Nani kaileta leo?Yaani mijitu mingine humu kama matrafic hata gari ikiwa mpya wataiandama kutafuta kosa la kupachika. Kesi ya makosa ya (trafic case) 2011 unaleta leo 2015 ?
Jamani muwe na uhakika na habari mnazo zitoa humu!
1. Aliyehusika na tukio hilo sio Mtoto wa Lowasa ni ndugu yake
2. Siku ya tukio kulikuwa na ajali mbili ambapo gari moja lililokuwa linatanua
pembeni baada ya kutaka kukamatwa na askari dereva aliliondoa kwa nguvu kitu
kilichomsababishia maumivu askari huyo (watu wengi walijichanganya na tukio
la pili ambalo askari Polisi inadaiwa alisukumwa na gari la mtu anayehusishwa
na undugu wa Lowasa.
3. Askari huyu hakugongwa bali gari lilimkaribia karibu kabisa ndiyo maana
aliendelea na kazi yake (haya ni maelezo ambayo kamanda huyo aliyasema
jana na kuwataka watu kutozusha habari ambazo hawana uhakika nazo.)
4. Kwamba kosa lililofanyika lilikuwa la kawaida ambalo lingefanywa na mtu
yeyote. Haya ndiyo niliyosikia kutoka kwa kamanda huyu na kukiri wazi kuwa
dereva huyo mwenye undugu na Lowasa aliachiwa muda mfupi baada ya
kufikishwa kituoni. sasa hizi habari za kushikiliwa mpaka sasa mmezipata wapi?
hebu tujuzeni kama kuna mwenye maelezo tofauti na haya niliyosikia kutoka
kwa kamanda wa Polisi kupitia kituo kimoja cha radio.
Na Masau Bwire,jijini
MTOTO wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa, Bernald Lowasa (30), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kituo cha Oysterbay, Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kumgonga kwa makusudi askari wa kikosi cha usalama barabarani E 9320 Koplo Cyprian akiwa katika kutekeleza majukumu ya kazi yake.
Tukio hilo lililolaaniwa na watu wengi waliolishuhudia na kuhoji sababu za mtoto huyo wa waziri mkuu mstaafu Lowasa kufanya hivyo, wengine wakienda mbali zaidi wakidai pengine alifanya hivyo kwa kujiona hawezi kubanwa na sheria kwakuwa ni mtoto wa kigogo, lilitokea jana saa 1 jioni eneo la Namanga, Oysterbay katika eneo la taa za kuongoza magari.
Akiendesha gari lenye namba za usajili T 573 BQV, Corona Primio, akitokea Msasani kwenda Morocco, mtoto huyo wa Lowasa alikaidi utaratibu wa trafiki huyo wa kuruhusu magari kupita kwa awamu hivyo kulazimisha kupita kabla hajaruhusiwa.
Koplo Cyprian pengine kwa lengo la kuepusha magari kugongana na kutaka kuchukua hatua kwa dereva huyo mkaidi Bernald, alilazimika kumzuia asipite lakini, kwa dharau na bila kujali wala woga, mtoto huyo wa kigogo aliendesha gari lake na kumgonga mguu trafiki huyo na kisha kumsukuma kwa gari.
Baada ya trafiki huyo aliling'ang'ania gari hilo hadi madereva wengine walipomuokoa kwa kulizuia gari lake kwa kusimamamisha magari yao mbele ya gari lake.
Baada ya madereva wengine ambao nao walikuwa wakisubiri kuruhusiwa na trafiki huyo kupita katika taa hizo walikerwa na kitendo alichokifanya kijana huyo kumgonga askari kwa makusudi waliamua kumuokoa trafiki huyo waliyeona anaonewa, nusura waanze kumshushia kisago mtoto huyo wa Lowasa lakini, askari huyo kwa moyo wa huruma na upendo mkuu aliwasihi wasifanye hivyo badala yake waiachie sheria ichukue mkondo wake.
Madereva hao walitii kauli ya askari huyo aliyekuwa akichechemea na kulia kwa uchungu na maumivu makali ya mguu na kumchukua kijana huyo hadi kituo cha polisi Oysterbay kwa hatua za kisheria.
Kamanda wa Jeshi la polisi, Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Koplo Cyprian alipelekwa hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya matibabu.
Kamanda Kenyela alionesha kusikitishwa na kitendo hicho cha mtu kudhani yupo juu ya sheria na kuamua kuvunja sheria za nchi kwa makusudi na kujaribu kutaka kutoa roho ya binadamu mwenzake kwa makusudi bila kujali athari katika familia inayomtegemea.
"Nimesikitishwa sana na kitendo hicho, mtu anaamua tu kutokufuata sheria za barabarani na kudharau kazi ya askari katika kutekeleza majukumu yao, kijana huyo wa mheshimiwa waziri mkuu mstaafu amekamatwa na anahojiwa na polisi, tuiachie sheria ichukue mkondo wake na kuamua cha kufanya kuhusu kitendo hicho cha uvunjifu wa sheria kilichofanywa na kijana huyo wa Lowasa," alisema Kamanda Kenyela.
Source: Dar Leo
My take:
Sasa huyu mtoto baba yake ni Waziri Mkuu aliyeachia ngazi (sio mstaafu) kwa tuhuma za richmond sasa akipata huo urais anaoutaka si wataleta mambo ya Ditopile.
Mtoto wa Lowassa mbaroni kwa kumgonga trafiki
Na Masau Bwire
MTOTO wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Bw. Bernard Lowassa (30), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Oysterbay, Kinondoni, Dar es Salaam kwa Ty za
kumgonga kwa makusudi askari wa Kikosi cha Ty barabarani E 9320 Koplo Cyprian akiwa ttykatika kutekeleza majukumu ya kazi.
Watu walioshuhudua tukio hilo waliaalaani na kuhoji sababu za mtoto huyo kufanya hivyo, wengine wakienda mbali zaidi wakidai pengine yalifanya hivyo kwa kujiona hawezi kubanwa na sheria kwa kuwa ni mtoto
wa kigogo.
Tuko hilo lilitokea juzi saa 1 jioni eneo la Namanga, Oysterbay katika eneo la taa za kuongoza magari.
Akiendesha gari lenye namba za usajili T 573 BQV, Corona Primio, kutoka Msasani kwenda yMorocco, alikaidi utaratibu wa trafiki huyo wa kuruhusu magari kupita kwa awamu kwa kulazimisha kupita kabla hajaruhusiwa.
Koplo Cyprian pengine kwa lengo la kuepusha magari kugongana na kutaka kuchukua hatua ukaidi wa Bernard, alilazimika kumzuia asipite lakini, bila kujali wala woga, aliendesha gari lake na kumgonga katika mguu na kumsukuma.
Mshuhuda walioshuhudia tukio hilo walisema askari huyo aling'ang'ania gari hilo hadi madereva wengine walipomuokoa kwa kulizuia gari la kijana huyo baada ya kusimama mbele ya gari lake.
Baada ya madereva wengine ambao nao walikuwa wakisubiri kuruhusiwa kupita katika taa hizo kukerwa na kitendo alichokifanya Bernard kumugonga kwa makusudi.
Watu wakiwa na hasira nusura wamshushie kipigo mtoto huyo lakini, askari huyo liwasihi wasifanye hivyo bali waiache sheria ichukue mkondo wake.
Madereva hao walitii kauli ya askari huyo aliyekuwa akichechemea na kulia kwa uchungu kutokana na maumivu makali kutoka katika mguu
Polisi wa kituo hicho walifika katika eneo hilo na kumchukua mzobemzobe mtoto huyo hadi Kituo cha Polisi Oysterbay, na habari zaidi zinasema baadaye aliachiwa kwa dhamana kwa sharti la kutakiwa kuripoti kituoni leo.
Kamanda wa Jeshi la polisi, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Bw. Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba koplo Cyprian alipelekwa Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu.
Kamanda Kenyela alionesha kusikitishwa na kitendo hicho cha mtu kudhani kuwa yuko juu ya sheria.
"Nimesikitishwa na kitendo hicho, mtu anaamua kutokufuata sheria za
barabarani na kudharau kazi ya askari wakati wa kutekeleza majukumu yao.
"Kijana huyo amekamatwa na anahojiwa na polisi, tuiachie sheria ichukue mkondo wake na kuamua cha kufanya kuhusu kitendo hicho cha uvunjifu wa sheria kilichofanywa na kijana huyo wa Lowassa," alisema Kamanda Kenyela.
Askari wa vyeo vya chini wameonesha wasiwasi kuhusu hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi ya mtoto huyo wa kigogo wakidai, kumekuwa na kawaida ya vigogo kulindana na haki ya mtu
hali ya chini.
Mmoja ya askari ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini alisema kwamba ana uhakika tkuwa mtoto huyo atalindwa, hatafanywa chochote, zaidi kulazimishwa askari huyo kumsamehe
Chanzo majira, march 31 2011[/QUOTE
Habari ya 2011 mnaleta leo huku ni kutupuuuuuuuuza jamani na kutukoroga
Acha kubwia unga issue hii ni ya mwaka 2011.historia.
Ama kweli Lowasa kashika akili za watu! kwa niniunadhani kasingiziwa ? and mind you hii ilikuwa 2011! maana ingewa sasa hivi mngesema ooh wanataka mchafua mgombea wetu. Kama wapambe wake ndio wenye akili za namna hii. zenyew ukatiliwa namna hii. Kumtaka mtu atakaekuja tutembelea vichwani pamoja na watoto wake. No way! sema BIG NO to LOWASA!Watamfanya nini? Chenge aliua faini yake chini ya milioni itakuwa huyu traffic officer ambaye hakutaka kupisha gari? Labda utokee mujiza. Kule Arusha si polisi waliua raia wasio na hatia pamoja na kuwapiga wananchi. Hii nchi ina wenyewe nyie wengine mmesingiziwa tu.