Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,357
- 18,632
Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani, Conrad Kahyoza ameachiwa kwa dhamana baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kusomewa shtaka moja la kushambulia mwili.
Kahyoza anadaiwa kumshambulia askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, F.8886 SGT Andrew, Septemba 8, 2026, majira ya saa 1:30 asubuhi katika Barabara ya Bagamoyo, eneo la Makongo, wakati askari huyo akiwa akitekeleza majukumu yake.
Soma: Daktari Bingwa wa Mloganzila, Conrad Agonza, anayedaiwa kumshambulia Trafiki afikishwa Mahakamani, 10/09/2026
Akisoma hati ya mashtaka, Leo Septemba 102026 mwendesha mashtaka wa Serikali, Irene John, amesema mtuhumiwa huyo anashtakiwa kwa mujibu wa kifungu cha 243(d) cha Sheria ya Makosa ya Jinai, Sura ya 16, kama kilivyofanyiwa marekebisho.
Baada ya kusomewa shtaka hilo na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Jacqueline Rugemalila, Dk Kahyoza alikana kutenda kosa hilo.