hadhi ya kimataifa, chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM.
Ninashauri tena, Ikulu iandae watu kwa kazi hii, yeye kama Rais awape mawazo yake, wao wajue wanaandikaje, lakini kwa utaratibu huu, kwenye nchi ambayo watoto wa darasa la sita kwenye international schools wanazungumza kiingereza kumzidi mhitimu wa chuo kikuu, ni aibu kubwa, kwa taasisi ya Urais na taifa kwa ujumla.
Wako katika demokrasia na maendeleo
View attachment 440130
Kama Kingereza ni utumwa bora tuachane nachoHiv kiingereza ndo maendeleo? Hapo angeandika kiswahili tu ingetosha mbona wachina hawajui kiingereza na wanasonga? Wabongo kwa utumwa.
hawajui ! je wanatumia kingereza katika level zote za elimu kama kwetu?Maraisi wote wanajua Kiingereza?
Kwanini analazimishwa kutumia kingereza?Maraisi wote wanajua Kiingereza?