Mtoto wa Lowassa mbaroni kwa kumgonga trafiki

Mtoto wa Lowassa mbaroni kwa kumgonga trafiki

mchakachuaji

Member
Joined
Aug 12, 2010
Posts
58
Reaction score
7
Na Masau Bwire,jijini

MTOTO wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa, Bernald Lowasa (30), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kituo cha Oysterbay, Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kumgonga kwa makusudi askari wa kikosi cha usalama barabarani E 9320 Koplo Cyprian akiwa katika kutekeleza majukumu ya kazi yake.

Tukio hilo lililolaaniwa na watu wengi waliolishuhudia na kuhoji sababu za mtoto huyo wa waziri mkuu mstaafu Lowasa kufanya hivyo, wengine wakienda mbali zaidi wakidai pengine alifanya hivyo kwa kujiona hawezi kubanwa na sheria kwakuwa ni mtoto wa kigogo, lilitokea jana saa 1 jioni eneo la Namanga, Oysterbay katika eneo la taa za kuongoza magari.

Akiendesha gari lenye namba za usajili T 573 BQV, Corona Primio, akitokea Msasani kwenda Morocco, mtoto huyo wa Lowasa alikaidi utaratibu wa trafiki huyo wa kuruhusu magari kupita kwa awamu hivyo kulazimisha kupita kabla hajaruhusiwa.

Koplo Cyprian pengine kwa lengo la kuepusha magari kugongana na kutaka kuchukua hatua kwa dereva huyo mkaidi Bernald, alilazimika kumzuia asipite lakini, kwa dharau na bila kujali wala woga, mtoto huyo wa kigogo aliendesha gari lake na kumgonga mguu trafiki huyo na kisha kumsukuma kwa gari.

Baada ya trafiki huyo aliling'ang'ania gari hilo hadi madereva wengine walipomuokoa kwa kulizuia gari lake kwa kusimamamisha magari yao mbele ya gari lake.

Baada ya madereva wengine ambao nao walikuwa wakisubiri kuruhusiwa na trafiki huyo kupita katika taa hizo walikerwa na kitendo alichokifanya kijana huyo kumgonga askari kwa makusudi waliamua kumuokoa trafiki huyo waliyeona anaonewa, nusura waanze kumshushia kisago mtoto huyo wa Lowasa lakini, askari huyo kwa moyo wa huruma na upendo mkuu aliwasihi wasifanye hivyo badala yake waiachie sheria ichukue mkondo wake.

Madereva hao walitii kauli ya askari huyo aliyekuwa akichechemea na kulia kwa uchungu na maumivu makali ya mguu na kumchukua kijana huyo hadi kituo cha polisi Oysterbay kwa hatua za kisheria.

Kamanda wa Jeshi la polisi, Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Koplo Cyprian alipelekwa hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya matibabu.

Kamanda Kenyela alionesha kusikitishwa na kitendo hicho cha mtu kudhani yupo juu ya sheria na kuamua kuvunja sheria za nchi kwa makusudi na kujaribu kutaka kutoa roho ya binadamu mwenzake kwa makusudi bila kujali athari katika familia inayomtegemea.

"Nimesikitishwa sana na kitendo hicho, mtu anaamua tu kutokufuata sheria za barabarani na kudharau kazi ya askari katika kutekeleza majukumu yao, kijana huyo wa mheshimiwa waziri mkuu mstaafu amekamatwa na anahojiwa na polisi, tuiachie sheria ichukue mkondo wake na kuamua cha kufanya kuhusu kitendo hicho cha uvunjifu wa sheria kilichofanywa na kijana huyo wa Lowasa," alisema Kamanda Kenyela.


Source: Dar Leo

My take:
Sasa huyu mtoto baba yake ni Waziri Mkuu aliyeachia ngazi (sio mstaafu) kwa tuhuma za richmond sasa akipata huo urais anaoutaka si wataleta mambo ya Ditopile.
 
authenticity of the news ..... photos please
 
wanajifanya nchi y a kwao hii njoja tuingie madarakani ss cdm watakiona
 
maksudically?

can you report a serious incident with its seriousness? this ain't Facebook for phuck sake! unazidi kuididimiza siku yangu
 
Katika hali ya kuonyesha sisi ndio wenye nchi hii na ulevi wa madaraka kama mtoto wa gadafi mtoto wa lowasa ameripotiwa kushikiliwa katika kituo cha polisi oysterbay baada ya kumgonga kwa maksudi trafic.

Kwa makusudi? kweli makusudi?
 
Katika hali ya kuonyesha sisi ndio wenye nchi hii na ulevi wa madaraka kama mtoto wa gadafi mtoto wa lowasa ameripotiwa kushikiliwa katika kituo cha polisi oysterbay baada ya kumgonga kwa maksudi trafic.

Watamfanya nini? Chenge aliua faini yake chini ya milioni itakuwa huyu traffic officer ambaye hakutaka kupisha gari? Labda utokee mujiza. Kule Arusha si polisi waliua raia wasio na hatia pamoja na kuwapiga wananchi. Hii nchi ina wenyewe nyie wengine mmesingiziwa tu.
 
Mmeishafanya uchunguzi kujua chanzo cha ajari ilikuaje au mnaimba taarabu 2 humu ilimradi kuziba pengo la walio2toka.
 
ndugu mtoa mada heshima mbele!je unaweza kudhibitisha kwamba alimgonga makusudi?kama hauna ushahidi nakushauri uache unafiki,umbea na uchonganishi!leta uzi wenye mashiko na si umbea na chuki binafsi
 
Tatizo ni uletwaji wa mada kwenye jukwaa. Kwanza ilibidi ianzie kwenye hayo majukwaa ya wakina nanii kwa jinsi ilivyoletwa. Alafu iweje ye ndo'addmit moja kwa moja ya kuwa "kakonga makusudi" pasipo uchunguzi wa kina. C kwamba natetea ila huwa 2napenda mambo ya kukurupuka na kuhukumu papo hapo pacpo uthibitisho wa kina, 2kumbuke na ye ni mvuta pumzi ka viumbe wengine.
 
kwamba kagonga hilo halina ubishi!tatizo anaposema MAKUSUDI!!
 
ndugu mtoa mada heshima mbele!je unaweza kudhibitisha kwamba alimgonga makusudi?kama hauna ushahidi nakushauri uache unafiki,umbea na uchonganishi!leta uzi wenye mashiko na si umbea na chuki binafsi

Hapo kwenye red alimaanisha kudhibiti au kuthibitisha? Kwanini watu wengi wana tatizo la matumizi ya maneno KUTHIBITISHA na KUDHIBITISHA? Hata hivyo tumeelewa ujumbe wake!
 
Watamfanya nini? Chenge aliua faini yake chini ya milioni itakuwa huyu traffic officer ambaye hakutaka kupisha gari? Labda utokee mujiza. Kule Arusha si polisi waliua raia wasio na hatia pamoja na kuwapiga wananchi. Hii nchi ina wenyewe nyie wengine mmesingiziwa tu.


Acha majungu, madereva wangapi huko safarini wana ua abiria na wana kimbia still hawakamtwi na wana dunda mitaani , hakuna kesi wala nini, sembese huyu chenge kalipishwa fain. Niambie kesi ngapi za hawa madereva wazembe wa mabasi ya mikoani yanao ua watu wengi kwa mpigo , halafu dereva kafungwa.
 
'citizen grade a' sheria zinazowahukumu ni tofauti na zetu, ngoja tusubiri tuone,
 
Back
Top Bottom