Ukoo wangu hakijawahi kutokea mtu kupata nyadhifa ya kisiasa au nafasi ya juu ya kuajiriwa tangia nchi ipate uhuru hadi leo ,mpaka leo tumepata walimu wawili tu,ngazi ya cheti na diploma.
Msiba au kikao ikitokea wanaangaliwa kama watu wenye unafuu ,lakini uhalisia wako vibaya na Wana madeni ya mikopo hayo nilijua baada ya wao kunielezea kama mdogo wao mwenye unafuu kiuelewa kuliko wengine.
Cha ajabu Kila mwana ukoo anataka wawasaidie sana sana kuwasomeshea watoto wao....utasikia "mdogo wg wewe ni mwalimu kabisa nimekuachia mwanangu umsaidie kimasomo"...duh..mara mwalimu naumwa naomba pesa nikatibiwe, mara mwalimu naomba pesa nitatue shida fulani. Shida ya ukoo ni nyingi kuliko mapato yao..
Tatizo hili inawaletea hata shida kwenye familia yao ,utashangaa mtu anapanga safari kwenda Kuwatembelea wanakofanyia kazi na wanaweza kukaa hadi mwezi kisa ndugu yao ni mwalimu na akitoka huyo wengine wanaenda na muda mwingine wanaweza Kuwatembelea hata watatu Kwa pamoja.
Kiuhalisia ukoo wangu tuna ufukara muda mwingine machozi yananitokea nikiona uhalisia ya ukoo wangu,wengine wanakufa sababu ya kukosa tiba ya uhakika ,elimu ni tatizo ,ujinga ,mila potofu, kuamini ushirikina, umaskini ulio kithiri ,ulevi wa gongo ,bangi,ukimwi Kwa kurithi wajane .
Changamoto ni mengi kuliko hata umri wetu, niliamua kutoka nikapambane kivyangu na nilienda mkoa mwingine baada ya kuona Kila nikipigana nijiondoe kwenye huo utiriri wa ufukara narudishwa nyuma pamoja na lawama kibao kutoka Kwa ukoo na familia.
Jamani..jamani...jamani... sipendi familia yangu ije idumbukie kwenye huu umaskini ,unadhalilisha .KWA KWELI UMASKINI NI MBAYA HARUFU YAKE HAISHI IPO LEO KESHO NA KESHOKUTWA.