mke wa mkuu
JF-Expert Member
- Dec 19, 2013
- 634
- 277
Jamani msimlaumu ajali ikifikia haina kinga RIP yaani bongo ni hatari kwanini serikali isipige marufuku hizi boxer
sidhani, nimetoka hapo hata dk 20 hazijaisha.
Huu mtindo wa kushika bahasha za hela waziwazi wakihisi hawahulikani ndio unao waponza wabongo wengi,hata pale posta huwa nawaonaga wengi sana na vibahasha vyao nabaki kunichekea tu...
Mtu hivyo alikuwa anakiita kifo haina hja ya kumuonea huruma...
Kova alishachanganyikiwaga na hizo Boxer hataki hata kuzisikia
Tatizo sio majambazi, serikali imebadilika kuwa jambazi na kuwadhulumu raia wake kwa wizi wa wazi wazi, unategemea nini kutoka kwa hawa wezi wa kuku. Hakuna amani, wananchi wanalipa kodi ili kuona serikali inakuwa na jeshi madhubuti la polisi matokeo yake viongozi wa juu kabisa serikalini wanatumia pesa hizo kwa shopping nchi za nje na kuwaacha walipa kodi solemba. Aibu kuwa na rais dhoofu.
Katiba ni sheria mama. sisi au ccm inaandaa katiba feki. Hilo ni moja Vitambulisho vya taifa ni feki kwani havina taarifa muhimu. Hilo ni pili. Asilimia 99 ya watanzania finger print zao au sura zao haziko kwenye data base yoyote ile duniani. kwa hili tutamkamataje mhalifu hata kama kagusa mahali au cctv ilipiga picha ? CCTV sio solution. first things first. HII KATIBA YA CC TUIPINGE KWA UDI NA UVUMBA BECAUSE WE ARE PLANNING TP FAIL SO THAT UFISADI CAN PREVAIL. CCM IS REALLY SHORT SIGHTED. BY EATING THE PROVIDING HAND
Ni kweli CCTV na taa za barabarani si gharama, lakini je serikali metoa kipaumbele hicho?
Ndio maana kwa wenzetu kuna makampuni na taasisi binafsi ambazo zinashirikana kwenye maeneo kama kutengeneza software na hardware na baadae unakuwa na system inayokuwa ikiangaliwa na watu masaa 24
Sasa kuanzia eneo la Magomeni, Manzese, Ubungo hadi kimara na kupita ha[po, ikifika saa 12 jioni hakuna taa za barabarani zinazosaidia kuona uzuri.
Mimi huku ughaibuni pamoja na mambo mengine najishughulisha na mambo haya yote tunayoyazungumzia, lakini kwa Tanzania kunahitajika mazingira mazuri ili kazi hizi ziweze kufanyika kwa ufanisi mzuri.
Lakini kwa kuanzia ni kwamba kila ofisi, benki, maduka makubwa na maeneo yenye biashara kama la Mlimani City yanahitaji uwekezaji katika CCTV na taa za barabarani.
Nchi yetu imeoza siyo siri, polisi wako busy kuwadhibiti CHADEMA huku ujambazi ukizidi kushamiri sehemu nyingi nchini. Hakuna hata sekta moja nchini ambayo tunaweza kusema hii ina ahueni. Poleni sana wafiwa Mungu awape nguvu na subira katika kipindi hiki kigumu kwenu na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi~AMEN.
Mkuu, kuna madai kuwa eti polisi wanakuwa "well adviced" na hawa maharamia!Yaani ni "deadly brutal combination of two frontiers- the bandits and the police.
This combination is very scary and dangerous.
ni km dili limeanzia ndani vile kuna mtu kawatonya majambazi.
Wewe una matatizo yako, mtu hawezi kuporwa na majambazi useme alikiita kifo. Utakuwa mmoja wa majambazi wewe
Sawa.....!Ningekuwa Jambazi mimi ningekuwa Tajiri mkubwa sana kwa hizi pesa za bure wanazotembea nazo utafikiri wamebeba takeaway
Kwanza sheria inasemaje ukiwana pesa unataka kupelek benki(sijui ni kweli alikuwa anaenda benk Saa tatu hii)?!
Unamlaumu vipi Polisi wakati ulitakiwa uende kituoni kuomba ulinzi na ni bure...kuna haja ya kumuonea huruma mtu aliyeona kuuza roho yake kwenye mfuko wa kaki nfio cha maana kuliko kwenda hata kumuomba msaada askari hata ukimpa 10 thao unapungukiwa nini?
Kumbuka Jambazi haji tu nakuhisi wewe una hela la hasha,huwawanafatilia na wanajua risk ya kuwa na escort ya Polisi kidogo inawapa uoga(ilishawahi nitokea Tazara nikitokea Temeke naenda Bank CRDB Quality Plaza,yule askari nilimpa 50elf japo tulikubaliana 20),ndio maana Majambazi wakiingia sehemu yyt huwawanaanza na wenye uniform kwanza ni standard procedure hiyo...
All in all sina huruma na Wachuuzi wa roho zao kwenye "vifuko vya kaki)...
Braking News as received. Risasi zarindima Mlimani City mminiliki wa burger outlet auwawa !
Kapigwa mbaba mwenye hii sowers sehemu ya baga
Nasikia ameuwawa!
Yaan huyo baba aliepigwa ni ndugu yangu hapa niko msibani.
Ni Shipddda!Bilionea wa mlimani city auwawa
kama hao jamaa walikuwa na boxer basi tena sio rahisi kuwapata hizo cruser haziwexz kupenya
Sawasawa , nimesema hapo juu kwamba vijana siku hizi wanatawaliwa na tamaa ya utajiri wa harakaharaka.
Si wanaona wapambe na marafiki wa viongozi mafisadi au mawakala wao wakitanua mitaani?
Ukiangalia kesi nyingi za wizi wa kwenye mabenki na mauaji ya yule mama mfanyabiashara wa kiasia mwaka jana pale mtaa wa Congo ambae pesa yake alokuwa akipeleka benki ilichukuliwa na ule wizi wa pale Barclays pale Mwananyamala, kuna kila dalili ya "inside job" kufanyika.
Ni kutoa taarifa tu kwamba hesabu leo ni ngapi na kama inakwenda benki au imo ndani.
Sasa ukitaka kutatua tatizo huwa unaanza na kiini cha tatizo na sio matokeo ya tukio.
Polisi wanapenda sana kutoka kwenye TBC kuelezea jinsi tukio lilivyosababisha maafa, lakini kupitia askari kanzu, hawako kwenye maeneo husika yenye mipango ya ujambazi.