Mtu akishakufa anatoa wapi power ya kufanya matukio?

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,326
5,266
wakuu heshima kwenu.,

Kuna maswali huwa najiuliza sana.
Inakuweje mtu akishakufa anaweza tena kufanya matukio na laana ikafanya kazi?

Mfano kuna jamaa mmoja alikuwa anaishi Canada na alikuwa na uwezo sana sana ila huku Tanzania mzazi wake akawa anamuhitaji kuja kumjulia hali na amletee na wajukuu zake jamaa akawa haji yeye ni kutuma pesa tu na mzazi hakuwa na haja nazo kwani na yeye zilikuwemo .

Mzazi akamtumia ujumbe kuwa ukisikia nimekufa kabla hujuja tutazikwa wote!

Jamaa akaone masihara, akapuuza siku ya siku mzee akafa,jamaa akafunga safari na mke na watoto kuja kuzika kutua kia akapewa gari na rafiki yake,hakufika home ajali,yeye na mtoto wake wakafa ikabidi msiba usogezwe wakazikwa na baba yake.

Mwingine alikuwa anaishi Dar ni tajiri ajabu baba yake kijijini alikuwa mgonjwa na jamaa hakwenda kumuona akawa anatuma tu pesa,mzee akasema kama hauji ukisikia nimekufa HUTANIZIKA,haikupita muda mzee akafa jamaa akaenda na mafaki kuzika kwa mbwebwe na magari ya kifahari.

Wakapewe mwili huko mochwari wakaenda wakazika baada ya mazishi na matanga kuvunjwa wakaja MASAI kudai huo mwili kuwa wakikosea ni wa ndugu yao,kweli kufukua kaburi kitizama ni masai kumbe baba alibaki mochori kimiujiza tu!

Matukio hayo na mingine ni liyowahi kuyasikia ndio inanifanya najiuliza inakuweje mtu akishakufa anakuwa na power ya kutenda matukio?

Niwie radhi nimeandika kwa simu,nimefupisha story
 
Ni swali gumu kwa kweli.....hii mifano kama sio wachaga hao ni bahati....
 
Nafikiri NENO unalolitoa kwa kuumia na kudhamiria (tuseme kwa msisitizo wa uchungu na kumaanisha) huwa lina nguvu. Tunasoma Mungu aliumba dunia na vitu vilivyomo kwa neno.... alitamka tu. Nasi tuna uwezo na tuna siri ya Mungu ndani mwetu... inawezekana ndio maana tukitamka wakati mwingine hutokea. Hivyo nguvu ya NENO lililotamkwa hutenda kazi na si kwamba mtu au roho yake huja kutenda.
 
Pole sana kwa kutatizika na matukio uliyoelezea. Sasa ondoa shaka kabisa, nakupa majibu ya uhakika kabisa kulingana na Biblia:
1. Mtu akifa hawezi kufanya kitu chochote kile, hana uwezo wa kufanya jambo lolote linalofanyika chini ya jua. Swali. Hayo matukio uliyosimulia yaliwezaje kutimia?
2. Shetani ibilisi ni muongo (tapeli) na anaitwa baba ya uongo. Alimdanganya Hawa kwamba hatakufa bali eti kitendo cha kufa ni kubadilika na kufanana na Mungu!
3. Shetani anachezea akili za wanadamu kwa kuwafanya waamini kwamba wakifa hawafi kabisa na wanaweza kutekeleza mambo kadhaa. Matukio uliyosimulia ni baadhi ya mazingaombwe yanayofanywa na shetani ili kutufanya tuendelee kuamini kwamba tukifa hatufi kabisa
4. Mungu alishasema "utakufa hakika". Utarudi kwenye udongo alikokutoa. Roho (yaani nguvu ya uhai iliyo ndani yako) itamrudia yeye aliyekupatia.
5. Ukiujua ukweli utakuwa huru na mbinu mbaya za shetani!
 
Umenikumbusha bibi yangu alikuwa hai akamwambia mdogo wake wa kiume tena anamtaja kwa jina fulani fulani fulani wewe nikifa hutaniona utashuhudia kaburi langu tu wewe endelea kunichezea yani huwa nakumbuka hata position aliyosimama akitamka hayo kweli babu yangu yule alisafiri ghafla tu huku nyuma bibi akafariki kwa kuanguka tu na mdogo wake alifika siku ya tatu baada ya kuzikwa dada yake kweli hapa kuna jambo nakubaliana na wewe lkb pia tujiulize kwa nini mfano mtu anapata matatizo huku duniani na akienda kuzuru makaburi ya wazazi wake au wazee wao kama walitangulia huwa yale matatizo yanaisha? Kuna jambo hapo ila ASIEAMINI MAITI INASIKIA KILA KITU NI MUNAFIKI.
 
Nafikiri NENO unalolitoa kwa kuumia na kudhamiria (tuseme kwa msisitizo wa uchungu na kumaanisha) huwa lina nguvu. Tunasoma Mungu aliumba dunia na vitu vilivyomo kwa neno.... alitamka tu. Nasi tuna uwezo na tuna siri ya Mungu ndani mwetu... inawezekana ndio maana tukitamka wakati mwingine hutokea. Hivyo nguvu ya NENO lililotamkwa hutenda kazi na si kwamba mtu au roho yake huja kutenda.

Kweli dunia ndio hii , ni hadithi ya ajabu sana ila inafundisha
 
hizo story za wafu zipo sana na zinatokea sana kwenye jamii zetu lakini swala la msingi ni kuheshimiana na kumwamini Mungu pekee
 
Umenikumbusha bibi yangu alikuwa hai akamwambia mdogo wake wa kiume tena anamtaja kwa jina fulani fulani fulani wewe nikifa hutaniona utashuhudia kaburi langu tu wewe endelea kunichezea yani huwa nakumbuka hata position aliyosimama akitamka hayo kweli babu yangu yule alisafiri ghafla tu huku nyuma bibi akafariki kwa kuanguka tu na mdogo wake alifika siku ya tatu baada ya kuzikwa dada yake kweli hapa kuna jambo nakubaliana na wewe lkb pia tujiulize kwa nini mfano mtu anapata matatizo huku duniani na akienda kuzuru makaburi ya wazazi wake au wazee wao kama walitangulia huwa yale matatizo yanaisha? Kuna jambo hapo ila ASIEAMINI MAITI INASIKIA KILA KITU NI MUNAFIKI.

hapo kwenye MAITI toa weka ROHO nazani inaweza ku make sense!
 
swali gumu sana hilo, wafia dini watakushushia nondo za hatari ila me nasema heshimu wazazi japo wengine wanazingua sana.
Mkuu mzee anazingua sana nini? halafu unajikuta huna jinsi kwa sababu unaogopa mazingaombwe kama haya.
 
Umenikumbusha bibi yangu alikuwa hai akamwambia mdogo wake wa kiume tena anamtaja kwa jina fulani fulani fulani wewe nikifa hutaniona utashuhudia kaburi langu tu wewe endelea kunichezea yani huwa nakumbuka hata position aliyosimama akitamka hayo kweli babu yangu yule alisafiri ghafla tu huku nyuma bibi akafariki kwa kuanguka tu na mdogo wake alifika siku ya tatu baada ya kuzikwa dada yake kweli hapa kuna jambo nakubaliana na wewe lkb pia tujiulize kwa nini mfano mtu anapata matatizo huku duniani na akienda kuzuru makaburi ya wazazi wake au wazee wao kama walitangulia huwa yale matatizo yanaisha? Kuna jambo hapo ila ASIEAMINI MAITI INASIKIA KILA KITU NI MUNAFIKI.
Sasa hata kama maiti inasikia, inatatua vipi hayo matatizo? Kama kuna ukweli sana kwenye hili la maiti basi ni bora tufe tu wote maana tunakuwa na nguvu zaidi kuliko kubaki hai tukiwa dhaifu dhaifu tu au wewe unasemaje?
 
Mkuu mzee anazingua sana nini? halafu unajikuta huna jinsi kwa sababu unaogopa mazingaombwe kama haya.

ndo ivo mkuu masikio hayazidi kichwa eti mzazi ndo mungu wa dunia wengine vituko mwanzo mwisho na we na vihela vyako unataka kushindana nae mwishowe chali
 
Suala sio kushindana na mzazi. Infact if you think about it, hakuna haja ya kushindana na yeyote kwa misingi ya kuleta ubabe. Ila mimi huwa nasema kuna mahali inafika kama mzazi anashindwa kuwa reasonable inabidi umwambie ukweli. Uungu wa pili wa mzazi unakuja tu pale anapokuwa yuko sawia na Mungu wa kwanza. Sio Mungu wa pili wakati tayari yeye mwenyewe anapingana na utaratibu wa Mungu wa kwanza. Ni sawa na kutii amri ya waziri mkuu inayopingana na amri ya raisi kwa kisingizio kuwa waziri mkuu ni kiongozi wa serikali pia. Hiki kitakuwa kioja.

Mkuu mtii mzazi kwa kuwa ni jambo jema na lenye neema. Usitii kwa woga wa haya mazingaombwe maana yapo tu na ukiendelea hivyo kuna watu wana uwezo wa kufanya haya mazingaombwe licha ya kuwa sio wazazi wako, sasa na wao vipi utawatii tu?
 
upo sahihi mkuu.
 
Back
Top Bottom