Mtoto wa Lowassa mbaroni kwa kumgonga trafiki

Mtoto wa Lowassa mbaroni kwa kumgonga trafiki

Msipige debe sana hiyo ni traffic case kutokana na sheria zetu fain ni shilling elfu 10,000/=,msichukulie kua ni mtaji.Hiyo kugonga kwa makusudi ni lazima muweze kuProof beyond A Reasonable Doubt ambayo ni ngumu.

Inaonekana uko karibu nao kabisa! Endeleeni tu.
 
Nimeshawishika kuchangia hapa kwani hata mimi ni muhanga.

Nomba nisimhukumu huyu dereva moja kwa moja kwani mie nilikutwa na mkasa kwenye taa za ubungo nikiwa nakata kuelekea Kimara Trafiki akalazimisha nielekee Buguruni kwa kuwa tu nilikuwa lane ya kati yaani the next kutoka ile inayokata kwenda Kimara, kitu ambacho ni cha kawaida kabisa. Nilivyomkatalia akaamua kulala juu ya Boneti na kudai nimengonga, ilikuwa kama picha, nikashuka nikasimama naye akawa juu ya boneti namstaajabu. Wakaja wenzie walio kuwa pembeni.

Mmoja ambaye ndiye incharge alikuwa akiiona ile picha toka awali akanipeleka kituoni Ubungo akasema hata yeye ameona jamaa hakunitendea haki hivyo akawa ananiandikia nile niendelee na safari. Heeee kumbe simu ishapigwa mpaka kwa mkuu wa trafiki mkoa ikatoka amri niwekwe lupango kwa kosa la kumgonga jamaa na jamaa akawa anachechemea eti kaumia, aibu jamani. Nashukuru nilikuwa najua nini cha kufanya sikuwekwa ndani baadae waliniomba msamaha nikaendelea na safari yangu. Hivyo wakati mwingine hawa jamaa zetu wanakuwa wamechoka wanatafuta sababu na wakifika kituoni wanapata nguvu hao za maneno ya kushadadia wewe acha tu.

Naomba nisiwe wakwanza kurusha jiwe kwani sijui mazingira ya ajali yenyewe
 
Na Masau Bwire

MTOTO wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Bw. Bernard Lowassa (30), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Oysterbay, Kinondoni, Dar es Salaam kwa tuhuma za
kumgonga kwa makusudi askari wa Kikosi cha Usalama barabarani E 9320 Koplo Cyprian akiwa katika kutekeleza majukumu ya kazi.

Watu walioshuhudua tukio hilo waliaalaani na kuhoji sababu za mtoto huyo kufanya hivyo, wengine wakienda mbali zaidi wakidai pengine alifanya hivyo kwa kujiona hawezi kubanwa na sheria kwa kuwa ni mtoto wa kigogo.

Tuko hilo lilitokea juzi saa 1 jioni eneo la Namanga, Oysterbay katika eneo la taa za kuongoza magari. Akiendesha gari lenye namba za usajili T 573 BQV, Corona Primio, kutoka Msasani kwenda Morocco, alikaidi utaratibu wa trafiki huyo wa kuruhusu magari kupita kwa awamu kwa kulazimisha kupita kabla hajaruhusiwa.

Koplo Cyprian pengine kwa lengo la kuepusha magari kugongana na kutaka kuchukua hatua ukaidi wa Bernard, alilazimika kumzuia asipite lakini, bila kujali wala woga, aliendesha gari lake na kumgonga katika mguu na kumsukuma.

Mshuhuda walioshuhudia tukio hilo walisema askari huyo aling'ang'ania gari hilo hadi madereva wengine walipomuokoa kwa kulizuia gari la kijana huyo baada ya kusimama mbele ya gari lake.

Baada ya madereva wengine ambao nao walikuwa wakisubiri kuruhusiwa kupita katika taa hizo kukerwa na kitendo alichokifanya Bernard kumugonga kwa makusudi.

Watu wakiwa na hasira nusura wamshushie kipigo mtoto huyo lakini, askari huyo liwasihi wasifanye hivyo bali waiache sheria ichukue mkondo wake.

Madereva hao walitii kauli ya askari huyo aliyekuwa akichechemea na kulia kwa uchungu kutokana na maumivu makali kutoka katika mguu

Polisi wa kituo hicho walifika katika eneo hilo na kumchukua mzobemzobe mtoto huyo hadi Kituo cha Polisi Oysterbay, na habari zaidi zinasema baadaye aliachiwa kwa dhamana kwa sharti la kutakiwa kuripoti kituoni leo.

Kamanda wa Jeshi la polisi, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Bw. Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba koplo Cyprian alipelekwa Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu.

Kamanda Kenyela alionesha kusikitishwa na kitendo hicho cha mtu kudhani kuwa yuko juu ya sheria. "Nimesikitishwa na kitendo hicho, mtu anaamua kutokufuata sheria za barabarani na kudharau kazi ya askari wakati wa kutekeleza majukumu yao.

"Kijana huyo amekamatwa na anahojiwa na polisi, tuiachie sheria ichukue mkondo wake na kuamua cha kufanya kuhusu kitendo hicho cha uvunjifu wa sheria kilichofanywa na kijana huyo wa Lowassa," alisema Kamanda Kenyela.

Askari wa vyeo vya chini wameonesha wasiwasi kuhusu hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi ya mtoto huyo wa kigogo wakidai, kumekuwa na kawaida ya vigogo kulindana na kupoteza haki ya mtu
wa hali ya chini.

Mmoja ya askari ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini alisema kwamba ana uhakika kuwa mtoto huyo atalindwa, hatafanywa chochote, zaidi kulazimishwa askari huyo kumsamehe


Chanzo majira, march 31 2011
 
"...Chanzo majira, march 31 2011..."

wacha bangi wewe
 
Sheria na iachwe ichukue mkondo wake

Ajali za barabarani hazizuiliki, lakini kama ikigundulika ni makusudi basi na apelkwe jela ili iwe fundisho
 
Wagongwe tu! Kazi yao kukusanya rushwa tu barabarani hata sioni umhimu wao!
Watuwekee CCTV CAMERA
 
Sheria na iachwe ichukue mkondo wake

Ajali za barabarani hazizuiliki, lakini kama ikigundulika ni makusudi basi na apelkwe jela ili iwe fundisho

Kweli wewe kapuku na msukule,hiyo habari ni ya Mwaka 2011. Na Ukawa ikiingia Ikulu jiandae kutafuta utapeli mwingine wa kufanya maana huo ulaghai unaowafanyia Watanzania kwa kushirikiana na CCM kukagua magari utafika kikomo.
 
saa bado masaa tuuu... mtoa maada pua zakoo. kichwa kaa nazii
 
Back
Top Bottom