Mtu mweusi leo kujitambua na kutambua historia yake halisi na ya ukweli ni kazi ya ziada

Natty Bongoman

JF-Expert Member
Oct 10, 2008
403
191
Habari zenu wanaJF wenzangu.

Kiujumla watu weusi tumeishi 'gizani' kwa karne nyingi. Tumeishi katika mifumo kadhaa iliyolenga kutupeleka huko 'gizani' na kutubakisha huko. Mifumo hii imepitia marekebisho ya kila aina - tokea mifumo ya kutumia nguvu hadi leo kutumia mifumo ya kutufumba macho na kutufanya tukubaliane na mifumo hiyo kiupofu kabisa, yaani bila kutambua tumekubaliana na mifumo ya kutubakisha gizani na kutukandamiza.

Cha kusikitisha sana ni kwamba Mtu mweusi amekuja kuishi 'gizani' karne za karibuni pale mifumo niliyoitaja hapo juu ilipoingizwa. Mtu mweusi ana historia kali sana kuhusu elimu, uvumbuzi, teknolojia, utabibu nk tena kabla mzungu wa leo kutoka pangoni.

Mababu na bibi zetu walitawaliwa kwa nguvu kwa sababu hawakudanganyika kirahisi. Waliopelekwa utumwani walidhihirisha tulivokuwa tumeelimika, tulivothamini elimu, na tulivokuwa na uchu wa elimu. Elimu waliyoipeleka utumwani iliwatunza na imeboresha dunia hadi kufikia ilipo leo katika nyanja mbali mbali kuanzia kiteknolojia, misosi hadi tamaduni na miziki. Pamoja na kunyimwa elimu utumwani, bado walijielimisha kimtindo.

Kwa juhudi hizi, walielimika na kuelimisha vizazi vyao kuendelea kutambua UHALISIA wa maisha yao. Hapa najihisi nawaona watumwa wakitaabika shambani, wanarudi wamechoka na wakipigwa mijeledi pale wanaposhikwa wamejificha wanasoma vitabu - lakini bado kesho yake atasoma tena.

Nawaona watoto wao walichosoma baadae kuwasomea bibi na babu walionyimwa fursa ya elimu. Kwa juhudi hizi, nawaona watumwa walivokuwa na uzalendo wa maisha yao Afrika na walivolia kila usiku wakitamani kurudi nyumbani Afrika. Najihisi namuona Chifu Mkwawa na wahehe wakitumia elimu na maarifa yao kumpinga Mjerumani wakitambua nia zao... Nawaona waanzilishi wa vita vya Maji Maji wakitumia elimu na maarifa yao kupinga kodi ya Mjerumani na kuunganisha upinzani wa kivita ulioanzia Songea ukatapakaa hadi Njombe hadi Bagamoyo na maeneo katikati.

Tuliingiaje 'gizani'? Wengi tutakubaliana na mfano huu - babu alieshia darasa la nne wakati wa ukoloni ana elimu kali na utambuzi wa dunia fasaha kuliko kijana wa leo alieishia la saba (wengine hata form 4). Naamini babu wakati anasoma alitafakari zaidi kwa sababu alishuhudia maishani mwake vile dini na elimu anayopewa haviandena na uhalisia maishani mwake, na pia alikuwa na elimu ya kijadi kulinganisha na anavofundishwa.

Sisi wasomi wa leo tumepewa ile elimu ya kutuingiza na kutubakisha 'gizani' ambayo lengo kubwa ni kutufundisha 'uhalisia' na kuvunja 'daraja' la elimu ya jadi iliyomfanya mtu mweusi atafakari kama elimu anayolishwa ni uhalisia na inamfaa maishani mwake. Unaetafakari umeshatambua 'uhalisia' haufundishwi, kwa hiyo niaje? Elimu ya leo inatufundisha 'uhalisia' wake - kwa maana inatufundisha eti 'uhalisia' uwe hivi wakati 'uhalisia' ni muonekano wa matukio na sio maneno ya vitabuni.

Nani huyu anaetufundisha 'uhalisia' wake na kuvunja elimu yangu ya jadi? Jibu ni kutambua historia ya mfumo wa elimu tunaopewa leo. Imetoka wapi? Imetoka kwa wazungu na ilienezwa kupitia dini. Hapa Tanzania, shule 'rasmi' za mwanzoni zilikuwa shule za misikiti na makanisa. Katika historia ya maendeleo ya mwanadamu, wazungu ni wa mwisho kutoka mapangoni na kuelimika. Aliipata wapi elimu?

WaAfrika, waArabu, waHindi, wa Asia mashariki (yaani waChina na wenzao) walikuwa na elimu na hata vyuo vikuu wakati mzungu anaibuka toka mapangoni. Walikuja Misri, Timbuktu, Ethiopia na falme nyingine za Afrika zamani kusoma na hata kufanya kazi kama tunavofanya siku hizi kwenda ng'ambo kusoma. Ushahidi, hawatakuambia wazi, unaonekana kwenye picha zilichorwa Misri ya maPharaoh, na hata majengo ya Ugiriki na Urumi walipoanza kujijenga kimaendeleo yaliigwa tokea kule walikosomea.

Tatizo kubwa liliibuka pale mzungu alipoelimika na kutamani kuwa na falme na nguvu zaidi ya kule walikosomea - tabia hadi leo. Mwanzoni walianza kwa kutumia ubabe kuiba vitabu nk na kuchoma moto vyuo na shule sehemu zote walizovamia na kutawala - kisha kusisitiza elimu yao tu ifundishwe. Mfano, fuatilia Alexander the Great alivochoma moto chuo kikuu maarufu duniani kule Alexandria, Misri.

Alipokuja mRumi na utawala wake, nae mwanzoni staili hio hio ila baadae alitumia dini kutoa elimu laghai bado akitumia ubabe pale ubishi ukitokea. Lengo la elimu yake hadi leo ni kumtukuza yeye na kuua elimu tofauti na yake - anatumia elimu kama pia chombo cha kueneza siasa, tabia na malengo yake ili ashikilie utawala wa dunia vizuri. Cha kuonyesha tabia chafu na zaliwa, alisomeshwa Afrika na kwingineko kirafiki na bila ubaguzi... akarudi kututawala kibaguzi na kuua elimu yetu.

Wakoloni hapa Tanzania walikuwa wajerumani na baadae waingereza. Tofauti ya elimu zao ilikuwa lugha na siasa. Hizi elimu zina chanzo kile kile - elimu yao mwanzoni iliyoletwa na wagiriki ikaenezwa na walatini (warumi). Historia fupi ya elimu hii. Mwanzoni, mrumi kila alikotawala - alibomoa elimu, dini na mila alizozikuta kiubabe - choma moto, ua wafuasi nk. Haikuwa siri.

Baadae warumi wakapambana na wakristo na elimu yao pinzani kwa mila zao. Kisha wakajiunga na ukristo na kuanzisha kanisa mama ambalo ndilo limeendesha elimu ya dunia, bado wakilenga kuvunja elimu na mila pinzani kwa kufundisha hadi uongo ili mradi unanyoosha utawala. Mfumo huu wa elimu ndio uliosababisha matengano kutoka kanisa mama.

Warumi ilibidi wakae kikao kutunga njama mpya za kutoa elimu laghai ili watu wasipingane na kanisa lao, mila zao potofu, nk. Hapa ndipo walipoanzisha kundi maalumu JESUITS kwa lengo la elimu potofu ambayo itakuza kanisa na mila zake. Hawa Jesuits ndio walifungua mashule mengi na vyuo vikuu vingi maarufu hadi leo. Hawa Jesuits wamefanikiwa pakubwa sana hapa duniani - leo hii mtoto wa kiTanzania shule ya msingi bado ataamini mganga wa kienyeji aweza mtibu, lakini mtoto huyu huyu akisomeshwa na kupata Phd (udaktari) ndani ya mfumo huu wa elimu - atamdharau mganga wa jadi na kuamini eti ni 'black magic' eti ni upagani ... kama alivofundishwa. Mkristo wa leo anakwambia eti ameruhusiwa kula nguruwe... na nani? na Jesuits na elimu yake, manake Biblia bado inakataza wazi wazi. Je siku ya hukumu utakuwa na haki ya kumlaumu Jesuit wakati sasa na wewe unajua kusoma?

'Gizani leo' - kwa mtu mweusi leo kujitambua na kutambua historia yake halisi na ya ukweli ni kazi ya ziada kwa sababu mfumo wa elimu ya leo hautaki ujitambue - unataka upotelee gizani ili usiibuke... Yaani ni mfumo wa kukandamiza elimu potofu na laghai kwa nguvu zaidi kadri unavopanda madarasa.

Biblia inasema uliumbwa kwa udongo - umeshawahi jiuliza maana yake? Makabila 10 yalipotea Israeli - umewahi jiuliza ama kuamini unaweza kuwa mmoja wapo? Umeshawahi kufundishwa kwa dhati uvumbuzi na mchango wa mtu mweusi ndani ya sayansi na teknolojia tunazotumia leo? Mfano, wangapi wanajua Garret Morgan (mweusi utumwani marekani) ndie mvumbuzi wa traffic lights na vifaa vingi viliboresha usafiri wa reli - ama yule mtumwa Onesmus aliewatambulisha wazungu chanjo ya ndui? Ama mchango mkubwa wa mtu mweusi kwa utabibu tunaojua leo?

Je Umetambua katika maisha ya elimu yako hapa Tanzania - unafundishwa punje kuhusu Mkwawa, Kinjeketile, Mirambo, Mwanamutapa, Mansa Musa, Songhay, Ashanti, Nubia, Meroe, Kush, maPharaoh weusi, nk lakini unafundishwa madebe kuhusu Archimedes, Alexander, Caesar, Isaac Newton nk???

Mwenzangu mtu mweusi - kama unategemea mfumo wa elimu ya leo utakuamsha akili bila wewe kuchimba na kuchambua, basi utabaki gizani - na utakuwa roboti msomi. Kuwa daktari bingwa usiejua historia yako sio kuelimika kamili, ni kuwa roboti. Madaktari wangapi kwa mfano mnajua maana kamili ya hiyo nembo yenu ya utabibu yenye nyoka wawili?

Zamani hakumruhusu babu asome zaidi ya darasa la nne... sasa anaruhusu hata usomee udaktari ila anakupa elimu potofu ya historia yako na uwezo wako. Usimtegemee akuamshe, mishe yake ni kukulaza akutawale na kukunyonya.
 
Back
Top Bottom