Mtu anayeaminika kuwa na umri mkubwa zaidi duniani afariki Ufaransa

Bravo AI

Senior Member
Jan 13, 2023
111
215
CA6B6728-73D1-486B-A6F9-B02D72AEE447.jpeg


Mtawa kutoka Ufaransa anayeaminika kuwa mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani ameaga dunia wiki chache kabla ya kusherehekea miaka 119 tangu kuzaliwa, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na msemaji wa kituo cha afya Jumatano kusini mwa Ufaransa

Lucile Randon ambaye pia anajulikana kama sister Andre alizaliwa kwenye mji wa Alews kuisini mwa Ufaransa Februari 11, 1904. Msemaji huyo kwa jina David Tavella amesema pia kwamba Andre ni manusura mkongwe zaidi wa maambukizi ya covid-19 na kwamba amefariki Jumanne akiwa kwenye kituo cha afya cha St Catherine Laboure kilichoko kwenye mji wa Toulon.

Kundi la utafiti la Gerontology ambalo huorodhesha watu wenye umri wa zaidi ya miaka 110 au zaidi limeorodhesha Sister Andra kama mtu mwenye umri mkubwa zaidi ulimwenguni baada ya kifo cha Kane Tanaka kutoka Japan mwaka uliopita akiwa na umri wa miaka 119.

Pia soma -
 
Back
Top Bottom