Katika hali ya kuonyesha sisi ndio wenye nchi hii na ulevi wa madaraka kama mtoto wa gadafi mtoto wa lowasa ameripotiwa kushikiliwa katika kituo cha polisi oysterbay baada ya kumgonga kwa maksudi trafic.
Jamani muwe na uhakika na habari mnazo zitoa humu!
1. Aliyehusika na tukio hilo sio Mtoto wa Lowasa ni ndugu yake
2. Siku ya tukio kulikuwa na ajali mbili ambapo gari moja lililokuwa linatanua
pembeni baada ya kutaka kukamatwa na askari dereva aliliondoa kwa nguvu kitu
kilichomsababishia maumivu askari huyo (watu wengi walijichanganya na tukio
la pili ambalo askari Polisi inadaiwa alisukumwa na gari la mtu anayehusishwa
na undugu wa Lowasa.
3. Askari huyu hakugongwa bali gari lilimkaribia karibu kabisa ndiyo maana
aliendelea na kazi yake (haya ni maelezo ambayo kamanda huyo aliyasema
jana na kuwataka watu kutozusha habari ambazo hawana uhakika nazo.)
4. Kwamba kosa lililofanyika lilikuwa la kawaida ambalo lingefanywa na mtu
yeyote. Haya ndiyo niliyosikia kutoka kwa kamanda huyu na kukiri wazi kuwa
dereva huyo mwenye undugu na Lowasa aliachiwa muda mfupi baada ya
kufikishwa kituoni. sasa hizi habari za kushikiliwa mpaka sasa mmezipata wapi?
hebu tujuzeni kama kuna mwenye maelezo tofauti na haya niliyosikia kutoka
kwa kamanda wa Polisi kupitia kituo kimoja cha radio.