Mtu anawezaje kulenga watu saba gizani...

Mtu anawezaje kulenga watu saba gizani...

.....wewe ndio hujamuelewa, mleta mada ana doubt uwezo wa wafanya tukio. Ukimsoma/ukimuelewa zaidi anaona hata tukio lenyewe ni la uongo/kuficha ukweli - 'mtu anawezaje kulenga watu 7 gizani' ...hilo ndo swali lake. Bado hajahoji uwezo wa wafanya tukio !
Kwa uelewa wangu nadhani anashangaa na kujiuliza watu kuwa na ufundi wa kupiga risasi gari bila gari kuwa na matundu ya risasi...risasi iliyovunja kioo na kuwapata wote( professional kiufupi au well trained)...nadhani point kubwa sio majambazi wa kawaida
 
Nina vyombo vingi vya usalama nawashukuru mnao changia positively. Kwa maslai ya opetesheni mpya kwenye haya maeneo sitasema nini kinaendelea.tunahitaji taarifa sahihi kutoka kwa raia wema hili kuleta amani kwa taifa letu. Kumbukeni matamko ya kisiasa hayana nafasi hii ni Vita.
Mkuu tunawatakia kila la heri katika hiyo operesheni, Ila kumbukeni kutenda haki huko mana hamkawii kubeba kila mtu. Tumieni weledi wenu vizuri
 
Kana kwamba risasi hazitowauwa angewapiga kichwani?
WACHENI UONGO
Mimi sikuwepo kwenye tukio ila hizo ni taarifa zilizoko kwenye media mkuu!! Wao ndio wanajua hizo taarifa wamezipata wapi.
 
Ilikuwa sio usiku!! Ilikuwa ni saa 12 jioni kwa mujibu wa polisi! Na baada ya gari kupoteza mwelekeo aliwafuata na kuwavua vest za kuzuia risasi na kuwamalizia kabisa.
mmmh???? kwahiyo yule aliejeruhiwa mkono alikua wapi wakati wenzie wanapewa njugu? hapa umeibua maswali mengi zaidi
 
Bandiwe hii posti hapo juu ndo inaonyesha hujamuelewa mleta hoja. Hata yeye ameshangaa, kwamba precision pia huwa ina determine if those ambushers are well trained or not. Wewe unajibu kwa kumshangaa mleta mada eti kwamba hajui ambushes na ndiyo maana anashangaa uwezo wa hao washambuliaji. Ungemuelewa usinhemshangaa kutokujuwa kwake, Bali na wewe ungejiuliza kama majambazi wa kawaida wanaweza kuwa trained kiasi hicho.
wewe ndo hujamuelewa huyo mbishi,, yeye anamaanisha hata mimi ambae labda kwa mfano sina ujuzi ama mbinu zozote za medani ningewaambush hao aska?ri ningeweza kuwalaza chini wote bila tatizo. kwahiyo kwake kinachowalaza chini wote ni neno "ambush" na sio uwezo wa silaha ama umahiri wa mshambuliaji
 
Kabla hatujakujibu ' Kiundani ' na ' Kiutaalam ' zaidi pitia pitia katika vyanzo vyako vyote vya Kiulinzi na Kiusalama kisha waulize ' Sniper ' au ' Mdunguaji ' kwa Kiswahili chetu ni Mtu wa aina gani, anapata mafunzo gani na kwa kawaida huwa anakuwa wapi Kitaasisi kisha ana uwezo wa kufanya nini ambacho wana ' Medani ' wenzie wengi hawawezi. Ukishapata majibu yake rudi tena kisha ' nitaririka ' zaidi na Wewe ili nikupe ' nondo ' na ' madini ' zaidi yaliyotukuka.
weka misifa pembeni muelezee aelewe kama hizi chara zote za sniping aweza kua nazo "jambazi" wa kawaida? nafikiri ndo msingi wa hoja ya mleta mada
 
Haya mambo kuyaacha yapite tu...
 
Maswali nayo jiuliza mm tukio si lakwanza na wakiuwawa police wanachukua sitaha,sasa hao ni majambazi,magaidi au wakombozi?nahisi kuna jambo hapa kubwa linakuja.unajua hata majambazi yanasikiliza muziki na kufatilia siasa hukute ndo kisasi kufuatia hali iliyopo kwa sasa watu wanahasira.ohoo
 
Hii issue inaweza kuwa ni drama. Cha kwanza picha hazionekani. Report ya tukio haieleweki. Motivation ya tukio mpaka sasa haijulkani.

Wasijekuwa wametafta sababu za kuuwa watu bure kwa kisingizio ya kifo cha polce
Mmhhhh....mkuu hili hata mimi ninaliwaza
 
Embu watutajie majina matatu matatu ya waliouawa ......
 
mkuu napata wasiwasi wa usalama wangu kwa kiasi kikubwa napoona majambazi yanafikia uwezo wa kurecruit mtu kama huyo...


wengine ni retired au waliofukuzwa...kumbuka lile tukio la Mbagala..mmoja aliyekamatwa walisema ni x-soldier
 
Ni wazi huyo aliyemdungua dereva na kumuua kwa risasi moja tu ni bingwa wa udunguaji. Tena labda wengi wenu hamjapita jeshi mkajua namna bunduki ya risasi nyingi inavyofanya kazi. Ukiiweka kwenye automatic fire (kupiga bust) inaachia risasi nyingi sana kwa sekunde chache. Kwa hiyo kama gari imeanguka lakini abiria wako ndani au wengine wako chini ukiizungusha bunduki taratibu risasi zitawapata wote kwa sekunde chache tu. Kwa hiyo wewe unayeshangaa kwamba mtu mmoja atauaje watu wengi kwa sekunde tano unashangaa kwa sababu hujui sub machine gun (smg) inavyofanya kazi.
 
weka misifa pembeni muelezee aelewe kama hizi chara zote za sniping aweza kua nazo "jambazi" wa kawaida? nafikiri ndo msingi wa hoja ya mleta mada

Hata Wewe pia kama unazijua ungeweza tu kumwekea pia na wala kusingeharibika kitu ILA kwakuwa unawashwa na aina yangu kubwa ya ' Uelewa ' na ' Ufahamu ' wa mambo mbalimbali ambayo kimsingi huwa kila siku yanakuchukiza ukaamua kuja na aina yako hii ya response ya ' Kipumbavu ' kabisa Kwangu. Narudia tena kukuambia utaendelea kuichukia 24/7 hii ID ila zawadi ya Kipekee ya kuwa ' Talented and Charismatic ' niliyopewa na Mwenyezi Mungu ' kamwe ' hutoweza kuwa nayo na yawezekana pia hata katika ' Koo ' zako zote mbili hakuna ambaye anathubutu tu kufikia robo yangu.
 
Ni wazi huyo aliyemdungua dereva na kumuua kwa risasi moja tu ni bingwa wa udunguaji. Tena labda wengi wenu hamjapita jeshi mkajua namna bunduki ya risasi nyingi inavyofanya kazi. Ukiiweka kwenye automatic fire (kupiga bust) inaachia risasi nyingi sana kwa sekunde chache. Kwa hiyo kama gari imeanguka lakini abiria wako ndani au wengine wako chini ukiizungusha bunduki taratibu risasi zitawapata wote kwa sekunde chache tu. Kwa hiyo wewe unayeshangaa kwamba mtu mmoja atauaje watu wengi kwa sekunde tano unashangaa kwa sababu hujui sub machine gun (smg) inavyofanya kazi.
Mkuu hayo yote si rahisi kuyafahamu hasa sisi raia wa kawaida.. Tunabaki kushangaa tu... Vp polisi wengine walishindwa kutake cover?
 
Back
Top Bottom