Mtoto wa nje ya ndoa

Mtoto wa nje ya ndoa

Usisogeze goal mbele kisingizio kubambikiwa mtoto labda kama hujadhamiria kuoa kutokana na mambo mengine.
Kuna haja ya kuwa mkali(siyo cris brown style) kwa mamaa kuwa kuna DNA na akikubambikia mtoto utapata ukweli ili ajue mumewe moto chini!
Hakuna haja ya kuzini nje wakati umo kifungoni ila mambo yanatokea sana kwenye mazingira tunapoishi!..
7 years sasa kitu kinaahirishwa na siku zinavyokwenda najihisi kuwa huru zaidi nikiwa single namna hii.......ya nini mtoto kzualiwa safari za kwa mkemia mkuu zianze.....kumbuka hapa hatuangalii mtoto tu......kuna kisonono,Gono,Pangusa na Ukimwi....

....swali kwanini atoke nje????? mtoto anaweza kuwa wangu lakini je kama kaukwaa?...... alafu hii masuala eti yanatokea ndio sitaki kusikia..yatokee huko huko lakini sio kwangu.....

....mie niko very simple sana nawapa uhuru sana TGNP....akiona kapata pedejee lingine nampa go ahead.....na imenisaidia sikai na TGNP miezi miaka mi3....tunavunja mkataba....

Make sure unaoa hiyo 2010, eti mwanaJF Yo Yo bwanaharusi mtarajiwa!..I can imagine maana utakuwa unawaza DNA DNA tu! Haitokei kwa kila mtu pia usimcheke mtu kesho yakakukuta halafu uelewe vizuri kashkash za maisha!..
Nilianza 2002 nakumbuka niliona demu wa msela anachemka na watu nikaona woote wako hivyo.....sitaki presha....nikavuta aka 2 nakuta bado wako vile vile tena ndio kama wamechanganyikiwa....ikavutwa mpaka 2008-now naona mauza uza tu nimeweka hapo labda iwe inanikumbusha

.....kisa ya Saleh wa clouds nimeisikiliza imenifanya nife moyo kabisaaaaa
 
Hello,

Nilitoa habari yangu katika forum hii na kupata maoni mbalimbali kutoka kwenu wadau.

Napenda kuwashukuru wote mliochangia na kunishauri, kwa wale walionipa pole asante sana. Ni kama mtu aliyepata ajali vile kwa hiyo nakubali pole zenu na hata wale waliokuwa wakali kidogo.

Kwa sababu fulani sitaweza kuendelea kuchangia katika hii mada. Ila napenda kuwaeleza msimamo wangu baada ya kupata ushauri wenu.

Msimamo wangu hautokani na sababu hizi hapa chini:
-Kujiona mkosa sana;
-Kwa sababu mimi ni mwanamke;
-Nina woga wa maisha ya baadae;
-Ni selfish na sifikirii wengine, nk

Nimeamua kusema hili kwa sababu tu NAMPENDA MUME WANGU na siwezi kuendelea kumdanganya maisha yote, hivyo NITAMUELEZA ukweli. Hata hivyo nitatazama muda muafaka na nitazingatia ushauri wenu mliotoa wa jinsi ya kuendea jambo hili. Nitakapokuwa tayari, hapo tu ndio nitafanya hivyo na nitaheshimu uamuzi wake atakaoutoa. Sitazamii lolote, Mungu atanisaidia.

Siwezi kuahidi kama nitarudi kuwaeleza matokeo kutokana na mazingira, ila nitajaribu kama itawezekana. Nashauri muwe waangalifu katika maisha yenu, hasa katika mambo kama haya.

ASANTENI SANA.

Dada amini usiamini utashangaa jinsi Mungu atakavyokupigania maana msema ukweli ni mpenzi wa Mungu,na katika hili Mungu ataangalia dhamira yako usishangae mume wako akakuonea huruma kuliko ulivyo fikiria maana umesumbuka kwa muda mrefu.
Lakini mimi ningekuomba swala hili liwe lako na mumeo iwe siri ya watu wawili,
hao wazee waheshima kumbuka binadamu tulivyo ukiniona mimi msiri wako kumbuka na mimi nina mtu ambaye ni msiri wangu tena ndo maana wahenga walisema Siri ni ya mtu mmoja/fanyeni hilo wewe na mmeo kwanza nyie ni mwili mmoja maumivu yako ndo maumivu yake japokuwa kwa namna tofauti.
 
Acha kumuingiza mwenyezi Mungu kwenye upuuzi wa namna hio......shetani ndio ana play part hapo...
 
Acha kumuingiza mwenyezi Mungu kwenye upuuzi wa namna hio......shetani ndio ana play part hapo...

YoYo
Wakati shetani ana pray part hapo Mungu alikuwa wapi?.Ukidanganywa na shetani unarudi kwake au una kwenda kwa Mungu kutafuta suruhisho?.Mungu pekee ndo anaweza kuleta suluhisho.
 
7

Nilianza 2002 nakumbuka niliona demu wa msela anachemka na watu nikaona woote wako hivyo.....sitaki presha....nikavuta aka 2 nakuta bado wako vile vile tena ndio kama wamechanganyikiwa....ikavutwa mpaka 2008-now naona mauza uza tu nimeweka hapo labda iwe inanikumbusha.....kisa ya Saleh wa clouds nimeisikiliza imenifanya nife moyo kabisaaaaa

Pole mkuu kwa ushuhuda wa yote hayo lakini kaa ukijua kila ndoa ina matatizo yake japo mengi hufanana kiaina ila haikufanyi usifurahie ndoa yako!..Ila mwisho wa siku mwamuzi ndo wewe,furahi kuishi utakavyo maana tuna nafasi moja kila mwanadamu kuishi hapa duniani!..

Hicho kisa cha Saleh sikijui, nipe hints kidogo nipate mwangaza!..
 
YoYo
Wakati shetani ana pray part hapo Mungu alikuwa wapi?.Ukidanganywa na shetani unarudi kwake au una kwenda kwa Mungu kutafuta suruhisho?.Mungu pekee ndo anaweza kuleta suluhisho.
Sasa Mungu hapo anahusika vipi kwenye uzinifu huo? unajua kwenye dhambi Mungu hayupo yuko Iblisi.....

......nafikiri sasa tuanze kufata sharia.....
 
YoYo kama kungekuwa hakuna kukosa basi kusingekuwa na kutubu, kwahiyo mungu alivyotuumba alijua kuwa tutakosea na ndipo toba ikawepo, hivyo binadamu anapokosea kimbilio lake ni kutubu na kumshirikisha mungu katika toba zake!!

kuhusu kuogopa kuoa kwa mikasa ya watu sio suluhisho, muombe mungu akupe mke mwema nawe uwe mume mwema ni hilo tu, hao wenye watoto na wake za watu pengine ni waume za watu au wanaume kama wewe na pengine miongoni mwao wapo wanawakosoa na kuwahukumu akina maindamainda!!
 
bibi kizee nashukuru kwa vile umeelewa ujumbe niliokuwa najaribu kumweleza yoyo.
 
Maindainda,

Hukupashwa hata kusema jambo hilo humu. Funga mdomo wako bibie. Baki na Mungu wako. Ukifikiri ukweli ni ukweli always, shauri yako hata Yesu aliulizwa 'ukweli ni kitu gani?' Na chamoto alikiona. Akalia sana kwa uchungu. Nakushauri, acha kabisa kuongelea zaidi suala hilo unless umechoka kuishi happily ktk ndoa yako hiyo. DON'T TELL HIM
 
Maindainda

Nadhani wengi wamekushauri accordingly but tunapaswa pia kuangalia mtoto mhusika. What if akijagundua kuwa anaye baba yake mzazi na huyu alonaye si mzazi?. Tutakuwa tuko tayari kumweleza what happened? kumbuka damu ni nzito kulikko maji. Nakuhakikishia kuwa ikitokea akagundua kuwa huyu si baba yake mzazi (pamoja na kuwa amemlea vizuri) itampain sana na inaweza kutengeneza ufa kati yenu (wewe na mtoto)

I am talking from my personal experience. Inauma sana.
 
Maindainda,

Hukupashwa hata kusema jambo hilo humu. Funga mdomo wako bibie. Baki na Mungu wako. Ukifikiri ukweli ni ukweli always, shauri yako hata Yesu aliulizwa 'ukweli ni kitu gani?' Na chamoto alikiona. Akalia sana kwa uchungu. Nakushauri, acha kabisa kuongelea zaidi suala hilo unless umechoka kuishi happily ktk ndoa yako hiyo. DON'T TELL HIM

Nadhani si sahihi kumnyamazisha lengo lake ni kupata mawazo na faraja ya hilo alilonalo, binadamu hukosea, na kuongea lile ulilonalo na kupata ushauri wa watu ni tiba tosha, kwa mawazo anayoyapata hapa na uhakika moyo wake kwa sasa haupo kama ulivyokuwa maana amesikia mengi toka kwawengine wapo wenye matatizo kama hayo, nk. suala la kumwambia au kutokumwambia mumewe hilo ni suala jingine lakini hapa angalau anapata ideas na hili litampa mwanga katika uamuzi wake,

ila kunyamaza ni mbaya mie ninsingemshauri, inaathari kubwa kisaikolojia, kwa maana unabaki na pain ya ndani hiyo ni yako tu, depression and then short life, mara kajinyonga, kanywa sumu, nk.

ushauri wangu, tujifunze kuwa na majibu ya kufariji zaidi, na si kukatisha tamaa, hii inaathiri jamii zetu sana, hata watoto wetu wanapokosea tunawashutumu zaidi inawafanya kuwa inferior na kujihisi wakosaji aidi, pengine hio alilofanya mtoto hata wewe umewahi lifanya...

NO ONE IS PERFECT.....,
 
Unasema ili iweje! Nyamaza kabisa, wengine hatuwezi kukubali eti kusamehe!!! Usaliti wa hali ya juu sana. Hapo hakuna msamaha. WE NYAMAZA YAMESHATENDEKA NA HAYAJAJULIKANA BASI ACHA YAFICHIKE HIVYO HIVYO
 
god eeeh hii mada imenishangaza na imeniuma sana na imeniacha hoi

kwa ushauri wangu moja ulikosea sana kujihusisha na mapenzi nje ya ndoa na hayakuwa salama sikushauri umwambie mmeo kwani hujui ni jinsi gani atalipokea hili ..
pili nini kilikutuma ukamwambie huyo mwanaume wako wa nje una mimba yake ..kosa la pili ambalo hukufikiria ulikuwa unampenda saana au???
Ni mwanzo wa mfurugiko wa ndoa yako na umesema mmeo anakupenda sana utakapoliongea hili kwa mmeo ..ndugu watakapojua itakuwaje ..
jamii inayokuzunguka
dada umeniiacha hoi pole sana na tatizo hili ni tatizo ..mwache mtoto aendelee kutunzwa na huyo babaake anayemjua
 
Mtoto wa Nje ya Ndoa
Maindainda
user_offline.gif
3rd June 2008, 07:07 PM
Vp mpaka leo hii hakurudi kutuambia kipi aliamua? bado tunaendelea kutoa ushauri? au hii ni kwa faida ya wengine?
 
Vp mpaka leo hii hakurudi kutuambia kipi aliamua? bado tunaendelea kutoa ushauri? au hii ni kwa faida ya wengine?

kwa faida ya wengine bwana wasifanye kosa kama la huyu mwanadafada
 
Vp mpaka leo hii hakurudi kutuambia kipi aliamua? bado tunaendelea kutoa ushauri? au hii ni kwa faida ya wengine?

alishatoa uamuzi wake na akasema atasema mwezi unaofuatia, alitoa hiyo post April kwa hiyo inawezekana mumewe tayari amesha jua ukweli....labda tumuombe Mainda aje hapa kutu habarisha hitima ya hii soo
 
Mimi niko tofauti na baadhi ya wengi, ni hivi, Kwa vile huyu baba (Mme wako) hajui na hakuna anayejua zaidi ya wewe tu, ni bora ukanyamaza, maana huyu mme wako anaweza akamwendea huyu baba wa mtoto akamuua, na hatima ya hili tukio ni yeye kunyongwa, na chanzo cha kunyongwa kitakuwa ni wewe,

Hakuna haja ya kusema nyamaza daiiiiiiiiima,

Kuna wengine huwa wanawaeleza watoto wao hii siri kuwa huyu sio baba yako ila baba yako ni mwingine, hii pia ni mbaya sana, itamuathili huyu mtoto kisaikolojia.

Ni hayo, kama kuna swali niulize
 
alishatoa uamuzi wake na akasema atasema mwezi unaofuatia, alitoa hiyo post April kwa hiyo inawezekana mumewe tayari amesha jua ukweli....labda tumuombe Mainda aje hapa kutu habarisha hitima ya hii soo
Huu ni uhamuzi mbaya, na madhara yake ni makubwa kuliko faida, msishangae mkisikia hawa mabwana wawili kwa sasa wanaburuzana mahakamani au wameisha uana,
 
Ndugu na rafiki zangu wa Jamii Forums,

Naomba msaada katika jambo hili.

Nina ndoa ya kama miaka kumi. Nina mume wangu ambae najua ananipenda, nami pia ninampenda. Miaka kadhaa iliyopita nilikutana na jambo ambalo limenitia simanzi sana na sijui hata nifanyeje, kuna wakati siamini kama ni jambo lililonitokea mimi maishani.

Kwa kifupi ni kwamba nina mtoto ambae najua si wa mume wangu! Amelelewa na huyu baba bila kujua kwa upendo mkubwa, kulipa ada za shule na mahitaji yote. Kusema kweli haijakuwa jambo rahisi maana kila anapomuita baba mimi moyo wangu hujaa simanzi. It happenned that I was at a wrong place with a wrong guy and it happenned. Si tabia yangu na wala sikujidhania kwamba siku moja naweza kuisaliti ndoa yangu. .

Huyo baba mwenye mtoto ana mke, simpendi kimapenzi na wala hatuhusiani tena, ikiwa ni pamoja na kuwa hajawahi kumtunza mtoto huyu ingawa anaweza. Sikutaka afanye hivyo. Tatizo ni kuna wakati fulani aliwahi kusema kuwa atakuja kumchukua mtoto wake siku moja, kivipi sijui. Naona ana fujo maana sioni uwezekano wa jambo hili labda avunje ndoa yangu kwanza. Sio kutokana na sababu hii ila kwa muda mrefu tangu nikiwa na mimba ile nimetaka kumwambia mume wangu ukweli lakini nimeshindwa. Maisha ya masikitiko na kuwaza jamani naona nashindwa na nataka nimwambie ukweli na atoe hukumu yake.

Naomba mnishauri hasa wanaume- ingekuwa wewe ungefanyaje? Nimwambie au niache?
Hili ni tukio la kweli, naomba ushauri usiwe katika yafuatayo:
1. Kusema kwamba mimi msaliti na mke mbaya-hilo nalijua na wengi wenu mnayajua haya na haitanisaidia sana.
2. Kusema nimefanya ngono zembe nikapime ukimwi - nimepima na sina

Naomba msaada.

Labda ndio wewe, kesi kama hii ilikuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni. Mama kazaa na Mume wa nje, mume wake hajui anaendelea kutunza, bahati mbaya mwenye mtoto anauwezo kifedha, basi alianza kudai kuwa mtoto wake analelewa katika manzingira magumu hivyo anamtaka ampeleke shule yenye akili. Mama aliomba kwa kugalagala ili aachane na mpango huo ambao ungemvunjia ndoa, lakini njemba ilikomaa, kesi ikapelekwa mahakamani na vipimo kwa ajili ya DNA test vikachukuliwa. Sijui kilichoendelea. Maindainda, nenda kin ondoni kamuona Social worker wa pale Mahakamani ndiye aliyekuwa na kesi hiyo odisini kwake. Niesema hayo baada ya kuona inafanana sana na hayo uliyotuambia
 
Back
Top Bottom